Matusi hayo mkuu
Wachina wana kawaida kule kwao kuvunja/bomoa baadhi ya madaraja na flyover na hata maghorofa mfano baada ya miaka 100 na kujenga upya kabisa ili tu kuvipa nguvu viwanda vya vifaa vya ujenzi na kutoa ajira pamoja na kuzungusha pesa
Tutasubiri sana
........
Interesting!
Yaani hapo ndo sisi tumeshindwa kabisa, yaani tunafurahia kujaza mapesa mfukoni bil kuyazungusha. Yaani mtu kuanzia jtatu hadi jpili anakula kwake tu, hajui kama kuna mamantilie wametoa ajira.
Na trend inayoendelea sasa badala ya kuifanya private sector iajiri watu wengi kwa kuipa tender za serikali serikali inachofanya ni kutoa pesa kwenye mfuko wa suruali na kuziweka kwenye mfuko wa shati utasema kadi nyekundu. Huwezi kujenga uchumi kwa kukalia mapesa huku bank zikishindwa kukopesha.
Kwa serikali kutoonesha kutaka kushirikiana na sekta binafsi (kana kwamba yenyewe ndo muajiri mkuu) linaundwa kundi kubwa la watu wasio na ajira na hii ni hatari kwa afya.
wenzetu wanazipa sekta binafsi ushirikiano ili zitoe ajira na uchumi usimame sawasawa sisi tunakazana (kazana) kujadili jaza ujazwe, lipa ukatiwe yaani akili za kijinga kabisa.
Kwa kusikiliza mijadala ya kuanzia kwa rais hadi bunge, utagundua kuwa, mosi wabunge wetu wengi wako hai kuanzia kiunoni kushuka chini ( ndo mana utasikia, kikalishe, jazwa ujaze) na pale feri kwetu tunapofurahia harufu ya shombo pameoza kuanzia shingoni kwenda juu. Shingoni kushuka chini pako makini sana kama makanikia.
Asante sana mdau, yaani ulichoandika hapo juu wallah tena nasikitika kwanini bia zinazidi kuongezewa kodi ilhali kuna watu serikalini hawalipi kodi kwenye mishahara yao mikubwamikubwa