Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

Maisha yangu mabaya sana nakaribia kujiua

afadhali wewe mimi sina hata ajira (yaani sehemu maalum ya kuingizia hela)..!!hiyo laki 2 naishia kuisikia tu kwenye biko,mahusiano kwangu ndo mtihani mkubwa(sina mpenzi wala nini) mara ya mwisho kutongoza nilijibiwa eti sina kitu eti yeye atanipeleka wapi Mimi!!sikumlaumu,sikukasirika kwa sababu alichokiongea asilimia 90 ni ukweli mtupu..!!hapa nilipo nipo mwenyewe tu sina chochote zaidi ya hii simu niliyonayo ambayo inanisaidia kupunguzia mawazo,nikiingia jamiiforums yah nahisi kufarijika sana..!!lakini sijakata tamaa mkuu nakaza kiume!!napambana siku zote..
cha msingi we elewa watu wako na matatizo kukuzidi wewe ila wanakausha tu kibabe!!na hawafikirii kujiua
 
Mshana ni kipimo gani cha chumvi kinatakiwa, na upatikanaji wa mafuta ya mizeituni ukoje I mean wp mtu anaweza pata.
Unakadiria kiwiko cha mkono ndoo ya Lita 20, mafuta yapo tuu
 
Mshana samahani hii chumvi unaiweka kwenye maji yakuogea moja kwamoja au unaoga Kwanza kwamaji yabila chumvi alafu ukimaliza ndio unachukua maji yenye chumvi unajimwagia? samahani nieleweshe hapo
Vyovyote ni sawa tu
 
Kataa hiyo hali ya mauti ndani yako,simama kwa miguu yako mlilie Mungu wako atatua shida zako! Kuwa na imani tu yote yatakwisha.
 
Mtafute Msabato karibu yako mwenye imani thabiti akujuze yakupasayo kufanya.
 
Ndugu zangu,

Kama nilivoandika kichwa cha habari mimi ni kijana niliye ajiriwa na mapato yangu kwa mwezi nikama 2000000 hivi.

Lakini nimekosa furaha kiasi kwamba sina furaha na maisha pamoja na watu wanaonizunguka hata hiyo pesa yote huishia kumaliza matatizo ya ndugu na kila mwanamke naingia naye kwenye mahusiano basi hata anza kuumwa kiasi pesa yote inaenda kumhudumia mgonjwa.

Sasa najiuliza nitakuwa nimerogwa au na kipindi hiki ndo nimekosa kabisa ujasiri wa maisha sasa je hiyo hali ya kawaida au kuna michezo ya kiswahili nafanyiwa na kama yupo mganga anitibie nikipona ndo namlipa maana nimeenda kwa hawa wa upako naona maigizo kabisa mtu ananiombea sijazimia ananilazimisha kuniangusha na wale wasaidizi wanashika kwa nguvu kama nina matatizo wakati nipo vizuri, ndo nikaona wote hawa maigizo.

Nimeenda kama kwa wa upako wa nne hivi wote hivohivo.

Sijui nifanye nini.

una serious psychological problem, kitaalamu wanaita Manic depression.
 
Back
Top Bottom