Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
UPDATE:
Wana Jamii Forums. Kwanza tunanaombeni radhi kwa kuwaangusheni. Mpango mzima ulisukwa Tanzania. Wafadhili wetu wapo Tanzania na wachache nchini marekani. Hatuhusiani na CHADEMA kama wengine wanavyofikiria. Sisi ni Wana CCM waliochishwa na ufisadi wa Kikwete. Sisi ni Wana UVCCM ila waandamanaji ni watanzania ambao hawakuonysha itikadi zao za kisiasa. Ukweli ni kwamba, tumekuwa tukifuatiliwa kwa muda na watu wasiofahamika. Tulikuwa na makundi matatu, sasa jana baada ya Kufika Washington DC kutoka majimbo tofauti tofauti, tulikaa hoteli tatu tofauti. Punde wakatokea watu waliojifanya ni wenzetu wakisema kwamba, wamepata taarifa kwamba Mh. Rais angekuja siku ya Jumamosi.
Cha ajabu ni kwamba, viongozi wote wa msafara walipewa hela nyingi sana ambazo chanzo chake hazieleweki. Kati ya watu 106 waliofika na mabasi, kila mmoja alipokea siyo chini ya $25,000. Viongozi inasemekana walipewa hela nyingi sana. Haikuchukua muda mrefu tukawa tunaambiwa na viongozi wenzetu kwamba tutapelekwa sehemu tofauti tofauti kula chakula cha jioni. Kumbe muda huo ndio JK alikuwa anafika ukumbuni. Nilipopigiwa simu kutoka ukumbuni kwamba JK kafika, kuwakusanya kila mshiriki ikawa ni shida. Usiku tulipokutana ndo ukweli unafahamika. Kila mshiriki akaanza kushangaa ni kwa nini waligawiwa hela? Hakuna aliyetambua kwamba hawa walikuwa ni watu wa kikwete
Waliogawa hela muda huo walishatokomea. Hawa ni Watanzania wenzetu. Wadada wawili na Wanaume watatu ambao walijitambulisha kwamba wamepewa hela na mfadhili na mmoja wa wafadhili wetu ili kujikimu tukiwa Washington DC. Kwa hiyo hivi ndo mambo yalivyokuwa Jana. Wala msihofu, mapambano bado yanaendelea. Vita vinarudi Tanzania. Kikwete awaelezee watanzania kwamba hizo dola millioni tatu walizowanga wenzetu kiujanja zimetoka wapi?
Kama ni wongo babu kubwa ndio huu, na hata maelezo yote ni kujikanganya tu, ni dhahiri mhuni fulani alileta hii mada hapa na sasa anajitahidi kujisafisha. Yako wapi aliyosema hapo awali anataka kumfungulia mashtaka mwanasiasa fulani nchini marekani?
Pesa za kutoka wapi za kuwagawia mamia ya waandamaji kuwanyamazisha kila mmoja kupata $25,000, kiasi ambacho ni sawa na pesa ya Tanzania Sh. 40.000,000? Sisi si watoto wadogo. Hii si kweli kabisa, ni uwongo mtupu. Uliwezaje kuingia kwenye mkutano wenu na mara ukageuka kuwa mkutano wa kukutana na Kikwete? Kwa nini hamkuondoka ndani ya ukumbi kama mlikuwa na malengo mengine?
Mode jaribu kuhakiki habari za watu wanaoingiza kwenye JF ambazo zinawapotezea watu muda wa kujadili badala ya kujadili mambo mengine ya muhimu zaidi.