Wakati najisomeasomea elimu za darasani, nilivutiwa naye sana.
Hakujikita katika mambo hasi yanayomfanya mtu asifanikiwe, yeye aliamini kila mmoja wetu ana uwezo wa kufanikiwa kwa kuwa tu tuna vipawa tofauti, na hasa tukitia jitihada kuboresha maisha yetu. Aliandaa hii inayoitwa 'hierarchy of needs'.
Ili ufanikiwe, kuna ngazi lazima uzipande, na ngazi moja hufanya hamu ya kupanda zaidi.
Ngazi ya kwanza; Mahitaji ya kimwili na kiasili: Unahitaji kula , kunywa , malazi, kulala na kulalana. Physiological and biological needs
Ngazi II: Mahitaji ya kuwa salama, hapa anasema ili ufanikishe ndoto zako baada ya kuwa umeshiba kimwili na kiafya basi ni lazima uwe na uhakika wa usalama wako pindi unatekeleza majukumu ya kujitafutia kipato iwe shambani (kule kibiti /Rufiji ni ngumu), usiwe na hofu.
Ngazi ya III: Mahitaji ya mapenzi na kujinasibisha, hapa kila mmoja ana haki ya kupendwa, ukaribu (intimacy), kuaminiwa na kukubalika (love and belongingness)
Ngazi ya IV: Esteem needs , weee
Mondray hebu njoo uweke link hapa ili kujua kwamba kuna hitaji la kujithamini, kutojiweka chini
Na ngazi ya tano ni kujitambua wewe ni nani na unajukumu gani. Hii utaifikia baada ya kuwa umepitia ngazi zote hizo.
Labda tu kwa kuongezea hapa, kuna hitaji/motisha ya utambuzi. Ukiweza kutambua na kuelewa kupitia maarifa tofauti uhakika wa kufanikiwa ni mkubwa tofauti na ukiwa bwege mtozeni, utatoswa hata na wanasiasa wajinga wa mwisho. Soma soma, angalia news, pitia Makapuku nk
Pia kuna motisha ya kujiweka smart, ndo maana watu hawakauki gym kujenga mwili , kujipodoa ukapodoka (aesthetic needs), kutafuta kakitambi kaheshima kama nilikonako.
Na pia kuna motisha ya kuwasaidia wengine kufanikisha ndoto zao (transcendence needs) hapa ndo unakutana na waombeaji wote, walimu na wewe Kapuku unayesoma hapa.
Well, nimeandika sana eeh. Pole na asante kwa kumsoma
Mussolin5 na leo katika historia