Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Mleta mada pwaaaaaa shz typ nyie ndy mlikuwa mnufaika na uongz wa mkwer! Mshazoea kuongeza 0 na 10%, naona kwa sasa umekula kwrnuuuu.. tpaul
 
Last edited by a moderator:
JPM ahakikishe dhahabu zinazozalishwa na migodi mikubwa zinatunzwa Benki Kuu ya Tanzania. Sio kupelekwa nje ya nchi moja kwa moja. Wakitaka kuuza wanachukua BOT kama ambavyo mwenye akaunti anavyochukua pesa zake benki. Hivyo ndivyo uchumi wa dhahabu unavyoendeshwa dunia nzima ukizingatia kuwa hata mwenendo wa thamani ya pesa unategemea thamani ya dhahabu.
 
Mbona Lowassa alidhalilishwa utazani hakuwa kiongozi mstaafu wa kitaifa?

Malipo ni hapa hapa duniani.
Na laigwanan alikuwa kimya hakujibu! Mkwer na bado atalambishwa sana shubiri
 
Kwakweli kikwete alikuwa mbovu haiitaji kufichaficha..yaani kikwete na mwinyi ni matatizo matupu..
Nyerere alikuwa bora..mkapa nafuu..pia magu atakuwa nafuu..waswahili ni shida
 
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!

wazee wako kivipi mkuu...alichosema magufuli ni uongo?shame on us blacks..ndo maana kina trump wanatutukana kila siku kwa ujinga na unafki km huu..binafsi sikumpigia kura magufuli lkn ktk hili kanikosha kwelikweli...tuache unafki,..yaani unataka mzee akinya ss tuseme kakojoa?!!wenze2 wanafikiria kwenda kuishi mwezini,cc hata kuusema ukweli ulio dhahiri tabu...kazi tunayo
 
,hakuna cha Jk sijui membe ,mmeyataka wenyewe .. ... Wacha waisome namba .
 
Acha utoto. Muache Raisi awape ukweli.
 
Mleta mada nadhani imemgusa, kama alikua si mdufaika wa safari hizi basi at least wa karibu nae walikua wanufaika. Ila kama hakua na manufaa yoyote na safari za nje za viongozi basi nadhani mleta mada ni mnafiki anayejifanya kuwa muungwani wakati hana lolote.
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

...acha kujitia upofu, umesahau Kikwete alivyomshambulia Mkapa kwenye kuzindua bunge Disemba 30, 2005? yy atulie ashakula bata inatosha, acha wanaume wachape kazi, #HapaKaziTu
 
Last edited by a moderator:
Ninashauri tumwelewe Mhe Magufuli kila mara anajitambulisha kwa kusema kuwa "msema ukweli ni mpenzi wa Mungu", na ndicho anachofanya!
 
Mh. Rais ameongea ukweli ! Hakupenda awe mnafiki kwa kuwafurahisha baadhi ya wanafiki waliomo serikalini. Wabadhilifu na majizi ya rasilimali na fedha za umma TINGATINGA hilo. Hapa kazi tuuuiiu
 
Nionavyo mimi hiyo ni namna/njia ya kuwapunguza nguvu upande wa pili na hata kuwashinda. Sometimes you need to adopt your opponent ideas kuweza kwenda naye sawa au kumshinda.
Tangia wakati wa kampeni, njia iliyotumika ya kuongea lugha ya upinzani ilikuwa ni mpango maalum kwa watu wa kawaida kurudisha imani kwa chama kupitia kwake.
 
Magufuli hana hekima angejifunza kwa Lowassa pamoja na kushambuliwa hata na JK yeye hakumjibu. Hata hvyo malipo hapa hapa duniani na JK alimshambulia Lowassa kwa hiyo asikasirike.

....umesahau alivyomshambulia Mkapa, acha apate za uso, eti anatengeneza mahusiano!!!! Shame on us
 
Nimekumbuka maneno ya Dr.slaa kuwa.. ukweli hauwezi kuwa na pande mbili lazima uegemee upande mmoja.
 
Magufuli hana hekima angejifunza kwa Lowassa pamoja na kushambuliwa hata na JK yeye hakumjibu. Hata hvyo malipo hapa hapa duniani na JK alimshambulia Lowassa kwa hiyo asikasirike.


Yeah, magufuli kasema ukweli wake na data zinaonyesha, kusema ukweli ndo kumdhalilisha mtu, mwache afichue maovu yao
 
Mh.Raisi Kikwete alisema namnkuu "Mie mnasema Mpole anakuja Mkali" vyo vyote mtavyosema Raisi mstaafu aliuhabarisha Umma.
 
Back
Top Bottom