Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

umenena ukweli mtupu mkuu....kuna watu wako kifua mbele kutetea huu udhalilishaji sijui wao baba yao angedhalilishwa kama vile ingekuwaje...kumbuka kwamba ridh1 alikuwemo mule ndani akishuhudia namna baba yake anavyodhalilishwa bila sababu. kuna watu wanadhani hili suala ni sawa lakini sio sawa hata kidogo.

Great! I like people like you whose conscience is still intactg
 
hapa hakuna kuremba mwandiko!
hotuba ya jpm ni ujumbe tosha kwa vibaraka na wanaodhan kuwa jk bado anaweza kuwatetea kwenye maslahi yao!
ni taarifa tosha kuwa jk is nobody! so wajiandae kunyonyolewa!!
wazee wa ngada, vijisent, popoos, etc.
Yeyote anayelalamikia hotuba ile ujue ni jipu!
 
mkuu, weye ulipomsikiliza uliona ile hutuba yake ilikuwa inahusu wakuu wa mikoa au ilikuwa inawahusu marais wastaafu waliotufikisha hapa ulipo? ulimsikiliza au ulimsikia tu?

Sikumpa kurayangu, lakini utanisamehe jipu.
Tumbuliwa tu!.
 
Malipo ni hapahapa dunian,jk alimshambulia mno mkapa,ila magufuli aende taratibu,vinginevyo mmh!
 
Mto hauna maji ya kujificha Mamba tena huu. Huyo Kikwete anatukanwa wapi wakati katumia raslimali zote kujinasibu yeye na rafiki zake huku akiwaacha watanzania wakiuawa na serikali yake na wegi tu wakikosa huduma muhimu za jamii?
 
MKUU karibu sana CCM ni chama safi, naona lile kapi lenye degedege linazidi kukimbiwa, sijui litabaki na nani
Hii lugha unayotumia haionyeshi kama wewe ni mtu uliyestaarabika,jaribu kuwa na busara ndugu.
 
faizagoxy aka mkufunzi wa mogadishu na simiyu kwetu njooni humu
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Unafahamu maana ya neno kudhalilisha?

Eleza wapi kwenye hotuba yake, raisi JPM amemdhalilisha Kikwete na maraisi wengine walopita.

Mbona neno udhaifu umelitumia sana kwenye hoja yako?

Mbona umetahayari na kughafirika kiasi hicho?
 
Watanzania sisi ni wajinga. sasa mabadiliko tuliyo yataka ni yepi kama tunalialia kila tunapoona kiongozi anataka alete mabadilikooo? Ujinga huu tutabaki hapahapa. nawashauri tumtie moyo Rais wetu tusonge mbele. Acheni utoto mayai mnataka mabadiliko gani? ni lazima aseme ukweli ili wahusika wajue tulikuwa hatujatendewa haki.

Wanaobeza juhudi za jpm no wale ng'ombe jamaa alosema atakuwa akichunga baada ya uchaguzi. Achana nao.
 
Tukuunge mkono hata ktk upuuzi wako uliotoa..wacha atumbue jibu hakuna namna.
 
Ni anapaka mbovu c mchezo,maccm wamechanganyikiwa.Penye madawa ya kulevya hapo sijui kama ataweza maana majamaa hayo mmh
 
Asije kuharibu kwa kufanya kazi kwenye vyombo vya habari kama inavyojionyesha kwasasa!afanye kazi kwa kufuata taratibu murua mambo ya magazetini na radioni awaachie wasanii
 
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!

Mnafiki ni wewe unayetaka rais asiseme yanayomkera.nchi hii tabia ya kuoneana aibu ndio imetufikisha hapa.sasa lazima tubadilike mabaya yasemwe hadharaani ili watu wajifunze.ulitaka magufuli akayaongelee wapi mambo yale ili watanzania tumsikie?
 
Mkuu, endana na maudhui makuu ya mada. Hatuzungumzii mambo ya Muhimbili, bali hotuba za JPM kuanika mapungufu ya JK huku JK mwenyewe akiwa hapo hapo.

Mkuu ulitaka asemee uvunguni mwa kitanda? Huyu si mnafiki
 
Mkuu wew ni kati ya watanzania wanafiki ambao hawaitakii mema nchi hii. Tuambie ni wap kwenye hotuba Rais kawadhalilisha wazee hawa, ulitaka aongee uongo upate cha kuandika? halafu wew si ulikuwa haumtak JPM... Lizee kizima limejaa unafikinafiki tu... watu kama nyie hamlitakii mema taifa hili... otherwise na wew ni mnufaika wa mfumo mbovu wa utawala, ni kati yawabinafsi wa nchi hii
 
Magufuli hana hekima angejifunza kwa Lowassa pamoja na kushambuliwa hata na JK yeye hakumjibu. Hata hvyo malipo hapa hapa duniani na JK alimshambulia Lowassa kwa hiyo asikasirike.
Watanzania kweli Malaga na wapumbavu Kama alivyosema mkapa, ni mara ngapi Hapa JF mmekuwa mkiomba kupata rais dikteta kwamba marais wapole wanadidimiza nchi sasa mmepatikana magufuli lazima awanyooshe, baba zetu walizoea kutotumia mishahara, walitegemea posho za safari.Msukuma atawanyooolosha mpaka mkae mguu sawa.
 
Back
Top Bottom