Makapuku Forum

Makapuku Forum

4d2290818acf55c6370b09970b9b3928.jpg
aisee
 
Umaarufu wa mtu au uzi unarokana na kilichoandikwa na siyo wingi wa like alizonazo mtu
Yaani maneno yako ndo hukaa moyoni kwa mtu likes zako hukaa kwenye profile tu pengine kwenye list ya Top 20

Pia uzi unaweza kuwa na post nyingi kila siku lakini ukafuatiliwa na wachache yaani Kusubscribe mfano nyuzi za The Bold zinafuatuliwa sana kule Jukwaa la Intelligence

Mtu unaweza kuwa na post nyingi na kuwepo kwenye list ya most posts lakini ukazidiwa umaarufu na asiyekuwepo kabisa kwenye list

Mtu unaweza kuwa na maLIKE mengi pengine kunizidi mimi lakini usiwe maarufu

Kwangu mimi hii thread imenisaidia kujifunza mengi pamoja na kupata marafiki wengi hadi kushirikiana nje ya JF.....
Hivyo uzuri wa thread ni kile kilichomo/kinachoandikwa na siyo wingi wa post
..........
kweli kabisa
 
Nitalipa hakika atoke dunia ya leo watu wanapenda vitu kuliko watu ukweli Mungu alituumba ili tupende na kupendwa ila mambo yamebadilika sana Mungu atusaidia after all hata hiyo bahati nasibu Mungu kakupa ndio mlango wa gereza umefunguka inabidi kusoma alama za nyakati Mungu hutumia watu kutufungua
ila mama mchuchu watu tupo tofaut kama ni mumeo mmeapa kwa shida na raha me naweza fanya jamaan
 
Uko sahihi mkuu, ila binafsi naona uzi maarufu ni ule uliofuatiliwa sana na kuchangiwa na watu wengi! Kwa sasa sasa nadhani hakuna kama Makapuku! Umaarufu wa mtu ni tofauti na umaarufu wa uzi japo vinategemeana... Ule uzi wa ma-likes unaweza kuwa maarufu ila hauwezi kutoa watu maarufu!
Upo sahihi....ila thread zote huanza kwa kasi zen hupungua taratibu na hata kupotea(sitabiri)

Mimi km mbunifu wa huu uzi sikubuni ili kupeana malike bali kupeana "maujanja* na kudumisha urafiki kutokana na watu kukosa sehemu moja ya kukutana
Like zilianza km utani tu wa baadhi ya watu wa mwanzo na kugeuka mazoea!!!

Ila kila mtu afanye lake
............
 
Na bado hawajatetereka wamefika mahali wana nyumba zinahimili na kupunguza Athari za maafa huku kwetu tunafahamu kabisa maeneo yenye uwezekano mkubwa wa kukumbwa na matetemeko mafuriko lakini hata uokoaji ni duni leave alone materials zinazotumika kujenga infact hatujifunzi!!
Hatuna mipango
Tunaishi kwa mazoea
.....
 
Japan na Indonesia zimo katika ile inaitwa "The Ring of Fire" yaani mipaka ambamo tectonic plates ama zinakutana (convergence zones) au zinaachana (divergence zones); na hata kupishana. Mabadiliko ya ghafla ya presha yanayotokana na misuguano ya plate tectonics hizi ndiyo husababisha mavolkeno makali na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara katika mataifa yote yaliyo katika ukanda huu wa moto. Na matetemeko makali yanapotokea baharini na kuinua sehemu ya bahari tunapata tsunami kama ile iliyoua maelfu ya watu mwaka 2004 Indonesia na ile ya mwaka 2011 iliyoharibu mpaka mitambo ya vinu vya nyuklia vya Fukushima kule Japan.

Wajapan pia ndiyo wanaongoza kwa teknolojia ya kupunguza madhara ya matetemeko haya. Maghorofa yao kwa kawaida huwa hayavunjiki wakati wa tetemeko bali hunesa nesa kama mwanamwali mrefu aendaye kwa mumewe. Na vifaa vyao vya kiseismolojia ni bora kabisa kiasi kwamba vinaweza kuhisi hata mmwagiko wa kifusi cha mchanga kinapodondoshwa na tingatinga, na inasemekana wapo karibu kugundua jinsi ya kutabiri kwa usahihi wa kuridhisha kuhusu utokeaji wa matetemeko hayo.
84f5e649b2f591cb7c55323cd60c82c8.jpg
Shukrani kwa somo
......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom