Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!
Mshazoea kuishi kisanii sania kinafki nafki! Magufuli anatumiaa sera za ukawa a kuwa komeshaaa na bado
Jk alikuwa mzigo tu kwa nchi hii bora amemaliza muda wake duh
 
Watanzania sisi ni wajinga. sasa mabadiliko tuliyo yataka ni yepi kama tunalialia kila tunapoona kiongozi anataka alete mabadilikooo? Ujinga huu tutabaki hapahapa. nawashauri tumtie moyo Rais wetu tusonge mbele. Acheni utoto mayai mnataka mabadiliko gani? ni lazima aseme ukweli ili wahusika wajue tulikuwa hatujatendewa haki.
 
kuna watu wamezoea maisha ya kinafiki magufuli ni mlokole kwa uongo ni zambi kaenda hospitali kakuta watu wamelala chini sasa na hilo aseme ni mafanikio? wakati wakiulizwa hela ya panadol wanasema hela hakuna lakini za kuzurura ulaya ziko huo unafiki mtabaki nao nyie mliozoea kwa magufuli sahauni kabisa
Mkuu, endana na maudhui makuu ya mada. Hatuzungumzii mambo ya Muhimbili, bali hotuba za JPM kuanika mapungufu ya JK huku JK mwenyewe akiwa hapo hapo.
 
Umasikini wa Watanzania ni unafki wao..tulikuwa tunamlaani Kikwete kwa kusafiri sana mpaka tukamwita Vasco da gama, leo amepatikana mtu wa ngazi ya juu kukemea hilo ili iwe onyo kwa watendaji wengine tunaanza kulalamika. Wa-tz unafiki utatuangamiza.

Halafu mleta mada kihistoria ni wa mrengo wa pili, inabidi tusugue akili maana madhaifu mengi tuliyokuwa tunaipigia ccm kelele inaelekea huyu "ulabu" ameyatolea macho! Tukumbuke "Mjinga akierevuka mwerevu huwa matatani"
 
Hakumponda raisi,raisi hyo ni kazi yke kwenda nje na kujenga mahusiano Mazuri na nchi jirani..aliponda baadhi ya safari za Idara za serikali kwenda nje hovyo hovyo..Mimi hapa mwenyewe nashuhudiaga wakurugenzi wa Idara za benki kuu wakienda kutanua Malaysia na Singapore kila baada ya mieZi mitatu

Labda nikukumbushe, safari nyingi za Rais zinaratibiwa Wizara ya Mambo ya nje..
 
Tahadhari hawa wote ni wasani wanajaribu kucheza na akili zetu maneno siyo sumu tuzinduke!
 
kuna watu wamezoea maisha ya kinafiki magufuli ni mlokole kwa uongo ni zambi kaenda hospitali kakuta watu wamelala chini sasa na hilo aseme ni mafanikio? wakati wakiulizwa hela ya panadol wanasema hela hakuna lakini za kuzurura ulaya ziko huo unafiki mtabaki nao nyie mliozoea kwa magufuli sahauni kabisa

magufuli mlokole?mlokole anasali st peters?mlokole anahonga nyumba hawara
 
Watanzania hamueleweki? Mnalalama matumizi ya serikali makubwa halafu Kaja mtu msema kweli anaguza maeneo ya kuthibiti na Anglia tena Huyu mleta Uzi anasema nini. Nahisi huyu bwana Ana bifu n.a. Magufuli n.a. atapinga chochote atakachokifanya. Poor you.

Imemuuuma ati, na sie tunasema kama kaumizwa basi yeye aitishe bunge na yeye atoe hotuba ya kwake ...watu kama huyu mleta uzi ndo wanatusababishia maisha magumu na tunatakiwa tuwatupe magerezani
 
Mimi nakushangaa sana wewe mleta uzi unayetaka chepe liitwe kijiko kikubwa badala ya jina lake halisi "CHEPE". Magufuli nakuunga mkono endelea hivyo hivyo kuwapa za usoni tena kavukavu ili wajijue walivyoboronga wakati wa utawala wao.Tusipoondoa unafki hii nchi haitaendelea kamwe.
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Umewaza vema
 
Last edited by a moderator:
Majipu ni mengi na yataendelea kutumbuliwa tu.

Jitihada na dhamira aliyonayo Dr. JPM lazima aungwe mkono na kila anayeitakia mema Tanzania.

Dr.JPM endelea kukaza hivyo hivyo.
 
Hotuba ya JPM ilikuwa nzuri sana na nimeshukuru kwa kuweka vitu invariably black and white bila kuficha unafiki . Alivyowaponda Mimi binafsi ninamuunga mkono na kumwombea afanikishe yote aliyoyaainisha Jana.
Wanaoona hajatenda haki ni wanafiki sana. Mwacheni afanye kazi tuliyomtuma wananchi na si kwenda kuwalinda akina kikwete . Tena natamani aanze kwanza kuyatumbua majipu ya wastaafu wetu wote ili kurudisha imani ya serikali kwa wananchi . Tulikuwa tumeshakata tamaa wananchi na hii serikali yetu . Mwache awashambulie kabisa na wala asiwe mnafiki .
 
Magufuli daima speech zake ni statistical. Hawezi kutoa taarifa bila kuungwa mkono na takwimu. Safari za nje ni kweli zilikuwa nyingi, azima yake ni kuzipunguza ili fedha iliyokuwa ikitumika huko itumike mahala pengine patakapoonesha matokeo chanya. Jambo hili ni zuri labda tatizo ni kulisema. tpaul hataki lisemwe. Kisa lilitendwa na Mgosi. Ukilisema unamuudhi mtu mmoja Mgosi pamoja na wapambe wake akina tpaul, lakini matokeo yake wanafaidika wagonjwa wengi zaidi akiwemo hata yeye tpaul. Sasa tuchague kufurahisha mmoja na kuumiza wengi au tuwaokoe wengi na kuudhi mmoja.Binafsi nachagua kuokoa pesa zitakazokuja kuboresha huduma zetu nyingi zaidi. tpaul atachaguakumfuharahisha Mkwere hatujui in exchange of what, anajua yeye.
Uongozi wetu ni wa kupokezana wenyewe wanaita vijiti. Kwa bahati nzuri au mbaya wanapokezana viongozi toka chama kimoja. Kiongozi aliyekuwa nje alikuwa akiyaona mambo kadhaa aliyoona hayafai na akajiapisha akipata nafasi ile atafanya hili aulile. Sasa anayafanya.Kama kuna watu hawaridhiki ni kawaida tu lakini azima yake lazima aitimize. Asipofanya hivyo itakuwa haina maana. Kama tpaul ina mkera ni sahihi kwa sababu panapotoka mtoto ndipo panapouma. Wacha paume lakini mtoto atoke salama
 
Back
Top Bottom