Obe
Platinum Member
- Dec 31, 2007
- 10,282
- 35,645
Anaumwa ujue nimemuomba tukamuone naomba twende wote
..lol! Njoo peke yako, huyu ukija naye hachelewi kula vya mgonjwa.
Anaumwa ujue nimemuomba tukamuone naomba twende wote
Nimemwambiaa..lol! Njoo peke yako, huyu ukija naye hachelewi kula vya mgonjwa.
Binamu anapanga kuja kukuona mama mchuchu naona dawa yako sasa inaanzaa kukoleaa
Basi wajiangalieVipapaiii jee
Tunaendelea vizuri Tunamshukuru Mungu
Amen mama mchungajiHakika
Inaonekana unamjua vizuri sana..lol! Njoo peke yako, huyu ukija naye hachelewi kula vya mgonjwa.
Asante Lee hadithi nzuri ubarikiweSehemu ya 04..
Ilipoishiaa
"Lol! kumbe hilo ndilo lengo lako? kujizungusha kote sijui nimekuota sijui nini lol! samahani kakaangu naomba usipoteze muda wako na umwambie huyo aliyekutajia jina langu kuwa siko hivyo. Hiyo ndoto haipo na kutokea usahau...Kwaheri." Aliniaga baada ya kunishua na kuondoka huku kijungu chake mnato kikitingishika kimadoido. Nilijaribu kumzuia ili anisikilize zaidi lakini Zai hakusimama hata nilipomshika mkono aliuputa. Sikuwa na jinsi ilibidi nami nigeuze huku nikijilaumu upande wa pili kwa kuwahi kumwambia vile kabla hata sijamuweka karibu zaidi.
* * * * *
Zilipita wiki mbili nikijitahidi kumjenga Zai kwa njia ya simu bila mafanikio. Kila siku nilimtumia ujumbe asubuhi 'umeamkaje' mchana 'umeshindaje' na ile ya 'usiku mwema' kila jua lizamapo. Ingawa sikujibiwa hata meseji moja lakini nilifarijika kuona zinafika na kupokelewa. Sikuchoka kujishusha zaidi na kuomba radhi kama nilichofanya ni kosa kwake hata kumtaka basi tuwe marafiki wa kawaida tu hata kwa kupitia mtandao ingetosha kama hatotaka tuonane tena. Lakini pia niligonga mwamba kwa kukosa majibu. Nilimtumia jumbe mbalimbali za vituko na vichekesho lakini bado alizidisha mikausho mikali.
Baada ya muda nilianza kukata tamaa na kumsahau pole pole. Lakini nakumbuka siku moja majira ya usiku nilipokea 'sms' iliyotoka kwa Zai ambayo aliandika kuwa anahitaji kuonana nami. Nilistaajabu hasa alivyosema safari hii alihitaji aje ninapoishi. Sikuamini nikihisi alikuwa ananikejeli ingawa nilimjibu na kumuelekeza ninapoishi. Aliniahidi asubuhi yake ingefika na kweli keshoye mapema asubuhi alinijuza kuwa yuko njiani. Hapo ndipo nilipoanza kuamini na kumhakikishia angenikuta kituo cha basi namsubiri. Ingawa nilijua nahitajika kazini lakini nilijikuta naua kazi siku hiyo na baada ya kumaliza kuchati na Zai nilituma ujumbe wa uongo kazini na kuwambia kuwa nisingefika kutokana na kufiwa na jirani yetu. Na kweli haikuchukua muda asubuhi ile Zai alinipigia kuwa alishafika kituoni. Nilimuwahi na kumkuta mtoto amesimama kama jike la twiga akiwa kavaa gauni lefu na mtandio uliofunika vyema kichwa chake. Tulisalimiana na kuishika njia ya ninapoishi huku moyoni nikiwa siamini kabisa kama kweli huyu ndie Zai yule yule aliyeninyali siku ile. Nilitamani kumuulizaali muda ule kwa shauku kama ndio nimekubaliwa ombi langu au kuna lengine tena ! Lakini nilijikataza nafsini nikiilazimisha subira ingawa kuna muda nilijiuliza kaswali kengine ka uzushi kuwa hivi huyu binti Zainabu ni binaadamu wa kawaida kweli au isije kuwa ni jini linanifanyia mchezo..!!
