Makapuku Forum

Makapuku Forum

SEHEMU YA 07

......Niliomba ruhusa ya wiki moja kazini nikakubaliwa. Kama tulivyoada safari ilitimu siku ya siku kwenda jijini Arusha kwa kina Zai kutafuta ridhaa ya kuishi naye. Niliamini huo utakuwa mwanzo mzuri wa maandalizi ya kufunga ndoa na binti yule wa ndoto yangu aliyechengua akili yangu. Lakini ajabu nilichoenda kukikuta kwa kina Zai kilinishangaza sana na sikutaraji hata kidogo. Sikuamini macho na masikio yangu hakika nilishangazwa mno.
Kwanza ni aina ya mapokezi punde tulipofika. Ilionesha wazi tayari ujio wetu waliutarajia ingawa Zai hakunambia kuhusu hilo. Tulipokewa vizuri na kukaribishwa kana kwamba tayari walishatambulishwa mimi ni nani. Nilikarimiwa na nduguze wakiongozwa na bibiake Zai aliyekuwa mcheshi sana. Sikupata tabu ya kujitambulisha zaidi walinitoa hofu na kunambia taarifa zangu wanazo muda mrefu na walikuwa wananisubiri kwa hamu. Hii ilinishangaza sana hususani pale nilipoambiwa wameshaandaa taratibu zote na siku inayofuata wataniozesha. Hapo ndipo nilipozidi patwa kiguguziko. Nitaoaje ghafla vile? Yaani sijajiandaa kipesa wala kivyovyote? Hata ndugu yangu mmoja hajui? Hapana. Akili iliweka ngumu lakini moyo ulilegeza.
"Usiwe na hofu wala mashaka mwanangu. Binti yetu ameshakutunuku na sheria ya imani yetu hatuwezi kuwaacha mkakae kiholela. Kwa kuwa mmeridhiana nawe umetuhakikishia unampenda basi kaa tayari kesho jioni tutakuozesha na utaondoka nae akiwa mkeo rasmi. Usiwaze kuhusu pesa na sherehe hiyo itakuwa juu yenu kwa wakati wenu. Jisikie amani." Maneno ya baba niliyetambulishwa kuwa ndie mjombaake Zai yalipenya masikioni na kujenga taharuki.
"Mbona Zai hakunambia kama safari yetu inahusisha ndoa moja kwa moja?" Nilijiuliza mwenyewe akilini na kubaki kuwa mpole.
Na hivyo ndivyo nilivyompata mke wangu kwa haraka vile tena kwa mahali ambayo sikufikiria kabisa. Kama sinema lakini ndivyo ilivyokuwa. Ilinigharimu elfu hamsini tu kutimiza mila na taratibu za kwao kabla keshoye jioni kuozeshwa. Ni kama ndoa ya mkeka nilivyostukizwa pasipo maandalizi binafsi. Ndoa isiyo kelele wa shangwe. Tulifunga ndoa ya kimya kimya. Zai alifurahi mno na kuniomba msamaha kwa 'suprise' aliyonifanyia nami sikuleta mzozo. Usiku tuliandaliwa chumba maalum na hiyo ndio siku nilipoutoa umwanamwali wa Zai. Purukushani ilikuwa kubwa ndani ya uwanja wa selemala. Mguu kusi mguu kasi nilimpanga ili nitoboe tundu lakini hakuisha kurusha mateke na kubana miguu. Ni kweli kabisa Zai alikuwa 'sild'. Mlango wake haukuwahi kutumika nami nikawa mtu wa kwanza. Nilivunja kikombe baada ya usumbufu wa muda mrefu nae akaipaza sauti ya wahka wa raha na maumivu.
"Nakupenda sana mume wangu naomba usije kunitendaaa." Sauti ya kideko ilitabaruku kinywani mwake huku machozi yaa kuukosa usichana wake yakichilizika mashavuni. Nilimbusu na kumhakikishia kuwa mimi ni mume sahihi kabisa wa maisha yake.
Tulikaa wiki moja kabla hatujarudi Dar. Tulifungashiwa zawadi nyingi na kupewa nasaha za kimaisha.
"Mkaishi salama Mungu awasimamie wajukuu zangu." Alitubariki bibi Zai baada ya kutuombea dua siku ya kuondoka. Tukiwa njiani ndipo niliwasiliana na baadhi ya ndugu wa karibu.
