Mahakama Kuu nchini Zanzibar yafuta kifungu kinachozuia uagizaji wa vileo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,422
5,037
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini:

Mahakama Kuu, Zanzibar imebatilisha kifungu cha 33(1) cha Sheria ya Kudhibiti Vileo (LCA) ya mwaka 2020 kinachoweka ukomo wa kampuni zinazoruhusiwa kuagiza vileo ikisema kinakinzana na Katiba ya Zanzibar.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji George Kazi katika hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mahakamani hapo na kampuni ya Quality Meat and Beverage Supplies (QMB), dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kampuni hiyo ilifungua kesi baada ya kunyimwa leseni ya uagizaji vileo kutokana na masharti ya kifungu hicho, yanayoweka ukomo wa kampuni tatu tu zinazoruhusiwa.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 01 ya mwaka 2023, pamoja na mambo mengine kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba Mahakama itamke masharti ya kifungu cha 33 (1)(a)(b)(c)(d), (2) na (3) cha Sheria ya Vileo Sheria namba 9 ya mwaka 2020 inakinzana na Katiba. Pia iliomba mahakama izingatie kifungu cha 43(1) na (2)(a)(b)(c)(d)(e) cha Sheria ya Ushindani Sawa na Ulinzi Sawa kwa Mlaji (FCFCPA) namba 5 ya mwaka 2018.

Katika maombi mbadala, kampuni hiyo iliiomba Mahakama ikiipendeza ielekeze wale wote walioathirika na masharti ya sheria hiyo, wapewe nafuu za kisheria kwa mamlaka yake kabla ya kutungwa au kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Vileo kuweka masharti ya usawa.

Jaji Kazi katika hukumu aliyoitoa Aprili 4, 2024 baada ya kusikiliza hoja za pande zote amekubaliana na hoja za kampuni hiyo na kuamua kuwa kifungu hicho cha Sheria ya Vileo hakipaswi kutumika na ni batili kisheria, hivyo hakitekelezeki.
IMG-20240407-WA0037.jpg

MCL
 
Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 01 ya mwaka 2023, pamoja na mambo mengine kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba Mahakama itamke masharti ya kifungu cha 33 (1)(a)(b)(c)(d), (2) na (3) cha Sheria ya Vileo Sheria namba 9 ya mwaka 2020 inakinzana na Katiba.

Pia iliomba mahakama izingatie kifungu cha 43(1) na (2)(a)(b)(c)(d)(e) cha Sheria ya Ushindani Sawa na Ulinzi Sawa kwa Mlaji (FCFCPA) namba 5 ya mwaka 2018.

Katika maombi mbadala, kampuni hiyo iliiomba Mahakama ikiipendeza ielekeze wale wote walioathirika na masharti ya sheria hiyo, wapewe nafuu za kisheria kwa mamlaka yake kabla ya kutungwa au kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Vileo kuweka masharti ya usawa.

Jaji Kazi katika hukumu aliyoitoa Aprili 4, 2024 baada ya kusikiliza hoja za pande zote amekubaliana na hoja za kampuni hiyo na kuamua kuwa kifungu hicho cha Sheria ya Vileo hakipaswi kutumika na ni batili kisheria, hivyo hakitekelezeki.
 
Habari hii nzuri sana, na tukiangalia kwa upana wake sheria kadhaa zinaenda kinyume na katiba.

Swali kuu kwanini vitungwe sheria nyingi zinazokinzana na kariba, sababu ni kukomoana, kukosa uelewa mpana wa kina wa kariba yetu au ni ubabe wa walio madarakani kutunga kanuni, masharti na sheria bila kuzingatia katiba ya nchi.
 
Taratibu wataruhusu vingi.
Hivi Ile kitimoto tunayokula tukiwa Zanzibar inafugiwa Zanzibar kule kule au Wana import kutoka Mbeya?
 
Mnaoshabikia kwamba mh. Simai kashinda how come awe yeye wkt kesi ilifunguliwa akiwa bado waziri?.

Lakini nini impact ya sheria hii kuwa wazi kuruhusu kampuni nyingine kuingiza vileo, unadhani hakuna sheria ndogo za kulinda utamaduni?.
 
Sheria ndogo ndogo hazitakiwi kukinzana na katiba au sheria mama.
 
Mnaoshabikia kwamba mh. Simai kashinda how come awe yeye wkt kesi ilifunguliwa akiwa bado waziri?.

Lakini nini impact ya sheria hii kuwa wazi kuruhusu kampuni nyingine kuingiza vileo, unadhani hakuna sheria ndogo za kulinda utamaduni?.
Huwezi endeleza mji/nchi ya kitalii tena ni beach tourism, wakati huo huo kuna sheria zinakinzana na maendeleo hayo...

Vileo vinauzwa sana mahotelini Zanzibar, na upatikanaji wake kuna muda unakuwa wa tabu sana, nadhani hii ilitokana na ukomo huo wa kuwa na kampuni tatu pekee za uingizaji vileo kwa wakati huo...

Now sidhani kama zitakuwa adimu sana
 
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini:

Mahakama Kuu, Zanzibar imebatilisha kifungu cha 33(1) cha Sheria ya Kudhibiti Vileo (LCA) ya mwaka 2020 kinachoweka ukomo wa kampuni zinazoruhusiwa kuagiza vileo ikisema kinakinzana na Katiba ya Zanzibar.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji George Kazi katika hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mahakamani hapo na kampuni ya Quality Meat and Beverage Supplies (QMB), dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kampuni hiyo ilifungua kesi baada ya kunyimwa leseni ya uagizaji vileo kutokana na masharti ya kifungu hicho, yanayoweka ukomo wa kampuni tatu tu zinazoruhusiwa.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 01 ya mwaka 2023, pamoja na mambo mengine kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba Mahakama itamke masharti ya kifungu cha 33 (1)(a)(b)(c)(d), (2) na (3) cha Sheria ya Vileo Sheria namba 9 ya mwaka 2020 inakinzana na Katiba. Pia iliomba mahakama izingatie kifungu cha 43(1) na (2)(a)(b)(c)(d)(e) cha Sheria ya Ushindani Sawa na Ulinzi Sawa kwa Mlaji (FCFCPA) namba 5 ya mwaka 2018.

Katika maombi mbadala, kampuni hiyo iliiomba Mahakama ikiipendeza ielekeze wale wote walioathirika na masharti ya sheria hiyo, wapewe nafuu za kisheria kwa mamlaka yake kabla ya kutungwa au kufanyika kwa marekebisho katika Sheria ya Vileo kuweka masharti ya usawa.

Jaji Kazi katika hukumu aliyoitoa Aprili 4, 2024 baada ya kusikiliza hoja za pande zote amekubaliana na hoja za kampuni hiyo na kuamua kuwa kifungu hicho cha Sheria ya Vileo hakipaswi kutumika na ni batili kisheria, hivyo hakitekelezeki.
View attachment 2956858

MCL
Takibiiir!
Njoo Zanzibar nikuonyeshe maelfu ya walevi wanao swali sala tano kila siku.
 
Back
Top Bottom