Mahakama Kuu yasitisha Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS)

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,319
24,218
15 December 2023

Mahakama Kuu ya Tanzania imeagiza kusitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS uliopangwa kufanyika kesho jumamosi tarehe 16 December 2023.

Amri hiyo imeyolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam kwenye maombi madogo no. 27673 ya mwaka 2023 ktk shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais wa TLS mwanasheria msomi Harold Sungusia awaomba wanachama kuwa watulivu.

1702698103556.png

Picha: Rais wa TLS wakili Harold Sungusia

Rais wakili msomi Harold Sungusia asema shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali likisikikizwa upande mmoja bila TLS kuhusishwa ijumaa 15 December 2023.

Na kuwa ofisi na uongozi wa TLS ulipata taarifa ya zuio hilo saa 12 jioni ijumaa tarehe 15 December 2023 .

===
Rais wa TLS alisema kuwa kikao hicho kilipanga kujadili mabadiliko ya Sheria ya Mawakili ili kuongeza wigo wa mawakili kujisimamia wenyewe na kufanya kazi pasipo kushurutishwa.

Pia walitaka kujadili suala la Kamati ya Maadili ya Mawakili, ambayo amesema imekuwa ikifanya maamuzi ambayo yanautata wa kisheria.
 
15 December 2023

Mahakama Kuu ya Tanzania imeagiza kusitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS uliopangwa kufanyika kesho jumamosi tarehe 16 December 2023.

Amri hiyo imeyolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam kwenye maombi madogo no. 27673 ya mwaka 2023 ktk shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais wa TLS mwanasheria msomi Harold Sungusia awaomba wanachama kuwa watulivu.
Hoja (sababu) ya kuzuia huo mkutao hasa ni zipi?
Huyo Baltazary Bosco Mahai hasa ni nani?
 
Hoja imeandikwa kwa hati ya dharura.

Haya tupe usuli sasa
15 December 2023

Mahakama Kuu ya Tanzania imeagiza kusitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS uliopangwa kufanyika kesho jumamosi tarehe 16 December 2023.

Amri hiyo imeyolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam kwenye maombi madogo no. 27673 ya mwaka 2023 ktk shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais wa TLS mwanasheria msomi Harold Sungusia awaomba wanachama kuwa watulivu.
 
Jana 15 December 2023 kongamano lilikuwa kali na kupanga maazimio mazito

Kongamano la TLS juu ya Muswada wa Sheria za uchaguzi December 15, 2023​


Hayo yamejiri katika kongamano leo lililoangazia sheria ya uchaguzi n.k

A National Stakeholders' Engagement Conference on Election Laws and Political Parties Affairs Laws in Dar es Salaam , Tanzania on 15th December, 2023.

View: https://m.youtube.com/watch?v=-Eqz8tIbtcQ
 
15 December 2023

Mahakama Kuu ya Tanzania imeagiza kusitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS uliopangwa kufanyika kesho jumamosi tarehe 16 December 2023.

Amri hiyo imeyolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam kwenye maombi madogo no. 27673 ya mwaka 2023 ktk shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais wa TLS mwanasheria msomi Harold Sungusia awaomba wanachama kuwa watulivu.

View attachment 2843731
Picha: Rais wa TLS wakili Harold Sungusia

Rais wakili msomi Harold Sungusia asema shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali likisikikizwa upande mmoja bila TLS kuhusishwa ijumaa 15 December 2023.

Na kuwa ofisi na uongozi wa TLS ulipata taarifa ya zuio hilo saa 12 jioni ijumaa tarehe 15 December 2023 .
Dhumuni na Agenda ya mkutano ilikuwa nini?
 
Dhumuni na Agenda ya mkutano ilikuwa nini?

Wakili Harold Sungusia anafafanua mkutano wa dharura agenda ni


View: https://m.youtube.com/watch?v=LAFUaEt885I

TLS kupitia baraza la uongozi la chama kuwaomba wananchama wote wafike ukumbi wa Pius Msekwa shule ya sheria ambapo wangezungumzia uhuru wa vyama vya taaluma ambavyo vinabana wanachama wa TLS kupitia miswada na sheria zilizotungwa kubana tasnia ya Mawakili kupitia marekebisho ya sheria, sheria za mawakili advocacy committee zenye utata mkubwa mfano kusimamishwa kwa wakili msomi Mpale Mpoki n.k


View: https://m.youtube.com/watch?v=mD80bAu3Gi4
 
sheria za mawakili advocacy committee zenye utata mkubwa mfano kusimamishwa kwa wakili msomi Mpale Mpoki n.k

6 Dec2023
Wakili msomi Edward Heche, Mwenyekiti wa Mawakili Vijana anatema cheche muda huu kuhusu sakata la Mawakili wenzao kusimamiswa Uwakili, hivyo kuelekea tarehe 16 December 2023 kujadili masuala kadhaa matumizi mabaya ya kamati za maadili zilizowatokea mawakili Fatma Karume, Jebra Kabole, Edson, Robert Joseph na sasa Mpale Mpoki ....


