Habari yenu ndugu zangu watanzania
Kwa macho ya wengi kuanzia mwaka 2015 Tanzania taratibu ilianza kuibomoa misingi ya kidemokrasia na kujenga misingi ya utawala wa kiimla. Dalili za kuwa mtazamo huu ni wa kweli zinajionyesha kupitia
1. Chaguzi zisizo huru wala za haki, rejea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024.
2. Kutoweka kwa wakosoaji wa serikali katika mazingira yasiyoeleweka. Rejea tukio la Humphrey Polepole na wengine.
3. Ukandamizaji wa wanasiasa wa vyama upinzani usio wa haki. Rejea tukio la kuzuiwa kushiriki uchaguzi mkuu la Mh Luhaga Mpina.
4. Bunge ambalo limejaza wabunge wa chama kimoja (Kwenye mfumo wa vyama vingi jambo hili ni gumu kutokea) ambao hata si halali kwa maana hawakuchaguliwa
Swali la kujiuliza ni kwanini serikali yetu imeamua kutufikisha hapa. Nitazigawa sababu za viongozi wa serikali kwenye makundi mawili zenye nia njema na zenye nia mbaya
Tuanza na zenye nia njema
1. Wapo wanaoamini vuguvugu la upinzani kupitia mikutano ya hadhara, mahojiano na waandishi wa habari, michango ya wabunge wa upinzani bungeni na maandamano ya kisiasa likipewa kibali litachangia kuidhoofisha serikali isiweze kutekeleza agenda zake, kuleta mivutano ya kisiasa isiyo na tija na kupelekea nchi isitawalike. (Rejea sababu za katazo la mikutano ya hadhara ya wapinzani katika serikali ya awamu ya tano)
Udhaifu wa hoja hii: Kwanza shughuli za upinzani zilipewa kibali lengo likiwa kuiwajibisha serikali kuhakikisha inatekeleza majukumu yake vizuri na inawasikiliza wananchi (rejea madhara ya shughuli za wapinzani kwenye serikali ya awamu ya nne). Sasa wanaounga mkono hoja hii watasema lakini hilo sii lengo la wapinzani katika Tanzania. Jibu langu litakuwa ni hili kama ni hivo suluhu sio kuweka makatazo haramu bali kuwaelimisha wananachi na kuwaamini watafanya machaguo sahihi pindi kipindi cha uchaguzi mkuu huru na wa haki utakapowadia.
2. Wapo wanaosema kuwa vyama vya upinzani nchini vinatumika na mabeberu kwa ajili ya maslahi ya mabeberu.
Udhaifu wa hoja hii: Kwanza sidhani kama kuna ushahidi wa maana ushawahi kutolewa pili kwa mara nyingine suluhu si kuvunja sheria na kuweka makatazo haramu bali ni kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa uhuru wa nchi, kutoa ushahidi wa mashtaka hayo ya kutumika na kuwaamini wananchi kuwa watafanya uchaguzi sahihi pindi kipindi cha uchaguzi mkuu huru na wa haki kitakapowadia.
3. Wapo wanaoasema kuwa demokrasia si matusi. Wanasema haiwezekani vijana wakawa wanawatukana viongozi kwenye mitandao ya kijamii na waachiwe kisha useme ni demokrasia.
Udhaifu wa hoja hii ni tafsiri ya neno tusi, mtu anaweza kuikosoa serikali kawaida tu na akaambiwa kwamba amewatukana viongozi. Pili huwezi kuharibu mfumo mzima wa kidemokrasia na kupuuza faida zake nyingi kwasababu ya kutukanwa na kijana mmoja mhuni mtandaoni. Sasa kama matusi ni tatizo suluhu ni kutunga sheria inayohusu kipengele hicho cha matusi na kupitia viongozi wa dini na taasisi za elimu kufundisha vijana maadili katika kuwasilisha hoja.
