silwelachole
Member
- Jan 17, 2017
- 8
- 3
Uswalin kuna vituko!
Mi nakumbuka kipindi nimeenda likizo kwa uncle mwaka 2012 hapo ndo nikajua nyumba za kupanga ni shida
Kwanza nilikuwa na tabia ya kukojo bafuni aisee mke wa uncle akapokea michambo kuwa aje aniambie niache kukojolea bafuni,
Kilichokuja kuniacha mdomo wazi ni siku ambayo mama WINNIE aliingia sebuleni kwetu akaiba BLUE BAND NA MAZIWA YA NIDO ile anatoka tu akakutana uso kwa uso na mdogo wake na uncle aiseee kwa kutumia heshima na busara tukamstahi.
aisee siwaambii kilichotokeaTena ukiwa wa kisure hutaki kuzoena nao, mume wako anaweza kukuaga akalala nyumba ya pili na wote wanajua wanakung'ong'a wewe. Uswaz network ni muhimu sana.Nyumba za kupanga noma hapo sinza dada yangu alipanga akawa na house girl basi kuna sehemu unamwaga maji machafu yule house girl akamwaga kwenye ukute weeee baba mwenye nyumba kampa kichambo wewe huko ukuta ozesha wakati hata mshahara wako wa mwaka huwezi nunua hata kitanda tulichekaaaa
Uswazi komedy nyingi sana kuibiana waume na boyfriend kawaida
Na mashindano ya kuvaa nguo mpya + kusuka
Huyu mama aliniwacha HOI tena anachamba kama vile anamchamba mwanawe sasa hiyo nyumba yenyewe ni ya udongo ukumbini ndio wanapikia yani duu nilisema mwenyezi mungu nakushukuru kwakuniepusha maisha kama haya,choo cha makuti mlango hakuna wameweka gunia,chooni kumeota majani na uyoga yani we acha tuu...Nyumba zingine kuna vitimbi. Unaweza kuhama kwa siku moja Kama hujazoea haya mambo
..........wenye nyumba wengine wazungu japo mnaishi nyumba moja mnaweza msionane hata miezi.mnaishi Kama familia no makelele....
Kuna kaka mmoja alikuja kusoma UDSM, alipangisha chumba Tandale. Alikuwa na girl friend wake wa long time, mtoto wa kisure basi mtoto akawa anakwenda weekend kwa jamaa, maji mnachota mtaa wa pili ndiyo kuna kisima, basi asubuhi mkaka akawa anakwenda kumchukulia babe wake maji ya kuoga, mwe wewe wa mama wasiache kumchamba, huyu ndiyo utamuoa huyu, mwanamke amelala wewe unakwenda kuchota maji.
na siri ya kwenye nyumba ya kupanga kama mama mwenye nyumba akikutaka ukamkatalia,then ukahama pale kwake alafu ukamkumbushia kutaka umtafune,hawezi kukupa uchi wake kamwe,sijui tatizo linakuwaga niniHabari za leo wandugu,
Dunia hii kuna wengine hawajawahi kabisa kuishi katika nyumba za kupanga, wengine maisha ya uswazi hawayajui kabisa, basi leo nimeona tuangalie maisha katika nyumba za kupanga. Ukweli ni kuwa maisha katika nyumba za kupanga si mabaya, ni wewe mwenyewe utakavyoiweka akili yako.
Unaweza kujifunza mapishi katika nyumba za kupanga, kwani kupika wote mnapika pamoja, kama ulitoka kwenu hujui kipika chapatti, utakutana na wapangaji wenzako ambao tena wanapika chapatti za biashara, na utajifunza kukanda unga hapo. Si chapatti tu, ni mapishi mengi.
Ukitaka kuishi vizuri kwenye nyumba za kupanga usiwe mbea na mfuatiliaji wa mambo ya watu pia usipende kuanika ya kwako. Ukikuta unaongelewa wewe dharau tu, kama hujaanika sana yako watakayo kuwa wanaongea watakuwa wanahisi.
Rafiki zangu wa kiume kama watatu hivi waliniambia bikra zao zilitolewa na wapangaji wengine wakati wakiwa wadogo kwenye nyumba za kupanga, mimama isiyokuwa na haya anamsubiri mama wa kijana ametoka, ndipo kijana anapoitwa chumbani, huko anakuta ameandaliwa chai na vitafunwa na akapewa mchezo. Kama vile wale wa ushuani wanaposema bikra zimetolewa kwa ma housegirl huku kwetu kwa Mtogole kuna mengi pia yanaendelea.
Dhumuni la waraka huu ni kufahamishana dunia inavyoendelea katika nyumba hizi, kuna mengi yanayoendelea ambayo wazazi hawayafahamu. Fikiria kama hili li mama linalomuitia kijana wako chai lina magonjwa, mpaka uje uhfahamu mtoto ameathirika kabla hajafikisha miaka 20.
Siku njema.
Hahahahah nmejikuta nacheka nkiwaza pale ntakapomkuta mbea wa mtaa akihesabu maganda ya mayai kwenye dustbin yanguKuna brother mmoja alipata chumba uswaz, sasa asubuhi alikaanga mayai mawili kwa breakfast, khe it was a talk of the house, anakunywa chai na mayai. Basi mkaka kuwakomesha akawa anapita kwa wauza chips anaomba maganda, asubuhi akishakaanga mayai yake mawili anatupa maganda kama ya mayai sita hivi, wee wa mama wanakaa kabisa kuhesabu maganda.
Hahahahahahah mmhh nmejikuta nmecheka kwanguvu af npo offisini mpaka nmejishtukia...... Mmhh kweli jf is never boringMmenikumbusha wakat naanza maisha kule kwa ali maua siku nayofunga dish la GTV mtaa mzima umesimama unashangaa jioni nkirudi home nakuta watu mlangoni wanasubiri waje kuangalia tv
Asubuhi mnawahi foleni ya kuoga maana bafu si ni moja..... Mwingine anaweka ndooo mwingine jiwee kila Mara anatoka kusogeza foleni take mbele"Raha" ya nyumba za kupanga ni pale nyumba inapokuwa na familia zaidi ya sita lakini choo na bafu ni kimoja!
Huyo afadhali. Mimi nilikuwa narudi na maganda ya mayai matano hivi asubuhi naweka sufuria jikoni inapata motooo halafu naimwagia maji utasika chaaaaaaaaaaaaaaaa kama mayai vile. Nikitoka naenda kutupa maganda!Kuna brother mmoja alipata chumba uswaz, sasa asubuhi alikaanga mayai mawili kwa breakfast, khe it was a talk of the house, anakunywa chai na mayai. Basi mkaka kuwakomesha akawa anapita kwa wauza chips anaomba maganda, asubuhi akishakaanga mayai yake mawili anatupa maganda kama ya mayai sita hivi, wee wa mama wanakaa kabisa kuhesabu maganda.