View: https://m.youtube.com/watch?v=VRyazMpdOR4
 
Muda sasa mawakili wasomi wakatae kuburuzwa, waseme imetosha ni unyanyasaji kutoka kwa walioshikilia mhimili wa dola (state).

Kutoka Maktaba :
Police Tuesday summoned lawyer and advocate Rugemeleza Nshala over remarks he made during a discussion on the social audio app Clubhouse on July 3, 2023, where he criticised the Tanzania-Dubai deal, which would allow DP World, an Emirati multinational logistics company, to take control of the operations of the Dar es Salaam’s port.

In a letter dated July 10, 2023, which has been circulating online, the Director of Criminal Investigation (DCI) Camilius Wambura ordered Dr Nshala, who doubles as the Executive Director of the environmental group Lawyers’ Environmental Action Team (LEAT), to report at the DCI’s office today, July 11, 2023, at 9:00 AM.

DCI said in his letter that his office was investigating the claims Dr Nshala made during the discussion that has since gone viral on social media platforms and that they needed to question the renowned advocate as part of that investigation.
1702704414691.png

Dr. Rugemeleza A.K Nshala wakili msomi
 
Wanasheria wanapaswa kuelewa viongozi wa kiafrika wanataka kutukuzwa na kusifiwa tu ukikosoa au kuwapinga vikwazo vinaanza na sababu tele unapewa, tunarudi zama za zidumu fikra za Mkuu.
 
Maono ya rais mstaafu Tundu Lissu

2017 30 Juni

MKUTANO WA DHARURA WA TLS: Tundu Lissu apinga pendekezo la Serikali kuiweka TLS chini ya Waziri -Katiba na Sheria.


View: https://m.youtube.com/watch?v=DZrEULt6TjY
Leo Juni 30 2017 kwenye Mkutano wa Dharura wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Rais wa Chama hicho, Mwanasheria Tundu Lissu apinga mapendekezo ya Serikali yaliyomo kwenye "Bango Kitita" yanayotaka kuiweka TLS chini ya Waziri wa Katiba na Sheria.

Toka mwaka 1954 chama cha TLS kilipoasisiwa .....
 
TLS kupitia baraza la uongozi la chama kuwaomba wananchama wote wafike ukumbi wa Pius Msekwa shule ya sheria ambapo wangezungumzia uhuru wa vyama vya taaluma ambavyo vinabana wanachama wa TLS kupitia miswada na sheria zilizotungwa kubana tasnia ya Mawakili

BUNGE LARIDHIA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA​

Imewekwa: 01 Nov, 2023
Bunge laridhia Muswada wa Marekebisho ya Sheria

Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesoma kwa mara ya tatu Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria wa mwaka 2023 (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023) na kuridhiwa na Bunge na sasa utapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo naye akiridhia Muswada huo utakuwa sheria.
Muswada huo unaolenga kufanyia marekebisho sheria Ishirini na Tatu ili kuondoa upungufu uliobainika wakati wa utekelezaji wa Sheria hizo umesomwa tarehe 31 Oktoba, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.
Source : MoCLA | Bunge laridhia Muswada wa Marekebisho ya Sheria

The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2023 is a Tanzanian law that amends various laws relating to the legal sector. The Act was enacted on August 16, 2023 and has not yet been commenced.

The Act amends a number of laws, including the Advocates Act, the Legal Aid Services Act, and the Business Registration Act. The amendments are intended to improve the efficiency and effectiveness of the legal sector in Tanzania.

Some of the key amendments made by the Act include:

  • Amending the Advocates Act to make it easier for foreign lawyers to practice law in Tanzania
  • Amending the Legal Aid Services Act to expand the scope of legal aid services available to Tanzanians
  • Amending the Business Registration Act to make it easier for businesses to register and operate in Tanzania
The Act is expected to have a significant impact on the legal sector in Tanzania. It is hoped that the amendments will make the legal system more accessible and affordable for Tanzanians.

