Makapuku Forum

Makapuku Forum

5ce986308e7d53bbfcdad0d249df1368.jpg
Na bado hawajatetereka wamefika mahali wana nyumba zinahimili na kupunguza Athari za maafa huku kwetu tunafahamu kabisa maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kukumbwa na matetemeko mafuriko lakini hata uokoaji ni duni leave alone materials zinazotumika kujenga infact hatujifunzi!!
 
Umaarufu wa mtu au uzi unarokana na kilichoandikwa na siyo wingi wa like alizonazo mtu
Yaani maneno yako ndo hukaa moyoni kwa mtu likes zako hukaa kwenye profile tu pengine kwenye list ya Top 20

Pia uzi unaweza kuwa na post nyingi kila siku lakini ukafuatiliwa na wachache yaani Kusubscribe mfano nyuzi za The Bold zinafuatuliwa sana kule Jukwaa la Intelligence

Mtu unaweza kuwa na post nyingi na kuwepo kwenye list ya most posts lakini ukazidiwa umaarufu na asiyekuwepo kabisa kwenye list

Mtu unaweza kuwa na maLIKE mengi pengine kunizidi mimi lakini usiwe maarufu

Kwangu mimi hii thread imenisaidia kujifunza mengi pamoja na kupata marafiki wengi hadi kushirikiana nje ya JF.....
Hivyo uzuri wa thread ni kile kilichomo/kinachoandikwa na siyo wingi wa post
..........
Uko sahihi mkuu, ila binafsi naona uzi maarufu ni ule uliofuatiliwa sana na kuchangiwa na watu wengi! Kwa sasa sasa nadhani hakuna kama Makapuku! Umaarufu wa mtu ni tofauti na umaarufu wa uzi japo vinategemeana... Ule uzi wa ma-likes unaweza kuwa maarufu ila hauwezi kutoa watu maarufu!
 
Japan na Indonesia zimo katika ile inaitwa "The Ring of Fire" yaani mipaka ambamo tectonic plates ama zinakutana (convergence zones) au zinaachana (divergence zones); na hata kupishana. Mabadiliko ya ghafla ya presha yanayotokana na misuguano ya plate tectonics hizi ndiyo husababisha mavolkeno makali na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara katika mataifa yote yaliyo katika ukanda huu wa moto. Na matetemeko makali yanapotokea baharini na kuinua sehemu ya bahari tunapata tsunami kama ile iliyoua maelfu ya watu mwaka 2004 Indonesia na ile ya mwaka 2011 iliyoharibu mpaka mitambo ya vinu vya nyuklia vya Fukushima kule Japan.

Wajapan pia ndiyo wanaongoza kwa teknolojia ya kupunguza madhara ya matetemeko haya. Maghorofa yao kwa kawaida huwa hayavunjiki wakati wa tetemeko bali hunesa nesa kama mwanamwali mrefu aendaye kwa mumewe. Na vifaa vyao vya kiseismolojia ni bora kabisa kiasi kwamba vinaweza kuhisi hata mmwagiko wa kifusi cha mchanga kinapodondoshwa na tingatinga, na inasemekana wapo karibu kugundua jinsi ya kutabiri kwa usahihi wa kuridhisha kuhusu utokeaji wa matetemeko hayo.
84f5e649b2f591cb7c55323cd60c82c8.jpg
 
We ongea tu mwisho povu namwagiwa mie Shem
Ohoooo

Wengine tuna za kunguni au ile misemo ya wahenga ya "kunya anye kuku akinya bata kaharisha"
Nunua overall la plastic ulitumie kujikinga na mapovu. Au kuwa ngangari tu shemu. Dunia hii ukiwa mnyonge mnyonge utaonewa sana!

Ikibidi tuungane tuwe tunapambana pamoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom