Maisha katika nyumba za kupanga

Maisha katika nyumba za kupanga

Kuna brother mmoja alipata chumba uswaz, sasa asubuhi alikaanga mayai mawili kwa breakfast, khe it was a talk of the house, anakunywa chai na mayai. Basi mkaka kuwakomesha akawa anapita kwa wauza chips anaomba maganda, asubuhi akishakaanga mayai yake mawili anatupa maganda kama ya mayai sita hivi, wee wa mama wanakaa kabisa kuhesabu maganda.
Brother ama ex-boy wako?
Mpe heshima yake bhana
 
Mh! Mi zilinishinda nyumba za kupanga, nimepigwa majungu sana nimesemwa sana lakini mistari ya Fid Q ndio imenisaidia "maneno mkuki hekima ngao"
Sahv nimeshajenga yangu
 
Kuna brother mmoja alipata chumba uswaz, sasa asubuhi alikaanga mayai mawili kwa breakfast, khe it was a talk of the house, anakunywa chai na mayai. Basi mkaka kuwakomesha akawa anapita kwa wauza chips anaomba maganda, asubuhi akishakaanga mayai yake mawili anatupa maganda kama ya mayai sita hivi, wee wa mama wanakaa kabisa kuhesabu maganda.
KAH! lolest.
 
ukipanga nyumba za wazaramo, wasambaa, waha , wapogoro, wamakonde zenye watu Wengi Mara nyingi wenye nyumba wanakuwaga hapo tegemea makelele
 
Kuna raha yake kuishi Tanzania in general, kuna siku Dar nilikwenda dukani, nilijikutua ninamahitaji mengi kuliko cash niliyokuwa nayo, nilimwambia kijana wa dukani niwekee hivi pembeni nitarudi kuvichukua, aliniambia hapa aunt chukua vyote wewe si unakaa nyumba ile yenye gate ... unatanipitishia hata kesho pesa yote. Kwanza nilishtuka sana, kumbe mtaani baada ya wiki mbili tatu watu wote wanakufahamu.
Utakuwa una kitu flani amazing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katika maisha yangu kinachonisumbua ni kupika,nimekulia kwenye familia ambayo hata kupika sijui tulikuwa tunapikiwa mpaka sasa nikienda nyumbani kuna msaidizi anayepika,nikiwa nyumbani nafua na kufanya usafi, kwa sasa nimepanga baada ya wazazi wangu kuhamishwa nikaamua kupanga ila najitahidi kupika ,lakini siwezi kupika inavyowezekana, natamani kwenda kusomea mapishi ...nimekuwa mtu wa kula matunda jion mchana nakula kwenye canteen..
Takuja kukufundisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
When In Rome,Do As Romans Do.
Uswahilini Kutamu. Mar Mtoto Anatolewa(Radhi Itakayomwagika Ni Ya Kiwango Cha Lami),Mara Kuna Kombe La Rede(Mibaba Mizima Na Ndevu Hukusanyika Kuangalia Vyupi Na Bikini,And Getting Glimpses Of Coochies,Sembuse Sie Vijana?),Mara Kuna Harusi,Kigodoro Siku 3,. Honestly Kuishi Huku You Feel Lively. Full Matukio,Hapa Juzi MSINGI KIUNO Waligombana Na USTAARABU ZIRO,Bas Kukawa Na Civil War Ya Kuchambana Na Kutiana Masingi,Na Mara Chache Kupigana (How Do They Solve It?Well Kuna Mechi Ya Rede Ikaamuliwa Ichezwe,Sasa Jiulize Kutoka Allegations Za Kuibiana Mabwana Mpaka Kuamuliwa Na Rede). Ghafla Mwingine Katalikiwa Hataki Kuondoka ,Mwingine Muuza Ngada Wazee Wa Pira Wanamsaka Anaishi Kama Phantom. Mimi Ni Ripota Wako,Juan Moses From CNN,
Uswahilini,Back To You Sky Esclat Hapo Studio.
This comment gave me a replay of my old street, down town mtoni kwa azizi Ali.

Mzee flani kapigwa roba mchana, mama flani kasutwa kwa matarumbeta, jamaa fulani kafumaniwa chooni na mke wa jirani, ni tukio baada ya tukio!

Cheap cookies zipo uswaz, ukiwa na elf hamsini you gon *** truck loads of them. Tena wakaliiii

From Tandale kwa tumbo, mbagala kwa mfuga nyoka, mpaka tandika kwa mchambia chupa.

Huwez kukosa cha kufanya uswaz asee.

Till next time, tukutane uswaz!

- KANA -
 
Kuna m-Jaluo mmoja wa Kenya alipata kazi kwenye kampuni moja mjini, basi alipangisha huku kwetu uswaz, sasa asubuhi anamuona baba mwenye nyumba anakwenda msalani na birika bovu hivi, yule jamaa alikuwa anataka sana kujua shughuli ya lile birika kule maliwatoni.

Siku moja alipanda juu ya mnazi anamlia timing mzee, mzee aliingia na birika akatawaza, basi m-Jaluo alienda kuhadithia wenzake ofisini, nyinyi watu ya TZ mnapiga deki m***ko.
Atiii?

Kwani hao hawachambi kwa maji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukipanga nyumba za wazaramo, wasambaa, waha , wapogoro, wamakonde zenye watu Wengi Mara nyingi wenye nyumba wanakuwaga hapo tegemea makelele

Ndio ninapoishi hapa Mwananyamala Qumamae...
Umeme mchana unazimwa. Ukitaka nunua wa 2000 watumie wote.
***** week ijayo nahamia Survey Mwenge.
 
Umenikumbusha shosti,nilienda kumuona shogangu tuliachana zamani sanaa baada ya kukutana nae akanikaribisha kwake
na alikua best yangu sanaaaa nikasema wavha weekend moja niende sasa kuelekezwa mpaka kufika ilikua shughuli,haya kufika wako wapangaji wenzie nikawa nimemchukulia zawadi,mara akatoa jiko kuanza kupika duu mara huyu anatoka anapiga msuwaki ,mwengine kavaa kanga moja anakwenda chooni sehemu ndogo,mwengine kawasha redio sauti kubwa,mama mwenye nyumba nae anaongea msijua kula vizuri tuu nakua na wageni wenye magari mjue nakulipa kodi nakufagia zamu ikifika,muache na kuchukua waume za watu manake hamna miko wengine hata anaewafadhili mnamchukulia bwana wake,mie nilibakia nimetoa macho na mijicho yangu ilivyokua mikubwa,nikamwambia shosti huku hamaa ntakusaidi kodi duu sijawahi kuona mama mtu mzima akiongea pumba kama yule....

Ya ukhty, nifadhili kodi na mie nihame huku, nafwaa
 
Back
Top Bottom