Asante sana mdau Shimba, kuandika ni 'hobby' na ninafurahi na kujiskia vizuri kuwa sehemu ya familia hii, Makapuku ambako kumejaa member wanaojitambua na kujali masiha yao na ya wengine bila kukereka wala kukereketwa.
Nikiingia humu huwa najifunza mengi sana tena ya msingi na yananifanya niwe na wakati mzuri nikaa kusaka mkate wangu na wa wapwa zako.
Hapo nilipopabold, ndo wanapokosea, ni kweli wapo watoto wa shule humu, JF ni kama kokoro... na unajua kokoro linaleta si samaki tu. Humu makapuku kuna watu wa fani zote na mada humu huwa zinaongelewa japo kiurahisi rahisi lakini ndo zinaeleweka vizuri sana.
Nikupe mfano mdogo tu, enzi hizo gazeti la Daily News lilikuwa linaandikwa kwa kiingereza kigumu hadi unajiuliza hawa waandishi ni maAnglo Saxon ama vipi? Yalipokuja mengine kama The Express, Guardian na mengine nikaona kumbe huna haja sana ya kuandika mabombastic ili uonekane unajenga hoja.
Hoja ni hoja pale inapoeleweka, na hili ndilo linalofanywa na Makapuku