Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Ukweli na usemwe kama msamaha wataomba baadaye na hii itasaidia kuondoa kulindana kwenye uovu. Kama na yeye atavurunda atakayekuja baada yake atamnyooshea kidole tuache unafiki wa kulialia kila siku eti nchi imeharibiwa na hatutaki kuwataja walioiharibu eti tunaogopa wasijeacha kutoa ushauri kwani wazee wenye hekima nchi hii wameisha? Au kwakuwa wao si maarufu? Punguzeni kula sembe watanzania.
 
Magufuli bado ni trainee kwny ajira yake hii mpya, bila shaka anahitaji sana msaada wa ushauri toka kwa watangulizi wake....kuwadhalilisha hadharani ni nzuri kwa upande wake hasa akihitaji sifa za waliomchagua, ila ni mbaya sana pale atakapohitaji msaada toka kwa kaka zake, mfano kwny mgogoro wa Zanzibar kina Mkapa na Kikwete wanahitajika sana#

Hebu tujikumbushe ya Mkapa alieingia madarakani akiwa msafi hana doa (Mr Clean), lakini alikuja kumaliza uongozi wake akiwa amechafuka kupindukia!

Kila lakheri Dk Magufuli, ila angalia usije ukatukana mamba kabla hujavuka mto!


Ni nani aliemchafua??
 
Wewe Muweka Mada Ndo umesema hayo na kufanya hayo, KUWAPONDA NA KUWADHALILISHA MARAIS WALOPITA, Alichofanya Magufuli ni kutimiza wajibu wake wakupunguza matuizi na kutatua kero za wananchi na ukumbuke katika safari hizo hakumtaja Rais mfano aliotoa ni wale walokuwa wakienda kimafunzo akasema kama upo uwezekano wa huyo mtaalam kuletwa kwanini Asiletwer tz?? Je hapo panahusiana na rais??? kingine aligusia wizara zote zilokuwa na matumizi mengi ya safari za nje ikiwepo bunge, hajamtaja kiongozi yoyote, ila ametimiza wajibu wakutueleza atapambana vipi kupata kipato ili kutimiza ahadi zetu, kumbukeni angesema elimu bure, maji bure sijui nini bure mngeanza kuuliza chanzo cha mapato atapata wapi, kwahiyo amewaonyesha jinsi atakavyopata pesa na kutatua kero zetu, mfano mdogo sherehe ya kujipongeza bungeni imezaa vitanda 500 na godoro 500 acheni unafiki wenu, tujengeni nchi hajadhlilisha mtu bali ametimiza wajibu wake, acheni kuparaganya maneno.
 
Magufuri alilitaja Bunge, Wizara ya Mambo ya Nje, Ofisi ya Waziri Mkuu n.k kama Ofisi zilizoongoza kwa matumizi makubwa mno ya safari za nje. Hakumtaja JK wala Ikulu katika hili. Ana akiri kuliko mnavyofikiria. Aliliacha hewani ili watu wajishuku wenyewe
 
Wewe Muweka Mada Ndo umesema hayo na kufanya hayo, KUWAPONDA NA KUWADHALILISHA MARAIS WALOPITA, Alichofanya Magufuli ni kutimiza wajibu wake wakupunguza matuizi na kutatua kero za wananchi na ukumbuke katika safari hizo hakumtaja Rais mfano aliotoa ni wale walokuwa wakienda kimafunzo akasema kama upo uwezekano wa huyo mtaalam kuletwa kwanini Asiletwer tz?? Je hapo panahusiana na rais??? kingine aligusia wizara zote zilokuwa na matumizi mengi ya safari za nje ikiwepo bunge, hajamtaja kiongozi yoyote, ila ametimiza wajibu wakutueleza atapambana vipi kupata kipato ili kutimiza ahadi zetu, kumbukeni angesema elimu bure, maji bure sijui nini bure mngeanza kuuliza chanzo cha mapato atapata wapi, kwahiyo amewaonyesha jinsi atakavyopata pesa na kutatua kero zetu, mfano mdogo sherehe ya kujipongeza bungeni imezaa vitanda 500 na godoro 500 acheni unafiki wenu, tujengeni nchi hajadhlilisha mtu bali ametimiza wajibu wake, acheni kuparaganya maneno.
 
