Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

We ni mpuuzi na kigeugeu.
Watu tumechoka na uozo ulioko serikalini tunataka mabadiliko we unaleta za kuleta.
Ulikuwa ni mmoja wa watu waliomkandia sana JK kwa michemsho yake hapa JF.
Sasa ulitaka JPM asifie?
Alishamsifu kwa mazuri yake mkamtukana..sasa ni wakati wa kurekebisha na kuzoa uozo uliolitrsa taifa we unaleta propaganda.
Watu wa aina yako hawana jema.
 
Last edited by a moderator:
mimi sijakataa suala la usomaji namba...kama ni kuisoma namba kila mtanzania anaisoma...ama uwe UKAWA, CCM au nyumbu! kama ni kufa kwa kukosa huduma bora za kijamii kama vile matibabu bora, nk, kila mtanzania anakufa pasipo kujali kabila, dini, rangi, chama au kitu chochote.

ninachokikataa mie ni kitendo cha magufuli kutafuta CHEAP POPULARITY kwa kuwachafua viongozi waliomtangulia. wewe unadhani kama mkapa asingesimama kidete kumzuia membe, leo hii magufuli angekuwa rais wa nchi hii? halafu anakuja kumdhalilisha mzee mkapa hadharani wakati yeye ndiye aliyemuokotea magufuli embe dodo chini ya mchongoma...hii ni sawa?

kwa staili hii sitashangaa kama magufuli atafufua upya skandali ya ununuzi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira....wewe unadhani akifufua skandali hii atakuwa namtendea haki mzee mkapa aliyemfikisha hapo alipo? think twice mkuu.
Sasa huyo membe mngemuweka urais si nchi ingezidi kufiliaaa mbali kwikwikwi
acha awambie ukweli tu najua truth hearts, na watanzania tunaongoza kwa kuwa wanafiki sana Ktk kila jambo!
Mkwer ameitia hasara nchi kaiongezea made ni kibao na mkwer hata hajali kwake it's normal tu! Maana hana uchungu na nchi hii
Magufuli anajua fika mzgo aliyoachiwa ni mkubwa na kumbuka wakati wa kampeni ametoa ahadi nyingi sana! Lazima kichwa kimuume kuzitekeleza!
 
Magufuli amekosea.Hakukemea safari za Rais.Kakemea safari za idara mbalimbali za serikali.
Kilio cha wananchi kilikuwa safari za rais zilizotafuna shilingi trilioni nne katika miaka kumi.Magufuli hakulizungumzia hili.Amefanya unafiki hapo.
 
Magufuli amekosea.Hakukemea safari za Rais.Kakemea safari za idara mbalimbali za serikali.
Kilio cha wananchi kilikuwa safari za rais zilizotafuna shilingi trilioni nne katika miaka kumi.Magufuli hakulizungumzia hili.Amefanya unafiki hapo.
Ukawa@james mbatia alishaelezea vya kutosha kuwa safari za mkwer na expenses nyingi zilikuwa za anasa tu! Kwani mabidada wengi walijumuishwa ktk safari hizo na vigogo wengine walikuwa wanaenda kula piknik huko ughaibuni
 
Sifa uchwara??? Anza na maneno haya kwa takwimu za safari za mwaka mmoja bilioni 600 zinatosha kujenga lami km 400, sasa endelea vinginevyo madarasa??/ magari washawasha??? Nk. Hapa kazi tu
 
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!

sijui unafki utakusaidia nn.
 
Hakumponda raisi,raisi hyo ni kazi yke kwenda nje na kujenga mahusiano Mazuri na nchi jirani..aliponda baadhi ya safari za Idara za serikali kwenda nje hovyo hovyo..Mimi hapa mwenyewe nashuhudiaga wakurugenzi wa Idara za benki kuu wakienda kutanua Malaysia na Singapore kila baada ya mieZi mitatu

we nae chenga,mamlaka ya idara za serikali kote nchini zinatoka kwa nani.mfano magufuli amepunguza safari za kwenda nje maana yake ni kuwa idara zote zinabidi kutii.shuleni mnasoma ujinga
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.
Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi.




:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Mkuu, Rais Pombe ameshajua nini kinachotakiwa na wananchi wa Tanzania. Alianza kwenye kampeni kwa wimbo wa Chagua CCM/Chagua Magufuli, na utekelezwaji wa ilani ya CCM, akaona hakuna hamasa wala mwitikio, Akabadili Channel akatumia sera za wapinzani na kuiponda Serikali yake ya CCM na udhaifu mkubwa wa kiongozi wake na kwamba yeye atabadilisha hali hiyo, akaona mwitikio wake mkubwa na matumaini kwa wasikilizaji wake na mitandaoni pia, mwanaume akaona mambo si haya bwana! Akakomaa hapo hapo na kuiga kila kitu cha UKAWA na mabadiliko mpaka Nembo yao akitumia akondoa rangi tu na kuweka za magamba, akaitupilia mbali Ilani na hotuba alizoandaliwa akaendelea kuwaeleza watu yale ambyo ndiyo hasa walikuwa wanayategemea kuyasikia toka kwa wagombea, nayo ni mabadiliko; Wapiga kura wakamuelewa na kumchagua.

