Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu

Hapa ndo huwa tunasema when GOD chose you nothing bad will hapen to you
Wewe ni mchaguliwa
am proud of you Sir
Hivi Kama Hitler angekufa katika Vita ya kwanza ya dunia, maana alijeruhiwa, wanadamu karibu milioni 20 wakiwemo Wayahudi milioni 6 wangekufa kwa halaiki chini ya ukatili wa NAZI!!!?
 
Kumbe Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli aka Baba lao, amepitia misuko suko mingi kila la kheri katika kutimiza kazi yako.
 
Titicomb, Hivi ni nani aliyemlinda Mussolini au Hitler hadi kupata madaraka makubwa yaliyosababisha Vita ya pili ya dunia na kuangamiza wanadamu kwa mamilioni!!!? Ni Mungu huyu huyu uliyemnukuu au Kuna mwingine?
 
Kiukweli baada ya kusikiliza maelezo ya Rais Magufuli namna alivyopitia changamoto mbalimbali za kisiasa bila kukata tamaa hadi kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi, mimi Johnthebaptist ninasadiki kuwa kweli huyu ni chaguo la Mungu.

Kwa namna mkono wa Mungu ulivyomlinda katika safari yake ya kisiasa hata kuwalegeza wale wenye nia ovu waliojaribu kumdhuru, mimi ninasadiki huyu ni chaguo la Mungu.

Mungu endelea kumbariki Rais Magufuli

Maendeleo hayana vyama

Amina!
 
Jambo hili sio la siri tena na kama limewekwa wazi linastahili kujadiliwa na ukweli kuwekwa wazi na sio kufichwa tena la sivyo itakuwa ni propaganda hatari kwa taifa.

Mheshimiwa Rais Leo kasema aliwahi kupewa sumu na kidogo afe baada ya Mkapa kumtaja kama waziri bora hivyo kuwafanya mawaziri wengine kumchukia.

Jee waziri aliye panga mpango wa kumuua (maana una mpa sumu mtu ili afe) ni nani na alichukuliwa hatua gani?
Mawaziri waliokuwepo na pengine sifa za Magufuli hawakupenda ziwafunike ni nani hao? Kikwete? Lowassa? au Mwandosya? Maana hao walikuwa kwenye mpango wa kuwania urais! Na kama sio wao ni nani?

Je, kama hakuna aliyechukuliwa hatua haiwezekani sasa hivi ana kinyongo hivyo ana kill them softly?
Au ni propaganda maana Leo ghafla upepo ukageuka badala ya kumzungumzia Mkapa na kitabu chake ikawa ni Magufuli na mchakato wake wa Urais.

Waandishi mahiri sasa mmefunguliwa mjadala mpana wa jambo hili kulianfikia kwa kutafuta ukweli kutoka kwake Magufuli mwenyewe na hata kwa Mkapa. Ikiwezekana hata kwa waziri mkuu wa wakati huo Fredrick Sumaye ambaye nashindwa kuelewa Mkapa kashindwa kumualika Leo wakati Urais wa Mkapa hauwezi kuelezewa mazuri na madhaifu bila kumtaja PM wake wa miaka kumi.
 
Hili lilikuwa swali la kwanza nililojiuliza. Kama bado wapo waanze kujihesabia maumivu, kwa sababu kumbukumbu zimeletwa mbele. Mafaili yamepanguswa mavumbi.
Hao watakuwa watu waliotaka urais wa nchi wakaona pengine Magufuli angekuwa tishio lao baada ya Mkapa kumaliza kipindi chake. Kumbe ule mtandao ulikuwa hatari sana sana na ulijipanga kuichukuwa nchi kwa namna yoyote. Nilikuwa napuuza wale walikuwa wanasema kifo cha mwalimu Nyerere kilikuwa cha utata lakini sasa naanza kupata mwanga.... (NB: Katika kuelezea hao waliompa sumu amesema ''baadhi ya mawaziri walianza kunichukia... tena wengine wa ngazi za juu kabisa'').
 
CCM ya kipindi cha nyuma isingeweza kufanya kitu cha hatari halafu cha ndani na kuacha ushahidi labda ya kipindi iki refer Karume Jumbe, Sokoine, Kolimba, Makamo wa Rais wa Mkapa Mwakyembe na Filikunjombe. labda mambo ya nje ya chama kama kuokotwa kwa Ulimboka Bunju.
 
Chakaza,
Nadhani itakuwa hakuna ushahidi. Pengine aliumwa na baada ya kwenda hospitali wakamwambia amekula sumu. Kwa hiyo kwenye mazingira kama haya atakuwa anahisi tu pengine ni kina fulani. Na hao kina fulani nadhani unaweza kuunganisha dots mwenyewe. Ni kina nani walikuwa wanautaka Urais kwa hali zote baada ya kipindi cha Mkapa? Ukitaka unaweza kwenda mbali zaidi na kujiuliza.

Zile tetesi kuwa Mwalimu Nyerere aliuawa na watu waliohisi kuwa anaweza kuwa kikwazo kwao katika kuutafuta urais zinaweza kuwa kweli?
 
Chakaza,

Sifahamu lakini wakati ule nakumbuka hapa JF tuliliongelea na alikwenda kutibiwa kwenye one of the Scandinavian countries. Kama sikosei Mzee Mwanakijiji vile vile aliligusia. Lakini hatukujua kama alipewa sumu, hilo linashtusha ndio mfahamu siasa zetu za Tanzania zilivyo. Mwenyezi Mungu atakulinda tu hata kama mafisi yako porini yanakusubiri.

Last time tuliongelea kutoruhusu kila Tom Dick and Harry kutaka kusalimiana na rais, ifike mahali huo mtindo uachwe maana waovu huwa hawana sura. Nimeshangaa leo hata Zito kajitokeza ambaye alivumisha ule udaku wake, the boy is not ashamed? Hivi Wizara ya Mambo ya Ndani imechukua hatua gani? Au walitaka kuchukua hatua akifa? Haya mambo ni lazima sasa yachukuliwe kwa upana na ukubwa wake. As a Country we need to act now.
 
Hivi hii inatoa picha gani kwa Nchi?? Kama wao kwa wao wanalishana sumu, waoinzani watapona?
 
Back
Top Bottom