Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Hapa ukweli tu unataka wafiche nn sasa wewe unataka tusiwe ngu ndani mguu nje
 
Ndiyo presida wenu.Hapa kazi tuu. Hana diplomasy nanyi mlimweka madarakani awatetee
Kwa kweli huyu JPJM alipaswa kushauriwa kuweka akiba ya maneno. Yaani amezungumza mengi kuliko ilivyokuwa lazima. Kuna mambo mengine ambayo alipaswa kuyanyamazia na kuacha matendo yake yafikishe ujumbe kunakohusika. Binafsi nafikiri tumepata raisi mpenda sifa na mwenye papara; sijui kama kweli anashaurika! Kweli naogopa iko siku tutajuta kimweka madarakani.
 
Majipu yameanza kutumbuliwa naona wenye nayo mnalalamika,tumbuanga hayo jpm
 
Uchonganishi tu ndio kazi yenu.

sasa hapa ni nani kamchonganisha nani? je, ni kikwete kamchonganisha magufuli au ni magufuli anayemchonganisha kikwete? hebu wewe tueleze kama kitendo hiki ambacho magufuli kamfanyia kaka yake, mh kikwete, ni cha halali au la? usipofanya hivyo, tutajua wewe ndiye mchonganishi, tena mchonganishi kungwi!
 
Magufuli bado ni trainee kwny ajira yake hii mpya, bila shaka anahitaji sana msaada wa ushauri toka kwa watangulizi wake....kuwadhalilisha hadharani ni nzuri kwa upande wake hasa akihitaji sifa za waliomchagua, ila ni mbaya sana pale atakapohitaji msaada toka kwa kaka zake, mfano kwny mgogoro wa Zanzibar kina Mkapa na Kikwete wanahitajika sana#

Hebu tujikumbushe ya Mkapa alieingia madarakani akiwa msafi hana doa (Mr Clean), lakini alikuja kumaliza uongozi wake akiwa amechafuka kupindukia!

Kila lakheri Dk Magufuli, ila angalia usije ukatukana mamba kabla hujavuka mto!

Mkapa alichafuka hata kwa jiki hang'ai!!!!
 
sasa hapa ni nani kamchonganisha nani? je, ni kikwete kamchonganisha magufuli au ni magufuli anayemchonganisha kikwete? hebu wewe tueleze kama kitendo hiki ambacho magufuli kamfanyia kaka yake, mh kikwete, ni cha halali au la? usipofanya hivyo, tutajua wewe ndiye mchonganishi, tena mchonganishi kungwi!

mchonganishi ni wewe,ukilala na kuamka magufuli,muache afanye kazi.na sijaona mahali kamdhalilisha kikwete hayo ni yako na mwisho Wako wa kufikiria.nguvu kubwa unayotumia kumshusha magufuli ndio kwanza unampandisha chati.
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Safari za Nje bado zipo isipokuwa sasa wamebadili mbinu wanasafiri kwa Siri kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mambo kama tusipobadilika hali yetu itazidi kuwa mbaya zaidi,Taifa zima kuanzia viongozi hadi wananchi tunapaswa kubadilika.Magufuli yote aliyoongea ni ukweli tuache unafiki

Kubadilika ni vigumu sasa maana asilmia kubwa ya watu waliomweka ikulu ni watu wa JK na mkapa huku wengi wakiwa ni wapiga dili wakubwa.
 
Tena ya Kikwete nadhani kuna aliyoyaacha Magufuli kiporo, atayasema huko mbele ya safari. Nadhani mleta mada hujui madhara na maafa yaliyosababishwa na safari za Kikwete. Ilitakiwa Magufuli amchimbe kisawasawa hata ikibidi amchunguze mali walizovuna na familia yake. Haiwezekani watu wake walikuwa wanakufa mahospitalini yeye kageuka Christofa Columbus! Ila hili inaweza kuwa iko njiani.
Pia yule mwanae aliyekuwa akichimba mikwara kwenye mitandao na yeye achunguzwe huku mfumo wa Uongozi wote ukitumbuliwa majipu huenda Magufuli atafanikiwa kwa 10% lakini akishindwa kitumbua majipu hatafanikiwa mpaka anamaliza mda wake.
 
Wakati Pombe akisema maneno hayo camera ilimzoom bwana January Makamba amekunja uso kama kaona kinyesi cha mtu mzima hadharani:banghead:
 
Katika hotuba yake JPM hakutaja jina la JK wala ofisi yake, alitaja ofisi zingine tu kwa lengo la kulinda heshima ya Ikulu na aliyekuwemo. Tatizo la watanzania ni kukosoa kila kitu hata kama kimefanyika vizuri. Dr JPM akitenda kama JK watu watasema CCM ni ileile akitenda tofauti wanasema anawadhalilisha wenzake. Ikiwa anatenda kwa manufaa ya watanzania tumuunge mkono na kushirikiana naye, tuache unafiki, tufanye kazi.
 
mchonganishi ni wewe,ukilala na kuamka magufuli,muache afanye kazi.na sijaona mahali kamdhalilisha kikwete hayo ni yako na mwisho Wako wa kufikiria.nguvu kubwa unayotumia kumshusha magufuli ndio kwanza unampandisha chati.

Amesema kuwa Kikwete ameenda safari nyingi za ulaya kuliko hata safari za kwenda kusalimu nyumbani Msoga.
 
Hizo njemba ndo zitamkwamisha Magu. Zilikaa zinamwangaliaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! Huku zinasema, ngoja aonje biashara aje aone Muziki wa utamu wa hela za Ikulu. Tena baadhi yatatumwa kumrubuni ili aharibu.
 
wacha waisome namba, na wakimsumbua wote atakamata. wana tuhuma nyingi mno
 
We mleta mada na wewe unaishi kwenye dunia hii,huna hata hofu ya Mungu.Binadamu hapaswi kusujudiwa.
 
Magu alichosema ni black and whote kuhusu udhaifu wa serikali iliyopita. Yeye pia alikuwemo. Hakumtaja JK kwa safari lakini indirectly ilimhusu
 
Hakumdhalilisha kiongozi yoyote alichosema ni ukweli na alikwisha sema mbele ya Rais Kikwete kwenye majukwa ya kampeni kuwa kuna watu aliwaamini lakini walikuwa wanafiki ndiyo waliyotufikisha hapa na alikuwa kabla hajasema alikuwa anamuomba Rais Kikwete na alipewa ruhsa ya kusema. Hapo ni ukweli mtupu hakuna unafiki.
 
Kwani Zanzibar kuna mgogoro? Kama upo unamhusu nini Magufuli ilhali Zanzibar ni nchi yenye katiba yake?
 
Back
Top Bottom