Sasa katika ufunguzi wa Bunge aliposema kuwa zile ahadi alizokuwa akizitoa za mabadiliko hazikuishia kwenye kampeni tu na ndiyo wakati wake wa kuzitekeleza, asingeweza kubadili maneno yaliyompa ushindi "just" kwa kumpa heshima mtangulizi wake, ingekuwa ni usaliti kwa waliomchagua. Kulikuwa hakuna namna nyingine kwa pale jana zaidi ya kuendeleza pale alipoachia kampeni zilipokoma. Na alichosema ndiyo ukweli mtupu. Kama JK aliona anadhalilishwa kwa hotuba ile angefanya mambo mawili: Angesimama akabisha na kupiga kelele AU angewafuata Ukawa kule nje akawaambie hata yeye ametoka huko ndani hakufai.

kwa sasa akubali tu kuwa ule wakati wa kusikilizwa yeye tu na kupigiwa vigelegele na wale wazee wa Dar es Salaam
hata anapotetea hadharani mambo ya wazi kama Escrow pale Diamond, yamekwisha.
Aliye madarakani ndiye JP Magufuli na si vinginevyo, na ana deni la ahadi alizowapa waTanzania ambazo ili azitekeleze lazima awe na uso wa mbuzi na asijali ka kuna wastaafu wanaokerwa na utekelezaji/utimizwaji wa ahadi hizo.

Mzee Ruksa alishasema kuwa " KILA NABII NA WAKATI WAKE", Kama JK hakumsikia angemuuliza maana walikuwepo pale wote watatu.
BIG UP MY PRESIDENT, YESTERDAY WAS YOUR DAY TO DISTANCE YOUR SELF FROM THE GRIP OF THE RETIRED TRIO.
 
Fikra zingine ni kikwazo kwa mabadiliko ya kweli......unafiki na ujingaujinga wa enzi za jk hatuutaki tena..
 
Msemo wa HAPA KAZI TU... Ungeliksa maana kama asingeweka wazi msimamo wa Serikali yake. Nazipenda zamani hizi, ngoja tuone Mwisho wa yote nani Ataisoma namba.
 
Huyu ni rais anaeweza kutuunganisha watanzania wote nimemuona na namuona shkamii sana kwake
 
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!

Mkuu,
Kwa wastaafu, ambaye atakiwi kuambiwa ukweli n rais tu. Au pia wakuu wa mikoa, mameneja na wangineo ambao amestaafu lakini waliboronga katika utawala wasiambiwe ukweli?!
 
Mimi nitarudi kama hao uliowatag watacomment kwenye hii post
 
Mbona huyu JPM akiwa WAZIRI alikuwa anatetea safari za raisi na kusema zilikuwa na tija ndiyo maana mabarabara yamejengwa? Hapo hakuwa mnafiki? Namuunga mkono kupiga marufuku safari za nje zisizo na tija ila naye akiwa waziri alikuwa anamtetea raisi wake. Iweje leo?

rais hakat tiketi ya ndege,tumia bichwa lako vizuri
 
mnafiki ni nani mkuu? kikwete, mkapa au mwinyi? kwa hiyo wewe unafurahia kuona wazee wetu wastaafu wakidhalilishwa hadharani? you can't be serious mkuu!

Wewe unafurahia kuona mwizi wa kuku anachomwa moto ila mifisadi idunde mtaani mjinga wewe ELIMU ELIMU ELIMU
 
Kaishawaambia yeye siyo mnafiki, ni mpenda haki na msema kweli daima.
Sijui msichoelewa nini
 
Wabongo mmejaa unafiki .alichokifanya magufuli ni safi kabisa.Ni mfano as kuigwa. wananchi tunataka Mabadiliko. Mmetunyima kwa Lowassa sasa mmejipa Magufuli hates anazochukua tunazifurahia msitake kutuchanganya .eti kubishana. Kulindana wapi. Said na wote wanaodhani sasa watakua wanapata matrip yasiokua na kichwa wala miguu wajiandae
 
Kila mtu anahaki ya kusema analoona linafaa mradi tu hakuna sheria inayovunjwa. Mimi nadhani Magufulia alichofanya ni kutoa mwelekeo wa Serikali yake. Tukumbuke pia ushindi wake ni was asilimia chache haijawahi kutokea kwa CCM. Ni lazima afanye au aongee vitu ambavyo vitavuta hisia za wananchi ili aweze kushinda awamu ijayo. Kumbukeni miaka mitano siyo mbali sasa imebaki minne. Sasa kwa kuwa maongezi yake yalilenga zaidi kufurahisha wananchi inaonekana kama alimponda JK, lakini sidhani kama nia ni hiyo. Kama kiongozi ni lazima siku za awali uweke mkwara ili watu wajuwe na wale waliotarajia kuja kukuyumbisha wabadili gia njiani. Suala la matumizi makubwa ya safari za nje well inabidi awe makini nalo maana matumizi makubwa yale kwa mfano ya Wizara ya Mambo ya Nje ni kwa ajili ya Zaira za Viongozi kwa maana ya Rais, VP na PM. Labda haukujua bajeti ya safari za viongozi ipo chini ya Wizara ya Mambo ya nje. Ila ni kweli kuna ziara nyingi hazina maslahi kwa nchi na ni muhimu kuweka mkwara. Kusema kuna rushwa kubwa, bandari wezi sioni kama hiyo ni kumsema JK maana ni suala ambalo lipo wazi.
 
Back
Top Bottom