Here are some of the potential benefits of the Act:

  • Increased access to justice for Tanzanians
  • Improved efficiency of the legal system
  • Reduced costs of legal services
  • Enhanced investor confidence in Tanzania
The Act is also expected to have some potential challenges. These include:

  • The need to train lawyers and legal aid providers on the new amendments
  • The need to increase funding for legal aid services
  • The need to ensure that the amendments are implemented effectively
Overall, the Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2023 is a positive development for the legal sector in Tanzania. The Act is expected to improve the efficiency and effectiveness of the legal system, and make it more accessible and affordable for Tanzanians. However, there are some potential challenges that will need to be addressed in order to ensure that the Act is implemented effectively.




MORE INFO :

BUNGENI 31 OKTOBA 2023

Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (Mb.),
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
31 Oktoba, 2023

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ahsante sana. Hoja
imeungwa mkono. Tunaendelea na utaratibu wetu. Namwita sasa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria. Wasomaji inabidi mkae upande wangu wa huku kulia, ikiwa
mmechaguliwa kusoma na wale wengine upande wa kushoto ili
tuwe tunakomboa wakati. (Makofi)
Kwa niaba ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa
Florent Laurent Kyombo.

MHE. FLORENT L. KYOMBO – MAKAMU MWENYEKITI KAMATI YA
KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa
Spika, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria, naomba kuwasilisha maoni na
ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria, kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali (Na. 4) ya mwaka 2023 (The Written Laws Miscellaneous
Amendments (No. 4) Bill, 2023).
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(5) ya Kanuni
ya Kudumu ya Bunge, Toleo la Februari, 2023, naomba kuwasilisha
maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali (Na. 4) ya mwaka 2023. Kwa kuzingatia masharti ya
Kanuni ya 93(2) ya Kanuni ya Kudumu ya Bunge, Muswada huu
ulisomwa Bungeni kwa Mara ya Kwanza katika Mkutano wa Kumi

Page 166



Eliezer Mbuki Feleshi (Mb) Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu
maudhui ya Muswada huu. Baada ya Kamati kupatiwa maelezo
ya Serikali, Wajumbe walipata fursa ya kuuliza maswali, na kupata
maelezo ya ufafanuzi katika ibara mbalimbali za Muswada.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge Kamati ilifanya Mkutano wa Kusikiliza Maoni ya
Wadau (Public Hearing) tarehe 19 Oktoba, 2023 ili kupokea maoni
yao kuhusu Muswada huu. Aidha, Kamati ilipokea maoni kwa njia
ya mtandao kutoka kwa watu na makundi mbalimbali ya wadau
ambao hawakuweza kufika mbele ya Kamati kuwasilisha maoni
yao.
Mheshimiwa Spika, nawashukuru wadau wote waliotoa maoni yao
ili kuuboresha Muswada huu na nichukue fursa hii kuwatambua
kama ifuatavyo: -

1. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS);

2. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC); pamoja na

3. Wadau binafsi kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Spika, baada ya hatua hiyo, Wajumbe wa Kamati
walipata fursa tena ya kujadili maudhui ya Muswada kwa
kuzingatia maelezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa
kuzingatia maoni ya wadau. Mnamo tarehe 23 Oktoba, 2023
Kamati ilikutana tena na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye
alijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati kuhusu
ibara mbalimbali za Muswada.
Mheshimiwa Spika, baada ya hatua hiyo, nilizingatia masharti ya
Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge na kukujulisha rasmi
kwamba Kamati imekamilisha uchambuzi wa Muswada ili ujadiliwe
Bungeni.
2.0 UCHAMBUZI WA MUSWADA
2.1 Utangulizi
Mheshimiwa Spika, kamati ilichambua Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.4 wa Mwaka 2023 [The

