Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Una akili ndogo sana.
 
Last edited by a moderator:
kuna watu wamezoea maisha ya kinafiki magufuli ni mlokole kwa uongo ni zambi kaenda hospitali kakuta watu wamelala chini sasa na hilo aseme ni mafanikio? wakati wakiulizwa hela ya panadol wanasema hela hakuna lakini za kuzurura ulaya ziko huo unafiki mtabaki nao nyie mliozoea kwa magufuli sahauni kabisa

Waambie mkuu wamezoea kuishi kinafiki tu.
 
Wakiugua hata mafua wanakwenda ulaya haya issue ya kufungulia maji mtera nayo magufuli akae kimya eti?
 
imemuuma sana jk jana kiasi kwamba hata coctail part hakuudhulia alijirudia zake dar jioni ile ile baada ya bunge
 
Ndiyo presida wenu.Hapa kazi tuu. Hana diplomasy nanyi mlimweka madarakani awatetee
 
kuna watu wamezoea maisha ya kinafiki magufuli ni mlokole kwa uongo ni zambi kaenda hospitali kakuta watu wamelala chini sasa na hilo aseme ni mafanikio? wakati wakiulizwa hela ya panadol wanasema hela hakuna lakini za kuzurura ulaya ziko huo unafiki mtabaki nao nyie mliozoea kwa magufuli sahauni kabisa
Magufuli ni mkatoliki
 
Kwani kamsingizia?!
Urafiki ndio uliotufikisha hapa kama Taifa!
Mabilioni yaliyofujwa yangeweza kusaidia masikini wengi badala ya kundi la wajanja wachache!
 
Kama sijasahau JK alipata kusema kwamba, akishinda Magufuli atapata Usingizi. I truly hope he sleeps in peace now.
 
Tena ya Kikwete nadhani kuna aliyoyaacha Magufuli kiporo, atayasema huko mbele ya safari. Nadhani mleta mada hujui madhara na maafa yaliyosababishwa na safari za Kikwete. Ilitakiwa Magufuli amchimbe kisawasawa hata ikibidi amchunguze mali walizovuna na familia yake. Haiwezekani watu wake walikuwa wanakufa mahospitalini yeye kageuka Christofa Columbus! Ila hili inaweza kuwa iko njiani.
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Wewe ni ndugu ya jk? Huyo Jk wako hastahili hata kuwepo uraiani...anahitajika mahakama ya mafisadi.
Huwezi kua rais na vile vile mshiriki mkubwa wa ukwepaji kodi-kosa la jinai
Safari 1800+ bila ya mpango unaenda hadi montego bay, Jamaica kufanya nini kwa kutumia hazina yetu na huku pesa zinabebwa cash kwenye mabegi kuficha ushahidi hili ni kosa la matumizi mabaya ya ofisi
Lazima ifike wakati tuwe na utamaduni wa kutokulindana ili twenge mbele. Mwambie uncle jk atafute Chaka la.kujificha huko ulaya alipoficha billioni zake.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Chadema mnataka Dr.Magufuli afanye nini ili mfurahi???
 
Watz mnapenda siasa na kusifiwa ata kama mnabolonga.
Inchi iko hoi kifedha alichoongea JPM ni ukweli mtupu usikute nawe ni mhanga wa safari za nje.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.Kumbuka CAG nae Aliwai fanya audit on the same na report zipo sijui nae alikuwa anamnanga JK
Kamua tweende baba JPM tuko nyuma yako
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4
JF kuna vituko pro-Chadema anaumizwa na CCM ni sawa sawa kocha wa Taifa Stars akitoa ushauri kwa Argentina kwa timu yao mbovu.
 
Last edited by a moderator:
Wakati huu ndio tuliosubiri,tunataka nchi isonge mbele lazima tumuunge mkono Magufuli atumbue majipu.

Mh magufuli endelea kutumbua majipu
Makubwa makubwa
Na madogo pia

Ukiona mtu anamlalamikia mh rais wakat anatumbua majipu hayo
Ujue na yy amedondokewa usaha

viva jpm
Rais wa kihistoria
Rais mzalendo
 
Dah! Vasco Da Gama alizipata ngumi za uso Jana. Bwana Pombe alimnywea na kupata ujasiri wa kumtwanga live bila chenga.
 
wapumzike!!!how tpaul wakat suala hilo linawahusu?me naona awachanechane tu hakuna namna,
hivimmesahau tulipoambiwa zile safar zilikua na tija?tungelala njaa?tungekula mihogo?kama zonaweza jenga barabara ya lami km 400 maana yake zile safat hazikua na tija wadau
 
Last edited by a moderator:
Wakati huu ndio tuliosubiri,tunataka nchi isonge mbele lazima tumuunge mkono Magufuli atumbue majipu.

Mh magufuli endelea kutumbua majipu
Makubwa makubwa
Na madogo pia

Ukiona mtu anamlalamikia mh rais wakat anatumbua majipu hayo
Ujue na yy amedondokewa usaha

viva jpm
Rais wa kihistoria
Rais mzalendo
 
Sioni jinsi Kikwete anavyodhalilishwa.Na hata kama anadhalishwa,kwani sisi hakutudhalilisha kwa kuharibu uchumi wa nchi yetu?Watu wamekuwa ombaomba,ndoa za watu zimevunjika kwa kuwa wanaume ni maskini,wanaume wamedharauliwa na wake zao,watoto na hata wazazi kwa kuwa wameshindwa kuwahudumia kwa sababu ya kipatato kidogo,social standing za watu zimeharibika kwa sababu ya umaskini nk.nk.Sasa mtu kama huyu ambaye amewafanyia unyama wa namna hii watanzania ana uhalali gani wa kusema anadhalilishwa?Sikuelewi na wala sitakuelewa.Alipokuwa anatumia trillions kwa safari za nje hakujua kwamba kitendo hicho kitawafukarisha watanzania kwa ujumla wao.Sikuelewi,sikuelewi,sikuelewi.Mkuki kwa nguruwe,kwa binadamu mchungu.

Back
Top Bottom