4. Wapo wanaohisi kuwa demokrasia pengine inaweza kuleta ushoga (ambayo ni dhambi kuu pengine kupita zote mbele ya mwenyezi Mungu rejea Mwanzo 18:20)
Udhaifu wa hoja hii: Demokrasia na Ushoga ni mada mbili ambazo hazina hata muingiliano unapozungumzia demokrasia unazungumzia mambo ya serikali na namna ya kuongoza watu akati unapozungumzia ushoga unazungumzia mambo ya mavimavi na wendawazimu. Kwa hiyo kuviunganisha hivo vitu siyo Sawa. Taifa zuri na tukufu kama Tanzania lenye wanaume rijali na wanawake warembo mno linaweza likaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia na bado likawa na sheria za kupinga ushoga. Pili demokrasia maana ake ni matakwa ya wananchi yafuatwe basi kwasababu wananchi wa Tanzania milioni 70 wazee, vijana na watoto, wanaume na wanawake wameupinga ushoga kwa kauli moja basi mfumo wa kidemokrasia ndio mfumo utakaohakikisha kuwa ushoga hautakuwepo hata Masihi atakaporudi. Kwa maana utamuaminije dikteta, vipi akihongwa na mabeberu(Kwa maana leo hii dikteta ambaye ni adui wa mabeberu kesho ni rafiki yao) kuleta ushoga na sisi wananchi tumekataa. Basi mfumo wa kidemokrasia utaweka hatma ya taifa letu mikononi mwetu sisi wananchi si mikononi mwa dikteta.
Zipo hoja nyingine za wenye nia njema lakini niishie hapo
Hoja za wenye nia ovu
1. Wapinzani wanapenda kupinga pinga ufisadi tukiwaachia tutapoteza kula yetu. Ni muhimu tuwadhibiti ili tuweze kufanya tunachotaka bila bugudha. Tufanye bidii tuhakikishe kuwa vyama hivi vya upinzani vinakufa kishapo tukidhibiti chama tawala na tuyale mema ya nchi kwa amani sisi na watoto wetu. HA HA HA HA HA (Cheko la kiovu)
2. Tungependea Koo zetu watoto wetu watawale serikali lakini je tukiruhusu siasa za ushindani watatoboa maana itawahitaji wawe makini kweli kweli kuweza kukubalika na wananchi na tunawajua watoto wetu walivyo. Hapana vijana njoeni hakikisheni mnamkamata yule anayeongea sana hakikisheni amepotea. Vijana wanajibu Sawa mkuu. AAAAAAAAHHH!! yalisikika makelele kwenye nyumba ya mwanaharakati.
Sasa baada ya kuzichunguza fikra za wapinga demokrasia. Sasa tuangalie manufaa ya demokrasia
1. Viongozi wanawajibika kwa wananchi.
Maelezo. Katika mfumo wa kidemokrasia ili uwe kiongozi ni lazima uchaguliwe na wananchi kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki. Kwahiyo kama huna hoja za msingi kwa wananchi hawatakuchagua. Na pia kama walikuchagua na wewe huku wafanyia kazi yoyote basi hawatakuchagua tena. Maana ake ni kwamba kiongozi katika mfumo wa kidemokrasia lazima uwe unaguswa na changamoto za wananchi, lazima uwe na uwezo na bidii ya kuzitatua ili uendelee kudumu katika siasa. Hiyo inawafanya viongozi wawe wanawajibika kwa wananchi. Hii itachangia kupata viongozi bora na kuleta maendeleo ya kweli.
2. Madaraka yanarudi mikononi mwa wananchi
Maelezo: Katika mfumo wa kidikteta yule dikteta pale juu ndio kila kitu. Wengine wote kazi yao ni kumtii, kumuogopa na kumsifia. Yeyote atakayempinga basi ataonewa pengine (mwenyezi Mungu atuokoe) atauliwa. Lakini katika nchi ya kidemokrasia mtukufu rais kipenzi cha watanzania, chaguo la wananchi, jemedari wetu namba moja kwenye vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi yuko chini ya sheria hawezi fanya vitu kinyume cha sheria, mbali na hilo anawajibika kwa wananchi, alipozunguka nchi nzima wakati wa kampeni alitoa ahadi njema kwa wananchi na ni hizo anazozitekeleza maana yuko chini ya wananchi, yeye ni mtumishi tu wa watu, akifanya jambo lolote ambalo si sahihi wananchi wanamtoa madarakani bila huruma wakitumia vichinjio(kadi za mpiga kura) vyao.
Basi ndugu zangu watanzania tumchague kiongozi atakaeirejesha nchi kwenye misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria.
#KATIBAMPYASASA
Viva Dr. Emmanuel Nchimbi
Viva Tundu Lissu
Viva John Heche
PIIIIIIIIIIPOOOOOOOZ ..............................