Page 176



Mheshimiwa Spika, Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mhe.
Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Pauline Philipo Gekul (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Mhe. Eliezer Mbuki Feleshi Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Serikali Ndg. Onorius Njole, pamoja
na watendaji wote wa Serikali kwa ushirikiano wao wa dhati katika
kuyafanyia kazi maoni na mapendekezo ya Kamati.
Mheshimiwa Spika, nawashukuru Watumishi wote wa Ofisi ya
Bunge chini ya uongozi thabiti wa Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa
J. Mwihambi, ndc na kwa upekee Sekretarieti ya Kamati kwa
uratibu wa shughuli za Kamati hadi kukamilika kwa taarifa hii.
4.2 Msimamo wa Kamati Kuhusu Hoja
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, Kamati inalishauri
Bunge lako tukufu kuujadili, kuukubali na kuupitisha Muswada huu
pamoja na Jedwali la Marekebisho kama lilivyowasilishwa na mtoa
hoja.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja.
Mhe. Florent Laurent Kyombo (Mb)
M/MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA
BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA
31 Oktoba, 2023
SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge, ahsante sana
Makamu Mwenyekiti. Nimuite sasa Mheshimiwa Waziri wa Katiba
na Sheria, Mheshimiwa Balozi, Dkt. Pindi Chana, aje awasilishe hoja
yake. (Makofi)
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa
ni mara yangu ya kwanza kusimama hapa kama Waziri wa
masuala ya katiba na sheria, nitakuwa mchoyo wa fadhila ikiwa
sitatumia fursa hii leo kwa mara ya kwanza nikiwa kama Waziri wa
Katiba na Sheria, nisipomshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwa

Page 184

kuendelea kuniamini na kuniteua tena kuwa Waziri wa Katiba na
Sheria. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais,
kwa kuridhia kutoa fedha za kuwezesha Mkutano wa 77 wa Tume
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, unaoendelea jijini Arusha.
Matokeo ya mkutano huu yamezidi kuing’arisha Tanzania kuwa
kinara wa ulinzi na haki za binadamu duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kipekee nichukue fursa hii kukupongeza
wewe kwa kupata ushindi wa kishindo, uliyokufanya kuwa Rais wa
31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Nampongeza pia
Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Muswada huu unakusudia kufanya
marekebisho katika sheria mbalimbali za sekta ya sheria ili kuondoa
mapungufu yaliyobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo.
Muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali za sekta ya sheria
wa mwaka 2023 kama ulivyowasilisha, unapendekeza
marekebisho katika sheria zifuatazo. Zimeelezwa hapo kuanzia
ukurasa wa pili hadi ukurasa wa nne, naomba ziingie kwenye
hansard kama zinavyojieleza namba moja hadi 23.
Mheshimiwa Spika, Muswada huu umegawanyika katika
sehemu 24, ambapo sehemu ya kwanza inahusu masharti ya
utangulizi, yanayojumuisha jina la Muswada na namna ambavyo
sheria mbalimbali zinapendekezwa kurekebishwa na Muswada
huu. Sehemu ya pili ya Muswada, inapendekeza kufanya
marekebisho katika Sheria ya Mawakili sura ya 341, ambapo
kifungu cha 4(a) kinapendekeza kurekebisha ili kuondoa cheo cha
Wakili wa Serikali Mfawidhi, State Attorney in charge, na badala
yake kuweka cheo cha Wakili wa Serikali wa Mkoa (regional State
Attorney).
Mheshimiwa Spika, madhumuni ya marekebisho haya ni
kumfanya Wakili wa Serikali wa Mkoa, kuwa muwakilishi wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika kamati ya mawakili ya Mkoa.
Pia kuendana na muundo wa sasa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Page 185

wa Serikali. Aidha Muswada unapendekeza kufanya marekebisho
katika kifungu cha 8(1)(e) ili kuongeza wigo wa vyuo na kuweka
sharti la lazima kupita katika shule ya sheria kwa vitendo. Lengo ni
kuimarisha mfumo wa udhibiti wa ubora wa Mawakili kwa kuwa na
mafunzo yanayofanana kwa wote.
Mheshimiwa Spika, vifungu vya 41 na 42 vinapendekezwa
kurekebishwa ili kuongeza adhabu kwa watu ambao siyo Mawakili
wanaofanya kazi za Mawakili. Lengo la marekebisho haya
yanayopendekezwa ni kuzuia utendaji wa makosa ambayo
huathiri utaratibu wa upatikanaji wa haki hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, sehemu ya tatu ya Muswada
inapendekeza kurekebisha sheria ya mamlaka ya rufaa sura ya 141
ambapo kifungu cha 4(e) kinapendekezwa kuongezwa ili kuweka
zuio kwa mahakama ya rufani kusikiliza maombi ya mapitio au
uwamuzi wa muda isipokuwa kama maombi hayo yanaradhimu
shauri la msingi.
Mheshimiwa Spika, vilevile kifungu cha 5 kinapendekezwa
kurekebishwa ili kuboresha masharti ya kukata rufaa katika
mashauri ya madai. Msingi wa marekebisho haya ni kuweka
utaratibu utakaosaidia umalizaji wa mashauri ya madai kwa
wakati.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya nne ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya usuruhishi,
sura ya 15 ambapo kifungu cha 82(3)(b) kinapendekezwa
kurekebishwa ili kuondoa mamlaka ya kusajili wasuruhishi kutoka
kituo cha usuruhishi, kwa kuwa wasuruhishi husajiliwa na Msajili chini
ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai, sura ya 33. Lengo
la marekebisho haya ni kuowanisha masharti ya usajili wa
wasuruhishi katika sheria hizo mbili.
Mheshimiwa Spika, sehemu ya tano ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, sura ya 391, ambapo kifungu cha 6
kinapendekezwa kurekebishwa ili kufuta maneno Administrative
Justice na badala yake kuweka maneno good Governance.