Ni kuogopana na kuoneana aibu kumetufikisha hapa tulipo kwa kudai tunafuata utaratibu na ustaarabu. Ili kuendelea tunahitaji mtu tofauti anayeganya Kazi tofauti na ilivyo zoeleka na asiyeogopa kwenda kinyume na mazoea na ustaarabu kama Magufuli. Huo ustaarabu wenu wa kuogopana sio wakati wake sasa
 
Nilichogundua mpaka sasa. Wale ambao hawakua wanachama hai wa ccm wanafurahishwa sana na Maguful na kusema kura zao hazikupotea bure. Lakini ajabu wale wanachama haswa na makada wa ccm wanaanza kumuogopa Maguful na kuisoma namba wao wenyewe.

Viva president, endelea kutumbua majipu ya ccm.
 
Mficha maradhi kifo kitamuumbua. Hayo ndo majipu yenyewe!
 
unless una agenda ya kupinga maendeleo au ni mnufaika wa maovu yaliyotufikisha hapa..HOTUBA ni kwa manufaa ya wengi na unafiki si mzuri.
 
Mnafiki ni magufuli mue na kumbukumbu alikua anazitetea ata posho za wabunge zilipoibuliwa na kambi ya upinzani.
 
Mkuu kwanza heading yako inashangaza,hata kama upendi modus operandi ya Dk.Magufuli kumbuka kwamba hivi sasa ndiye Rais wa Taifa letu hivyo it does not cost U a penny kutumia lugha ya staha na kumuheshimu.

Haya mambo ya kujaribu kumtisha tisha Mh.Magufuli as if hana uwezo wa ku- stand on his own feet hayatawafikisha popote,unawezaje kubeza beza mtu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini Serikalini akiwa na wadhifa wa Uwaziri,hapa mnaleta porojo tu za kujaribu kumkatisha tamaa!

Unaweza kuwa fafanulia members JK alikuwa na uzoefu wa miaka mingapi Serikalini kama Waziri kabla hajawa Rais - hilo hamlisemi kazi yenu kumkandia Dk.Magufuli.

Hapa mnakazania kwa kudai eti "Dk. kamdhalisha JK!" Kamdhalalisha kivipi,kama mnafikiri ni suala la safari za nje mimi sikumbuki kama Mh.Magufuli alitaja popote kuhusu Ofisi ya Rais,hakulitaja hilo 4 a good reason namely he knew safari za JK zilileta mafanikio makubwa kwa Taifa letu in terms of uwekezaji,ujenzi/upanuzi wa Mahospitali,barabara, umeme vijijini,mawasiliano nk hakuna mtu a
mbae anaweza kusahau mchango wake kwa Taifa letu bila ya kujali mapungufu yake ya kibinadamu kama sisi wote tulivyo. Dk.Magufuli ana uhuru wa kuomba ushauri kutoka kwa mtu yeyote Duniani, hakuna sheria inayo mlazimisha kupata ushauri kutoka kwa Marais wastaafu.

taratibu mkuu, angalia na wewe usije ukawa unalolitenda hilo unalokemea. sijui kwa nini umeulizia uzoefu wa jk serikalini ila jk alikuwa deputy minister (1988 - 1990) na full minister kuanzia 1990 - 2005. safari za nje za raisi zinatayarishwa na wizara ya mambo ya nje hivyo safari za jk zimetajwa pia.
 
Magufuli hana hekima angejifunza kwa Lowassa pamoja na kushambuliwa hata na JK yeye hakumjibu. Hata hvyo malipo hapa hapa duniani na JK alimshambulia Lowassa kwa hiyo asikasirike.

Acha zako Lowasa ni Lowasa na Magufuli ni Magufuli ni watu wawili tofauti ninyi ndio mlio kuwa mnaishi kwa madili kipindi cha jk
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo...
Mnafiki mkubwa. Wewe utaendelea kulia na kujifuta machozi hadi mwisho wa Dunia hii.
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4
Wewe ni mpumbavu na lofa. CCM ya sasa ni mpya!
 
Back
Top Bottom