Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

?..?UTENDAJI WA MTU NDIYO UTAKAOMLINDIA HESHIMA YAKE?..hii biashara ya kulindiana heshima ndiyo imetufikisha hapa. Mahospitalini wagonjwa wanalala chini, dawa hakuna, MRI+CT Scan zinakufa eti kisa tunalidiana heshima..acha MAGUFURI ?atumbue majipu? dawa ya jipu ni kutumbua siyo kukuna .. kama mtu alipanda mchicha asitegemee kuvuna mahindi
?aaariii S E R E M A ? ?
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4
Thick mind! Acha kuishi kwa mazoea au kwa kukariri. Unless we change our mindset we wont move forward. Tubadilike. Call a spade a spade. Alichemka aambiwe tu kwani ye nani?
 
Last edited by a moderator:
Magufuli msema kweli na mtu wa mungu hapendi unafiki. Hivyo lazima aseme ukweli. Anaeona kwamba kaongea vibaya bac na yy limemgusa. Endelea baba na moyo huo huo. Natamani uwe raisi wa tz miaka 50
 
Ht ya muhimbili Kwenye hotuba alitaja..ni mapungufu ya nani ya nyerere? ?,, au museven...ukosofu wa sawa na vifaa tiba Kwenye hotuba hakuongea?

bora umenisaidia kumjibu huyu jamaa inaonyesha huyu ndio wale wapambe wa mkwere tafuteni kazi za kufanya mkwere kashapigwa chini na sasa anasikilizia maumivu hataki tena wapambe
 
Wapi amemsema Kikwete,Magufuli alikuwa anazungumzia ngazi za chini sio ngazi ya uraisi

Inasaidia nini sasa kuzungumzia ngazi za chini na kuacha ngazi ya rais!? Uhitaji kuwa na cheti cha darasa la saba kuona safari za rais zilikuwa too much na wananchi wote wanajua hilo! Na wanajua nani alilengwa kwenye hotuba hata kama haikuwa hivyo!
 
Wapi amemsema Kikwete,Magufuli alikuwa anazungumzia ngazi za chini sio ngazi ya uraisi

Wizara ipi inayoratibu safar za rais nje ya nchi?kuna watu waliripotiwa kushikwa kwa kukwapua pesa za safar za nje wizara ya mambo ya nje unaikumbuka hii???
 
Aache mabovu ya watangulizi wake, achukue mengi mema yao aunganishe na dhamira yake njema ktk kuelekea Nchi ya ahadi aliyotuahidi.

Tuwashukuru wazee hawa ktk zama zao na salama walotuachia na sasa tumuombee Magufuli atende impendezavyo Mungu na kuiepusha Tanzania kuwa ni nchi ya visingizio.

Nimefurahia neno moja jana "NCHI HII NI TAJIRI" JPM....Admission hiyo ni wazi amedhamiria kuonyesha UTAJIRI WETU ambao tangu JKN ,AHM,BWM na JMK walishindwa kutamka neno hilo hadharani.

Na Wengine walisema hawajui y nchi hii ni MASKINI
 
kuna watu wamezoea maisha ya kinafiki magufuli ni mlokole kwa uongo ni zambi kaenda hospitali kakuta watu wamelala chini sasa na hilo aseme ni mafanikio? wakati wakiulizwa hela ya panadol wanasema hela hakuna lakini za kuzurura ulaya ziko huo unafiki mtabaki nao nyie mliozoea kwa magufuli sahauni kabisa

Unasema Magufuli ni mlokole?? Wewe mlokole haupo pale! Mnafiki yeye na genge lake! Bora mnafiki anaeonekana kuliko yule ambaye umejifcha kwa kofia ya Ulokole! Wote hawata ona ufalme wa Mung
 
kwakweli kikwete alikuwa mbovu haiitaji kufichaficha..yaani kikwete na mwinyi ni matatizo matupu..
Nyerere alikuwa bora..mkapa nafuu..pia magu atakuwa nafuu..waswahili ni shida
we maku toa ushenzi wako hapa, udini tu, nyerere ametuachia barabara kilometer ngapi na jk katuachia ngapi? Nyerere katuachia shule ngapi na jk katuachia ngapi? Nyerere katuachia vyuo vikuu vingapi na jk vingapi?Yahudi wewe
 
Wakati Pombe akisema maneno hayo camera ilimzoom bwana January Makamba amekunja uso kama kaona kinyesi cha mtu mzima hadharani:banghead:

MKUU karibu sana CCM ni chama safi, naona lile kapi lenye degedege linazidi kukimbiwa, sijui litabaki na nani
 
Amesema kuwa Kikwete ameenda safari nyingi za ulaya kuliko hata safari za kwenda kusalimu nyumbani Msoga.

😀😀😀😀😀😀😀😂😂😂😂😂😂 me hapa napoish ndo njia ya bagamoyo,jamaa alikua akienda sana kwao jaman
 
Katika hotuba yake JPM hakutaja jina la JK wala ofisi yake, alitaja ofisi zingine tu kwa lengo la kulinda heshima ya Ikulu na aliyekuwemo. Tatizo la watanzania ni kukosoa kila kitu hata kama kimefanyika vizuri. Dr JPM akitenda kama JK watu watasema CCM ni ileile akitenda tofauti wanasema anawadhalilisha wenzake. Ikiwa anatenda kwa manufaa ya watanzania tumuunge mkono na kushirikiana naye, tuache unafiki, tufanye kazi.