''Suprise anko. Nimetimiza amri ya mwenyezi Mungu.'' Huo ulikuwa ujumbe nilioutuma kwa kaka wa marehemu mama yangu. Huyo ndie alinilea na kunisaidia baaa ya wazazi wote kufariki. Nilimpenda sana naye hakuficha upendo wake kwangu.
''Unasema? sijaielewa meseji yako mjomba!''
''Namaanisha nimeoa mjomba.''
''He! acha utani wako Hussein. sema kweli.''
''Ni kweli mjomba nimetaka kuwafanyia suprise tu ila shughuli zote naomba zifanyike kwako. Tupange siku.''
''Mmmmh! ina maana umeoa kweli au unataka kuoa?''
''Nimeoa mjomba. Nitakuja na mke wangu umuone tuzungumze na tupange shughuli nzima.'' Baada ya majibizano ya ujumbe mfupi na mjomba nilimtaarifu na rafiki yangu wa karibu ambae tulikuwa wote siku ya kwanza kumuona Zai Arusha. Nae hakuamini hata kidogo hadi nilipomsisitizia na kuongea na mke wangu. Mwishowe ndugu wote walipata habari, tulikaa vikao na ikapangwa tarehe ya tafrija na pongezi kwa kuingia katika ulimwengu wa 'watu waliokubuhu'.
Siku ya siku ilifika. Sikumbuki tarehe wala mwezi lakini naikumbuka vizuri ile siku. Siku ya tafrija na pongezi iliyofanyika kwa mjomba. Waliokuwa nje ya familia walijua ndio nimeoa siku hiyo. Ndugu wengi walifika na tukapewa nasaha na pongezi kwa kutimiza amri ya Mungu. Lakini ulipofika muda wa kupiga picha za kumbukumbu ndipo kuna tukio lilinishangaza kidogo. Alikuwa ni babaangu mkubwa ambaye aliishi nje kidogo ya jiji. Yeye alikuwa mganga wa kienyeji. Alichonishangaza ni lile jicho alilomtazama mke wangu kwa muda mrefu sana na kutoonesha uchangamfu hata alipochangamkiwa. Alishindwa kulistara jicho lake la utuuzima. Hata mke wangu alijistukia nami ghadhabu kunitambaa nafsini na kuniwasha kama chavichavi. Nilijibalaguza kwa kukenua meno mara kwa mara ingawa nilichukizwa na hali aliyoionesha baba mkubwa. Baada ya heka heka za mchana kupita usiku uliingia. Watu wengi walipungua na ndugu wachache tulilala pale. Asubuhi na mapema nakumbuka baba mkubwa aliniita faragha pindi alipojiandaa kuondoka na kuniuliza maswali yaliyonishangaza tena.
“Hivi Hussein mbona unafanya vitu kwa kukurupuka sana?”
“Mh! kivipi baba?”
“Hujui? kweli hujui na sikuzote achelewaye kujua hujua baada ya kuungua.”
“Baba! mbona sielewi unachosema. Nifafanulie”
“Umeoa na wengi wamekupongeza. Nilipoipata habari sikulaumu sana lakini nilipoiona habari yenyewe ndio nimekushangaa sana. Sijui kwanini umeoa mtu tofauti na Mariam." Aliposema hivyo ndipo picha ilipojengeka kichwani mwangu. "Anhaa! kumbe ndio maana alimtazama kwa jicho la chuki mke wangu?" Akili ilinipasha kichwani.
"Ni hivi baba! huyu mwanamke ndie chaguo la moyo wangu na Mariam nilishamsahau muda mrefu sana. Sasa sijaelewa tatizo lako nini baba hadi unanilaumu na kunitoa akili." Nilinena kwa rabsha kiasi. Ba mkubwa alinitazama na kutikisa kichwa kwa kunisikitikia.
"Hivi huyu binti unamjua vizuri? kabla hujenda kuoa ulishawahi kuishi nae japo miezi miwili mitatu?” aliniuliza. Swali lake lilinibabaisha kujibu na kujikuta namuuliza yeye swali kwa sauti ya kisirani.
“kwani vipi baba?”
“Hapana. Nimekuuliza tu kwakuwa hukutwambia mapema kama ulishaachana na Mariam na unaishi na mtu mwengine. Lakini pia naamini kwamba umekurupuka na huyu binti si chaguo sahihi kwako."