Nilimuangalia pindi tunaingia 'ghetto' na kukaa kimagutu sebuleni mara baada ya kumuhudumia kinywaji alichohitaji na kufungua maongezi. Lakini ajabu nilishangazwa zaidi na kile alichokuwa anaongea Zai siku hiyo na kubaki na bumbuwazi zito sana kwa kutoamini nisikiacho Daaah!!... Unajua alisemaje..?
Zai alinsema hivi..
“Kiukweli kwanza naomba nisamehe kwa kutopokea simu yako wala kujibu meseji zako, lakini napenda ujue kuwa nilikuwa nafikiria sana swala lako kwani sijawahi kuwa na mwanaume japo nakutana na majaribu ya kutongozwa mara kwa mara. Na huku Dar nilichofata ni masomo tu na ndivyo nilivyoapa ila sijui imakuaje nimetokea kukufikiria sana na leo nimeamua kuja ili nikuhakikishie kuwa nimekubali niwe wako lakini kwa masharti matatu..”
Alinyamaza nami nikatumia nafasi ile kumeza mate na kukaa vizuri. Niliganda kama sanamu ya bisimini nikimtazama kwa makini nikionesha utayari wa kusikia hayo masharti ambayo nilishafuta pingamizi nafsini ingawa nilitaka tu kuyajua.
“sharti la kwanza naomba tusikutane kimwili mpaka utaponioa..."
Aliongea huku akinikazia macho nami nikatikisa kichwa juu chini juu kwa ishara ya kukubali na kumruhusu aendelee hilo sharti lengine.
"Lapili nipe muda nisome usinipigie simu ovyo hadi nikutafute mimi na kila mwezi tuonane mara moja tu tena maongezi yetu yasichukue zaidi ya nusu saa" Aliniangalia jinsi nilivyokuwa tuli namsikiliza.
"Na la mwisho uniapie kuwa hutokutana kimwili na mwanamke yeyote hadi utaponioa..”
Alimalizia Zai huku akinikazia macho nami bila kisito wala maswali nilimtoa hofu na kumhakikishia.
“Ondoa shaka kabisa mke wangu mtarajiwa niko tayari kufata masharti yote hayo na nakuapia sitokuja kuvunja hata moja niamini. Hata kama kuna mengine we niongeze.”
Alinyanyuka Zai na kunikumbatia lakini ajabu nyengine nilipomtazama machoni nilishangaa kuona anatokwa machozi.
“Vipi mbona unalia tena?”
“hamna ni mapenzi tu.. Nakupenda sana Zungu”
Sauti yake ya huba ilipenya zaidi masikioni mwangu na kunigandisha ubongo pindi aliponiita jina la Zungu. Niliganda staajibikoni kwani lilikuwa ni jina langu la utani enzi niko shule ya msingi sasa sikujua kalijuaje wala sikumbuki kama niliwahi mtajia mtu jina hilo na mbona ni miaka mingi mno hata kazini hakukuwa na mtu aliyenijua kwa jina hilo tena hata mwenyewe nilishalisahau. Nilitaka kumuuliza lakini nilijikuta napotezea na kusahau kwa pumbaziko la kumbato la huba na binti yule lililodumu zaidi dakika kumi. Baada ya maongezi machache ya hapa na pale ndipo aliponiaga nami kumruhusu bila kinyongo nikiwa mwenye furaha isiyo kifani.
Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa ukurasa wa kitabu changu kipya cha ulimwengu wa mahusiano. Kitabu kilichopambwa na kasha zuuuuri la mapenzi ya dhati lililonakshiwa kila aina ya mvuto na kumpendeza yeyote akionacho kitabu hiko na kutamani kukisoma bila kujua kuwa ndani yake kuna kurasa zenye maandishi mazuri yenye maana mbaya iliyofichwa na misamiati migumu sana yenye kuumiza. Daaah!! laiti ningejua nisingeendelea kusoma misamiati hii na kuipuuza bila kujua maana yake. Na Laiti ningefunua kwanza nyuma ya kitabu kujua fasiri yake nadhani kitabu changu ningekisoma kwa tahadhali na umakini mkubwa ama nisingekinunua kabisaaa. lakini Mwe! Tafsiri niliyoikuta kwenye kurasa ya mwisho imekuwa matokeo tu ya haya niyaonayo baada ya dharau yangu ya kutosoma hata dibaji na kukimbilia kusoma nisiyoelewa maana kiundani nikifurahia kwa kukodolea picha za michoro mizuri kwenye zile kurasa bila kujua siri na maana yake. Na nilipomaliza kufunua kurasa ya mwisho kulipofafanuliwa maana nikawa nishachelewa saaaanaa. Daaah!! Aaaaaaaaahh!… Amini usiamini baabaaa..... WANAWAKE NI WAUAJI.
*||*||*||*
Sauti ya jitimai ilikinai kusimulia hadithi ile ndefu ya maumivu. Kumbukizi zilimfanya mzee msimuliaji machozi kutabaruku machoni pasipo hiyana. Kimtazamo hakupungua miaka hamsini akiwa ameketi akifarijiwa na kijana aliyeketi jiraniye. Huyo ndiye alikuwa Hussein baada ya miaka mingi kupita. Mengi yalimsibu kwenye maisha yake hata kujikuta akishindwa zuia machozi punde kila aliposimulia mkasa wa kweli wa maisha yake. Ilikuwa kazi kwa kijana msimuliwa kum-bembeleza na kumfariji mzee yule. Wakiwa pembezoni mwa fukwe maarufu ya SUN RISE iliyokuwa Kigamboni jijini Dar es salaam. Lakini alipofikia pale mzee Hussein alinyamaza na uso wake ukizidi lowanishwa na machozi na mwishowe kilio cha kwikwi kilimponyoka.
* * * *
<<<---->
(MIAKA 8 NYUMA)
HATUA ZA
> SHAABAN MWINCHANDE <
----------------------------------
-------------------------------
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa familia ya mzee MWINCHANDE baada ya kijana wao wa pekee aliyeitwa SHAABAN kuhitimu elimu ya juu. Baada ya pongezi na sherehe kuisha siku hiyo Shaaban alikaa na mzee wake kwa mazungumzo juu ya hatua itayofata kuhusu elimu aliyoipata huko Nairobi Kenya alipokuwa kimasomo zaidi ya miaka mitatu.
“Mwanangu nimefurahi umefaulu vizuri na umerejea salama lakini bado narudia tena sikufurahishwa na kile ulichoenda kujifunza. Imani yangu ipo pale pale kwa elimu hiyo haitokusaidia hapa nchini kwetu labda ungekuwa ulaya.”
“Kivipi baba? Mimi ndiye mwenye chaguo tena kutoka moyoni. Naipenda sana elimu ya saikolojia na maisha ya viumbe na ndio ilikuwa ndoto yangu ambayo sasa imetimia.” Shabani alisimama kwenye imani yake ambayo ilikinzana na babaye mara kwa mara.
"Sawa baba. Kwa kuwa unaamini hilo basi subiria kazi." Alifunga maongezi mzee Mwinchande na kuingia ndani.
Siku zilipita baada ya tafrija Shaaban alianza mizunguko huku na kule kutafuta kazi juu ya kile alichokisomea lakini mambo yakawa kama vile alivyoambiwa na baba yake. Hakukata tamaa aliendelea kupwiyanga hatimae mwaka ulikatika bila kufanikiwa.
Babaye alijaribu kumshauri ajiunge na jeshi lakini Shaaban alipinga na kuamini taaluma yake ya elimu ya Saikolojia na mahusiano ya maisha ya viumbe. Alipokosa ajira aliamua kujiajiri kwa kufungua ofisi binafsi lakini bado kwa hali ya Tanzania hata hao wahudumiwa hawakuwa na elimu wala imani ya matatizo ya saikolojia. Kwa kipindi kilefu aliweza kujitolea tu mashuleni na kwenye semina kutoa elimu kwa watu kuhusu matatizo ya saikolojia na maisha lakini bado hakukuwa na cha maana kikubwa alichokivuna zaidi ya kupigiwa makofi ya hapa na pale, kula misosi ya semina na kuendelea kuwa tegemezi kwao.
