USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,896
- 22,666
Wapuuzi sana wao jinai ni kikiWatajijua wenyewe sisi tupo na Magufuli kwenda uchumi wa kati
Wapuuzi sana wao jinai ni kikiWatajijua wenyewe sisi tupo na Magufuli kwenda uchumi wa kati
Zito ni kada
*TAARIFA KWA UMMA*
...
Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!
....
*Dorothy J. Semu,*
*Makamu Mwenyekiti Bara,*
*ACT Wazalendo.*
*29 Mei 2020.*
Ndiyo maana alibeba saaana UDSM na kumaliza kwa taabu sana. Hawa wametumika mpaka wamesahau waongee kipi."Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!"
kwa hiyo ndio sababu inayomfanya atoe matamshi ya kichochezi?
Hiyo hukumu ni ndogo mno....mshenzi huyo amefanya visa vingi sana....mahakama ingemgonga na faini*TAARIFA KWA UMMA*
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mshtuko taarifa ya kutiwa hatiani kwa Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ambaye alishitakiwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu na kukabiliwa na mashtaka matatu chini ya Sheria ya Vyombo vya Habari.
Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Ndugu Wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo, kwa sasa itoshe tu kusema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinapokea na kuyaheshimu maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu yaliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na kwamba kwa sasa Chama kinasubiri kupokea ushauri wa mawakili wa Ndugu Zitto Kabwe kuhusu tafsiri ya hukumu hiyo na hatua sahihi za kuchukua.
Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!
Wakati tukiendelea kusubiri tafsiri na ushauri wa wanasheria, nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama kuwataka wanachama wote mtulie katika kipindi hiki huku mkisubiri taarifa mbali mbali zitakazotolewa na Chama kupitia viongozi wenu.
Tunachukua fursa hii pia kuwapongeza mawakili wote ambao wamefanya kazi kubwa sana tangu mwanzo hadi mwisho wa kesi hii. Mawakili hao ni Stephen Mwakibolwa, Bonifasia Mapunda, Peter Kibatala, Jebra Kambole na Jeremia Mtobesya.
Asanteni na nashukuru sana!
*Dorothy J. Semu,*
*Makamu Mwenyekiti Bara,*
*ACT Wazalendo.*
*29 Mei 2020.*
Iwapo mhukumiwa na wafuasi wake wataamini ni adhabu ndogo, watakuwa wanajidanganya. Kwa mtu aliyezoea kuropokaropoka, kama Zitto, adhabu hiyo ni kubwa sana.Hiyo hukumu ni ndogo mno....mshenzi huyo amefanya visa vingi sana....mahakama ingemgonga na faini
Zito amepotosha mengi
Zito amechonganisha sana
Zito anahujumu taifa
Mimi si mwanasheria lakini naona mtego hapo-kwani anae amua kuwa mtu amefanya uchochezi ni polisi, dpp na hakimu bahati uchochezi ni kama urembo,mrembo kwangu kwako anaweza kuwa si mrembo. Hivyo Zitto atafuatiliwa na wakiona inabidi basi ataambiwa mchochezi. Kazi moja ya upinzani ni kuibua udhaifu wa watawala na kwa Tanzania inaonekana ukiupiga utawala za uso unakuwa mchochezi.Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mkuu kama haujui Mahakama wengi wa kisutu ni threat sana kwa regime hii.Mkuu, hili ni kosa kubwa sana kwa hakimu. Kuna kupatikana na hatia au kutopatikana na hatia. Kama Zitto hakuwa na hatia ilikuwa inatosha kumwachia. Kosa lingine atalofanya Zitto halipaswi kuhusishwa kwa namna yoyote na shitaka hili ambalo hakukutwa na hatia.
Tuna au majaji wanasiasa au wanaotoa hukumu za hisia.
Mimi si mwanasheria lakini naona mtego hapo-kwani anae amua kuwa mtu amefanya uchochezi ni polisi, dpp na hakimu bahati uchochezi ni kama urembo,mrembo kwangu kwako anaweza kuwa si mrembo. Hivyo Zitto atafuatiliwa na wakiona inabidi basi ataambiwa mchochezi. Kazi moja ya upinzani ni kuibua udhaifu wa watawala na kwa Tanzania inaonekana ukiupiga utawala za uso unakuwa mchochezi.
Yes.Una uhakika?
Yes.
Iwapo mhukumiwa na wafuasi wake wataamini ni adhabu ndogo, watakuwa wanajidanganya. Kwa mtu aliyezoea kuropokaropoka, kama Zitto, adhabu hiyo ni kubwa sana.
Ni dhahiri hukumu hiyo imefungua ukurasa mpya nchini. Ni funzo tosha kuwa kila mtu anawajibika kupima uzito wa mawazo/maoni yake kabla ya kutamka. Kwamba uhuru wa mawazo una mipaka na haki uambatana na wajibu, kama inavyotakiwa katika Katiba ya JMT (1977).
Ibara ya 30(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.