Alipoitaja wizara ya mambo ua nje ndo Lithuli imetajwa,tutajie wizara inayoratibu safar za nje mdau
 
Mkuu,
Kwa wastaafu, ambaye atakiwi kuambiwa ukweli n rais tu. Au pia wakuu wa mikoa, mameneja na wangineo ambao amestaafu lakini waliboronga katika utawala wasiambiwe ukweli?!

mkuu, weye ulipomsikiliza uliona ile hutuba yake ilikuwa inahusu wakuu wa mikoa au ilikuwa inawahusu marais wastaafu waliotufikisha hapa ulipo? ulimsikiliza au ulimsikia tu?
 
mawazo mgando kama haya inabidi yapingwe kwa nguvu zote.Upuuzi aliofanya kikwete angekuwa raisi sehemu nyingine kama marekani angekuwa marehemu.Huwezi kutumia office ya raisi namna ile,na uppuzi wako kutetea ujinga na upumbavu haukubaliki.

goo magufuli.
 
magufuli yupo sawa, tulikuwa tunahitaji mabadiliko na hayo ndiyo yenyewe, kwani nani asiye yajua madudu ya kikwete, mleta mada ww ni bavicha nyumbu kwanza mlitoka bungeni hayo maneno umeyasikia wapi
 
Magufuli bado ni trainee kwny ajira yake hii mpya, bila shaka anahitaji sana msaada wa ushauri toka kwa watangulizi wake....kuwadhalilisha hadharani ni nzuri kwa upande wake hasa akihitaji sifa za waliomchagua, ila ni mbaya sana pale atakapohitaji msaada toka kwa kaka zake, mfano kwny mgogoro wa Zanzibar kina Mkapa na Kikwete wanahitajika sana#

Hebu tujikumbushe ya Mkapa alieingia madarakani akiwa msafi hana doa (Mr Clean), lakini alikuja kumaliza uongozi wake akiwa amechafuka kupindukia!

Kila lakheri Dk Magufuli, ila angalia usije ukatukana mamba kabla hujavuka mto!
Mkuu kwanza heading yako inashangaza,hata kama upendi modus operandi ya Dk.Magufuli kumbuka kwamba hivi sasa ndiye Rais wa Taifa letu hivyo it does not cost U a penny kutumia lugha ya staha na kumuheshimu.

Haya mambo ya kujaribu kumtisha tisha Mh.Magufuli as if hana uwezo wa ku- stand on his own feet hayatawafikisha popote,unawezaje kubeza beza mtu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini Serikalini akiwa na wadhifa wa Uwaziri,hapa mnaleta porojo tu za kujaribu kumkatisha tamaa!

Unaweza kuwa fafanulia members JK alikuwa na uzoefu wa miaka mingapi Serikalini kama Waziri kabla hajawa Rais - hilo hamlisemi kazi yenu kumkandia Dk.Magufuli.

Hapa mnakazania kwa kudai eti "Dk. kamdhalisha JK!" Kamdhalalisha kivipi,kama mnafikiri ni suala la safari za nje mimi sikumbuki kama Mh.Magufuli alitaja popote kuhusu Ofisi ya Rais,hakulitaja hilo 4 a good reason namely he knew safari za JK zilileta mafanikio makubwa kwa Taifa letu in terms of uwekezaji,ujenzi/upanuzi wa Mahospitali,barabara, umeme vijijini,mawasiliano nk hakuna mtu a
mbae anaweza kusahau mchango wake kwa Taifa letu bila ya kujali mapungufu yake ya kibinadamu kama sisi wote tulivyo. Dk.Magufuli ana uhuru wa kuomba ushauri kutoka kwa mtu yeyote Duniani, hakuna sheria inayo mlazimisha kupata ushauri kutoka kwa Marais wastaafu.
 
Full ujnga yaan mtu kaboronga asiambiwe kisa ni rais huo ni utumwa wa mawazo tena nampongeza hajapepesa macho wala kuwa na kgugumizi kamchana live,,, hapo angalau kdg
 
Kwa kweli huyu JPJM alipaswa kushauriwa kuweka akiba ya maneno. Yaani amezungumza mengi kuliko ilivyokuwa lazima. Kuna mambo mengine ambayo alipaswa kuyanyamazia na kuacha matendo yake yafikishe ujumbe kunakohusika. Binafsi nafikiri tumepata raisi mpenda sifa na mwenye papara; sijui kama kweli anashaurika! Kweli naogopa iko siku tutajuta kimweka madarakani.

umenena ukweli mtupu mkuu....kuna watu wako kifua mbele kutetea huu udhalilishaji sijui wao baba yao angedhalilishwa kama vile ingekuwaje...kumbuka kwamba ridh1 alikuwemo mule ndani akishuhudia namna baba yake anavyodhalilishwa bila sababu. kuna watu wanadhani hili suala ni sawa lakini sio sawa hata kidogo.
 
Back
Top Bottom