Hali hiyo mwishowe ilimchosha Shaaban na mwishowe alikuwa mpole na kumuomba msamaha babaye.
"Nimekiri baba mawazo yangu hayakuwa sahihi kwa kile nilichokiamini. Niko tayari kukusikiliza baba na kufanya kile nilichopinga mwanzo. Naomba uniunganishie nafasi ya jeshi niirithi kazi yako tu." Maneno ya Shaaban yalimfurahisha zaidi mzee Mwinchande ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa jeshi la magereza miaka ya nyuma.
“Usijali mwanangu nilitegemea siku moja utakuwa upande wangu tu. Sasa kutokana na elimu uliyonayo itakusaidia kupanda vyeo jeshini na wiki ijayo nitakupeleka makao makuu kwani mwezi ujao ndio usaili utaanza. Usiwaze naamini pia huko utapata nafasi ya kuitumia kazi yako kwani kuna mengi sana kwa wafungwa.”
Aliongea mzee Mwinchande na safari hii Shaaban hakuwa na pingamizi japo awali hakutaka kabisa kuja kuwa askari magereza kazi aliyowahi ifanya babaye.
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari ya Shaaban ndani ya jeshi la magereza baada ya kujiunga na kwenda mafunzoni mwishowe akawa askari rasmi. Kutokana na juhudi na elimu yake haikuchukua miaka mingi mbele alipandishwa vyeo na kupanda ngazi kwa haraka hadi akawa Kamishna baada ya miaka mitano tu.
Mwaka mmoja baadae akiwa kamishna alihamishwa na kupelekwa kwenye gereza moja lililohusisha wafungwa wa makosa mazito mazito. Huko alishika wadhifa wa juu kabisa mara baada ya mkuu wa gereza lile kuugua na kufa ghafla. Na huko ndipo alipokutana na kisa cha mfungwa aliyekuwa pale kwa zaidi ya miaka ishirini na tano akijizolea umaaarufu jela kwa jina la HUSSEIN BABU BUBU alilotungwa na wafungwa wenzake kutokana na kuwapo gerezani kwa muda mwingi na kutopenda kuongea. Kituko kikubwa zaidi alichokuwa nacho mbali ya kutopenda kuzungumza wala kujichanganya na wenzake na muda mwingi anapotulia hutumia kuandika maneno ya ajabu ajabu na hata kwenye kuta za jela alitumia mawe kusugua na kuandika japo alishaadhibiwa sana na kuteswa juu ya swala hilo lakini hakukoma kwa miaka yote ile. Yalikuwa ni mazoea yake na aliharibu kuta nyingi kwa michoro yake na maneno ya ajabu kama mtu aliyechanganyikiwa na alihukumiwa pale kifungo cha maisha kilichotokana na kesi iliyomkabili ya mauaji.
Kilichomshangaza zaidi Kamishna Shaaban ni baada ya kufatilia michoro ya huyo mfungwa na alipoichunguza zaidi kwa uyakinifu aligundua kuna maneno ndani yake yaliyosomeka 'Wanawake ni wauaji’ Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kamishna Shaaban kumtafiti na kumchunguza huyo mfungwa akianzia historia ya mafaili yake hadi kuhukumiwa na kuletwa pale huku moyoni Shaaban akiapa lazima atafute jinsi ya kuongea na huyo mtu kwani maneno yake yalionesha yana siri nzito na maana kubwa kwenye maisha yake.
Nisamehee ila sijasema kwa nia mbayaUsiseme kwa sauti ukaniharibia masharti mjomba
Serious Obe! Pole sana nakuombea nitakuja
Nitaenda naeAende peke yakee
Amen karibu
Kwema
Mama mchungaji leo umenunua kesi, ila kwa wewe tumekusameheAsante Lee hadithi nzuri ubarikiwe
Salama kabisaHabari ya uzima mkuu
Leo naona uko vizuriSalama kabisa
We acha tuKwema mkuu naona siku hizo unaonekana mda wa majeruhi