"He! baba naomba ishia hapo. Mbona bado una imani potofu ya kuchaguliana mke? Mimi ni mtu mzima baba nimekua najua zuri na baya. Namjua vizuri mno mke wangu naomba usije muhisi vibaya tena tafadhali sana baba sipendi kukuvunjia heshima." Nilijikuta mdomo ukikosa staha na kuongea kwa sauti ya mtetemo. Moyo ulitibuka kwa maneno ya maudhi toka kwa ba mkubwa.
“Basi nisamehe mie baba kama unamtambua vizuri mkeo. Ila nimetamani kukuhadhari kwa kuwa najua mchuma janga hula na wa kwao, kumbuka heri ya mjinga anayejifunza kwa kutenda makosa kuliko mpumbavu anayesubiri makosa yamtende.”
Ba mkubwa aliongea kwa sauti ya chini ya msisitizo kabla hajaondoka pale faraghani akiniacha nimesimama kama asakri gadi. Nilisonya na kupiga hatua kurudi ndani pasipo kuyatafakari maneno yake. Siku hiyo nilimpuuza ba mkubwa kuliko siku zote.
Niliporudi ndani niliificha hali ile machoni mwa mke wangu.
"Vipi baba anasemaje?" aliniuliza mke wangu.
"Aah! ameniaga tu na ametualika tukamtembelee kwake tukipata nafasi." Nilimdanganya nae akaonesha kuniamini. Na jioni ya siku hiyo nasi tulirejea kwetu kwa usafiri wa kukodi na tulisindikizwa na baadhi ya ndugu.
Hatimaye maisha ya ndoa yalichipua baina yetu. Ndoa iliyojengenga kwa misingi ya amani, upendo na heshima ndani ya nyumba. Siku zote nilimshukuru Mungu kwa kupata mke bora na mwema kama yule. Hakuchoka kunionesha wema kwa vitendo. Heshima, upole, imani na kila zuri alilopaswa kuwa nalo mke bora alikuwa nalo Zai. Hakika aliniloga kiakili siku baada ya siku nikazidisha upendo na imani juu yake. Tabia yake ya kupenda sala aliniambukiza nami taratibu nikawa sio mgeni msikitini. Pombe na sigala nilijikuta naziacha kwa hiyari yangu baada ya nasaha za mke wangu. Kazini nako nilipandishwa cheo na nuru njema iliangaza kwenye ndoa yetu. Rasmi niliukubali ule msemo kuwa 'nyota njema huonekana asubuhi'. Hakika mke wangu alikuwa kila kitu kwenye mawazo yangu. Ushauri wake mara zote ulikuwa mzuri na kuleta maendeleo. Hakujenga marafiki mtaani wala maadui. Alipendwa na kila mtu lakini hakuna aliyemzoea zaidi ya mimi mumewe. Starehe yake ya ziada alipenda kusoma vitabu hususani vya dini. Kwa miezi michache tu baada ya kumuoa Zai tuliweza kununua kiwanja maeneo ya Kigamboni jijini Dar. Hii ilizidi nijengea hamasa na furaha siku zote na kujiona mimi ni mwanaume mwenye bahati zaidi duniani. Nilifanya kazi kwa bidii siku zote. Mke wangu ndie akawa mtunza fedha pia msimamizi mkubwa na mfatiliaji kule Kigamboni kwenye kiwanja chetu na taratibu tulianza kujenga. Hakika maisha yalivyoninyookea baada ya kuoa sikuisha kutabasamu ingawa kuna muda nilisikitika nilipomkumbuka yule mlemavu ambaye maneno yake niliyakubali awali baada ya kutendwa na Mamu.
"Wanawake ni wauaji?! ha ha hapana yule bwana alikosa bahati tu lakini wanawake si wauaji." Hivyo ndivyo nafsi yangu ilinambia na kuamini kwa siku zote hizo kabla karata dume ya maisha yangu kubadilika ghafla na kuwa garasa.
Aksanteh mkuu
 
Mtaasisi, nilitingwa ile mada yetu vipi uiandalie siku kabisa ili at least tuwe japo na saa moja au 45 minutes za kuijadili na inakuwa ni kama segement lets say baada ya magazeti na Historia.

Ili jioni unakuwa ni muda wa kusogoa na ishu za hapa na pale
Sawa mtaasisi hoja yako imepita bila kupingwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom