Habari za Kifo cha Magufuli zilivyonifikia nikiwa Gerezani

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Ilikuwa saa 5 usiku Machi 17, 2021. Nilikuwa ndani ya gereza la Ruanda mkoani Mbeya, selo namba 16. Kelele za selo nyingine zilinishitua. Ikizingatiwa kuwa kelele haziruhusiwi nyakati za usiku mpaka pale kunapotokea tatizo, kwani kelele hutumika kama dalili ya kuwepo tatizo kwenye selo husika. Sasa kutokana na uzoefu wangu nilijua kwamba kelele zile ni mtu amenyatiwa.

Wiki haikuweza kupita bila tukio la mtu kunyatiwa. โ€˜๐™†๐™ช๐™ฃ๐™ฎ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ฌ๐™–โ€™ ni lugha ya msimbo ama code language ambayo maana yake ni kitendo cha mtu kumvizia mtu mwingine na kumbaka, hasa yule anayelala karibu naye. Selo kuzidiwa imekuwa fursa kwa wabakaji kutumia njia hii kuwabaka wenzao nyakati za usiku hasa wanapokuwa wamelala karibu yao. Unajua Magereza Tanzania bado yanaendeshwa kwa Sheria za kikoloni, fikiria Karne hii Magereza ya Tanzania hayana huduma za simu. Hata hivyo, turudi kwenye mada yetu.

Ila kelele zile zilinishtua sana maana zilikuwa ni kelele za furaha kiasi kwamba nikahisi kuwa huenda kuna kitu tofauti na tukio la mtu ๐™†๐™ช๐™ฃ๐™ฎ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ฌ๐™–.

Kipindi hicho nilikuwa na mgogoro mkubwa dhidi ya mkuu wa magereza Mkoa wa Mbeya RPO pamoja na mkuu wa gereza au bwana jela. Chanzo cha mgogoro huo ni uibuaji wa hoja mbalimbali wakati nikiwakilisha changamoto za wafungwa na mahabusu katika mkutano uliofanyika gerezani mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania CGP, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wabunge wanaounda kamati ya afya tarehe 6 Machi 2021.

Baadhi ya maofisa wa magereza ambao hawakupenda uwasilishaji wangu wa changamoto za wafungwa na mahabusu kwa wageni hao walianza kunitesa kwa kuhamisha selo, Kuzuia chakula kutoka nje na kuwazuia ndugu kuniona kabla ya kupigwa na kikosi maalum kiitwacho KM kama nilivyoeleza hapo awali katika sura hii. Ilinibidi kutumia njia ya kutumia majina ya mahabusu wengine kuingiza mahitaji yangu ndani ya gereza, kama vile chakula na matunda. Kwa hiyo wale Mahabusu walipokea chakula na matunda kutoka kwa ndugu zangu kisha wananiletea mimi tena.

Ukiacha mzozo wa askari magereza upande wa pili nilikuwa nafikiria jinsi ya kuandaa utetezi wangu dhidi ya kesi niliyoshitakiwa kusafirisha dawa za kulevya baada ya jamhuri kufunga ushahidi wake. Nilikuwa nimebakiza siku 8 tu kurudi mahakamani kujitetea. Kubwa zaidi ni kwamba katika kipindi hicho wakili wangu alishindwa kufika mahakamani kwa kukosa fedha za usafiri na malazi. Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu nchini Tanzania THRDC lililotoa ufadhili wa wanasheria wangu, akaunti zake za benki zilifungwa na utawala wa Rais Magufuli.

Sasa siku hiyo tarehe 17 Machi 2021, Nyapara mkuu msaidizi wa gereza alipewa maagizo na Askari Magereza aliyekuwa zamu mwenye cheo cha Inspekta, akimuagiza kuhakikisha Mdude na wenzake wanahamishiwa katika selo namba 4. Hii ni selo maalumu kwa watu wenye changamoto za afya ya akili. Kwa hivyo ilikuwa ni kawaida ukikosana na afisa yoyote wa Magereza atakuhamishia kwenye selo hiyo ya wagonjwa wa akili kama adhabu na kukukomoa. Kwa sababu maisha mle selo namba 4 ni magumu, yanatisha na hatari sana. Fikiria kukaa kwenye selo iliyojaa wanaume wendawazimu. Kumbuka kwamba wendawazimu katika selo hiyo hawawezi kulala bila kutumia dawa za usingizi na wakati mwingine katikati ya usiku huamka na kuanza kusababisha shida katika selo. Wengine hujisaidia haja zote hapohapo sehemu ya kulala wakiwa wamelala. Hii ndio selo ambayo amri ilitolewa kwamba Mdude na wapambe wake wahamishiwe.

Wakati huo huo unanyimwa huduma ya chakula gerezani, wakili wako anashindwa kufika mahakamani kwa kukosa fedha za malazi, unawaza utetezi wa kesi yako dhidi ya Jamhuri halafu ukiwa katika hali hiyo amri inatolewa upelekwe selo namba 4 ya wagonjwa wa akili. Ingawa siku zote nimejitolea maisha yangu kwa ajili ya wengine, lakini hapa nilihitaji kuchanganya ujasiri na ukichaa ili kuishinda hali hii.

Baada ya maagizo hayo, Nyapara mkuu msaidizi alinifuata kabla ya muda wa mafungio kunijulisha kwani alisikitika kuonesha kutokubaliana na maagizo ya bosi wake ya kutaka kunihamishia selo ya wendawazimu. Nilimwambia asiwe na wasiwasi nilikuwa tayari kuhamishiwa hata chooni.

Baada ya muda wa kufungiwa ndani ya maselo kufika, nilijiandaa nikiwa nimebeba mfuko au Shako mkononi, ambao ndani yake kulikuwa na chakula, maji, matunda na nguo. Moja kwa moja nilienda kwa askari Magereza waliokuwa zamu na nikawauliza; "๐™ƒ๐™ž๐™ซ๐™ž ๐™ข๐™ฃ๐™–๐™ฃ๐™ž๐™ค๐™ฃ๐™– ๐™ข๐™ž๐™ข๐™ž ๐™จ๐™ž๐™ค ๐™ ๐™ž๐™˜๐™๐™–๐™– ๐™ ๐™ž๐™–๐™จ๐™ž ๐™ ๐™ฌ๐™–๐™ข๐™—๐™– ๐™ž๐™ฉ๐™–๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™– ๐™ฉ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ฏ๐™ค ๐™ข๐™ ๐™ž๐™ฃ๐™ž๐™ฌ๐™š๐™ ๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™ฎ๐™š ๐™จ๐™š๐™ก๐™ค ๐™ฎ๐™– ๐™ฌ๐™–๐™ฉ๐™ช ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™ฎ๐™š ๐™ข๐™–๐™ฉ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ฏ๐™ค ๐™ฎ๐™– ๐™–๐™›๐™ฎ๐™– ๐™ฎ๐™– ๐™–๐™ ๐™ž๐™ก๐™ž? ๐˜ผ๐™ช ๐™ ๐™ช๐™ฃ๐™– ๐™จ๐™š๐™ก๐™ค ๐™ฃ๐™ž๐™ก๐™ž๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™– ๐™ฃ๐™–๐™ฎ๐™ค ๐™ฃ๐™ฎ๐™ช๐™ข๐™—๐™–๐™ฃ๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ก๐™š๐™ฉ๐™– ๐™๐™–๐™ฅ๐™– ๐™ ๐™ž๐™–๐™จ๐™ž ๐™ ๐™ฌ๐™–๐™ข๐™—๐™– ๐™จ๐™ž๐™ฉ๐™–๐™ ๐™ž๐™ฌ๐™ž ๐™ ๐™ช๐™๐™–๐™ข๐™ž๐™จ๐™๐™ฌ๐™–? ๐™‰๐™ž๐™›๐™ช๐™ฃ๐™œ๐™ž๐™š ๐™๐™–๐™ฉ๐™– ๐™˜๐™๐™ค๐™ค๐™ฃ๐™ž ๐™ฃ๐™ž๐™ก๐™–๐™ก๐™š ๐™ก๐™–๐™ ๐™ž๐™ฃ๐™ž ๐™จ๐™ž๐™ฉ๐™–๐™–๐™˜๐™๐™– ๐™ ๐™ช๐™ฅ๐™ž๐™œ๐™–๐™ฃ๐™ž๐™– ๐™๐™–๐™ ๐™ž". Nilimaliza hivyo kwa sauti ya juu lengo langu lilikuwa ni mahabusu na wafungwa waliokuwa karibu wasikie. Kisha nikaondoka kwa kujiamini nikielekea selo namba 4 huku baadhi ya mahabusu wakicheka na wengine wakisikitika.

Ilionekana kuwa ofisa mkuu wa zamu mwenye cheo cha ASP hakufurahishwa mimi kuhamishiwa selo ya wendawazimu hata kama nilikuwa na mgogoro na wakuu wake. Alimuagiza Nyapara mkuu msaidizi anihamishie selo namba 16 kutoka selo namba 11 niliyokuwa nakaa awali badala ya kunihamishia selo namba 4 yenye watu wenye matatizo ya akili. Wapambe wangu wote wanne walihamishiwa selo namba 4.

Kwa hiyo nilipelekwa kwenye selo namba 16 tukafungiwa watu 82 huku mahabusu wawili tu na wengine wakiwa wafungwa. Selo hii ina uwezo wa kuchukua watu 25 tu. Kama kawaida yangu baada ya kufungiwa ndani ya selo niliingia kuoga na kurudi sehemu yangu ya kulala na kufanya ibada. Baada ya kumaliza ibada nilifungua kifungashio changu na kutoa chakula nikala kisha nikakaa kwa kueegemea ukuta huku nikisoma Biblia yangu kama kawaida.

Sasa kwa mujibu wa taratibu za magereza inapofika saa tatu usiku ni muda wa kusikiliza taarifa za habari kutoka redio mbalimbali zinazosoma habari kwa wakati huo. Baada ya taarifa hiyo ya habari, amri inatolewa na Nyapara katika selo ya kuzima redio hadi asubuhi ili kusikiliza taarifa ya habari kutoka BBC Swahili.

Ni kwamba hadi redio ya selo inazimwa saa nne usiku hapakuwa na habari mpya zaidi ya habari tunazozisikia kila siku. Kwa hiyo tulilala. Sasa kuna watu wana redio zao. Kwa hiyo amri ya kuzima redio inapotolewa, wanaendelea kusikiliza redio kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba ni vigumu kuwagundua. Naam, hawa ndio waliomsikia Makamu wa Rais Samia Suluhu akitangaza kifo cha Rais Magufuli majira ya saa tano usiku.

Kumbuka katika utawala wa Magufuli aliwahi kuamuru wafungwa wapigwe mateke na wafanye kazi mfululizo. Lakini pia kwa upande wa mahabusu kulikuwa na kilio cha kukwama kesi nyingi huku kesi za uhujumu uchumi na jinai zinachukua miaka mingi bila upelelezi kukamilika. Hivyo si wafungwa wala mahabusu waliofurahia utawala wa Rais Magufuli. Sasa wakati nasikiliza kwa makini kelele za selo ya jirani, nikamsikia mmoja wao akisema; "Mungu amesikia kilio chetu huyu mtu alisema tupigwe mateke na tufanyiwe kazi mfululizo".

Hapo ndipo nilipogundua kuwa Rais Magufuli amefariki dunia ikizingatiwa kuwa kulikuwa na tetesi za kuugua kwake siku za hivi karibuni kabla ya kifo. Niliwaambia manyapara wa selo yetu wafungue redio iwapo kuna habari za kifo cha Rais Magufuli. Ni kweli walifungua redio nikamsikia Makamu wa Rais Samia Suluhu akitangaza msiba wa kitaifa. Ndani ya selo sasa watu walishangilia na kunifuata nikiwa nimelala na kuninyanyua hadi kuniumiza mguu. Lakini sikuona hata shida kwangu licha ya kwamba niliuguza maumivu kwa wiki kadhaa.

Kifo cha Rais Magufuli kilinifundisha kuwa unapokuwa na madaraka ni muhimu kuepuka kutesa na kuumiza watu wengine. Kwa sisi wakristo YESU alituagiza tusiwatendee wengine yale tusiyopenda kutendewa. Kwa hiyo, ikiwa wewe ni Mkristo halafu ukatumia madaraka yako kuwatendea wengine usivyotaka kutendewa, hata tukiliombea kaburi lako mara elfu, ni bure mbele za Mungu Mwenyezi.

Mungu bariki Tanganyika,
Mungu bariki Zanzibar,
Mungu bariki Tanzania.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
FB_IMG_1710682599882.jpg
 
Hivi umepona miguu, haivibrate tena ๐Ÿ’

Taks fosi walikulegeza bila huruma rafiki yangu, sijapenda kabisa ๐Ÿ’
 
Back
Top Bottom