Page 186

Lengo la marekebisho haya ni kutumia maneno yanayoakisi
majukumu ya Tume kama yalivyoainishwa katika Katiba ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, aya ya
kwanza, inayopendekezwa kufutwa na kuandikwa upya. Lengo ni
kuiacha tume na majukumu yake ya msingi ya uchaguzi na
masuala ya kuendesha mashauri ya kisheria yabaki katika taasisi
husika.
Mheshimiwa Spika, aidha, kifungu cha 11 kinapendekezwa
kufanyiwa marekebisho ili kuanzisha eneo na cheo cha Naibu
Makatibu wa Tume. Lengo la marekebisho haya ni kuboresha
utekelezaji wa majukumu ya tume. Vilevile kifungu cha 12
kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka sharti kwa Naibu
Makatibu wa Tume kuapa mbele ya Mheshimiwa Rais, kabla ya
kuanza kutekeleza majukumu yao.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya sita ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika sheria…
SPIKA: Mheshimiwa Waziri, subiri kidogo. Ni kitu gani hicho
kinasikika huko? Waheshimiwa Wabunge, tafadhalini sana.
Mheshimiwa Waziri.
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, sehemu ya
sita ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria
ya mwenendo wa mashauri ya jinai, sura ya 20 kwa kuongeza
kifungu cha 4(e) ili kuowanisha madhumuni ya msingi (overriding
objectives) katika sheria. Lengo la marekebisho haya ni kuzitaka
mahakama kutenda haki kwa wakati na kuangalia haki msingi
katika kusikiliza mashauri ya jinai bila kufungwa na kiasi kikubwa cha
masharti ya kiufundi.
Mheshimiwa Spika, aidha vifungu vya 202, 204, 205(a) na
205(b) vinapendekeza kurekebishwa kwa kuahinisha namna
ambavyo wataalam kama vile wataalam wa mripuko na
wataalam wa uchunguzi wa makosa ya mtandao wanaweza
kuteuliwa na Mkurugenzi wa mashitaka. Madhumuni ya
marekebisho haya ni kubadilisha nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa

Page 187
 
15 December 2023

Mahakama Kuu ya Tanzania imeagiza kusitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS uliopangwa kufanyika kesho jumamosi tarehe 16 December 2023.

Amri hiyo imeyolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam kwenye maombi madogo no. 27673 ya mwaka 2023 ktk shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais wa TLS mwanasheria msomi Harold Sungusia awaomba wanachama kuwa watulivu.

View attachment 2843731
Picha: Rais wa TLS wakili Harold Sungusia

Rais wakili msomi Harold Sungusia asema shauri la Baltazary Bosco Mahai dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali likisikikizwa upande mmoja bila TLS kuhusishwa ijumaa 15 December 2023.

Na kuwa ofisi na uongozi wa TLS ulipata taarifa ya zuio hilo saa 12 jioni ijumaa tarehe 15 December 2023 .

===
Rais wa TLS alisema kuwa kikao hicho kilipanga kujadili mabadiliko ya Sheria ya Mawakili ili kuongeza wigo wa mawakili kujisimamia wenyewe na kufanya kazi pasipo kushurutishwa.

Pia walitaka kujadili suala la Kamati ya Maadili ya Mawakili, ambayo amesema imekuwa ikifanya maamuzi ambayo yanautata wa kisheria.
Malalamiko yanaendelea kwa kasi kwamba huyu Jamaa amepwaya vibaya hapo TLS.
Wanashauriana kumtoa mwezi wa nne na kuweka Jaji mstaafu fulani jina kapuni.
 
Back
Top Bottom