Maandamano ya Kumpinga JK Washington DC

Maandamano ya Kumpinga JK Washington DC

Status
Not open for further replies.
Hapo kwenye blue umenichanganya kidogo. Huyu Mwingereza ni mpinzani au ni UVCCM? Nafikiri kwenye maelezo yake amejitambulisha kama UVCCM so does it make UVCCM wahuni pia?

anajitambulisha kama uvccm baada ya mpango kukwama...mbona mwanzo hawakusema ni wanaccm dhidi ya mwenyekiti wao,si ndio maana wengi tukaingia kichwa kichwa
 
update:
wakuu. Kunradhi kwa ukimya. Punde tutawamwagienie kilichojiri dicota. Siyo kila msafiri ni mmoja wenu; wengine ni mamba na siyo kenge. Mkae tayari kuhoji hizi dola millioni 3 zimetoka wapi. Hatunyamazi hadi kieleweke. Upuuzi wa kikwete umezidi, kuja kuhonga watu millioni tatu ni aibu kwa tanzania. Tunatayarisha ripoti ambao tutawaashuhia muda siyo mrefu

Kwanza mngetayarisha ripoti ya jinsi viongozi wenu walivyoshiriki kuhujumu hayo maandamano..msitupotezee muda kwanza wengi wenu huko hamna makaratasi ndio maana mmeshindwa kirahisi,hebu tuacheni tuendelee na kampeni zetu IGUNGA.
 
Wakuu katika hali isiyo ya kawaida, kuna vijana ambao walikuwa wanaishi ghetto hapa Washington DC, leo hii wamekuwa ma-millionea. Jamaa wanaendesha Lexus GS-350.

Kuna tetesi kwamba kuna hela zimemwagwa kwa wingi na watanzania fulani. Nahisi hili n kundi la mwingereza waliokuwa dau nene na kumuachia mzee wa kaya kufanya mambo yake Dicota. Mie nilikuwepo ukumbuni, hali ilikuwa siyo ya kawaida.

Hatukuwa na taarifa ya kuja kwa JK. Ghafla tukaambiwa tukae upande mmoja, pasipo mategemeo akafika JK na milango yote kufungwa..Ila kuna uvumi kwamba kuna helza zimemwaga kwa vijana ambao walikuwa hawana kazi.. yaani ni hela nyingi.

Tutazidi kuwataarifuni mara data zikiendelea kumwagika, kwa maana siyo siri tena kwamba jamaa wamehongwa Dola millioni tatu..

Habari ndo hiyo.....

Nakufananisha na mtoto si riziki
 
nyinyi mngelikuwa mnataka kuandamana kweli wala ilikuwa haina haja ya kwenda huko ukumbini, mngeingia barabarani tu na ujumbe ungekuwa umemfikia, maandamano gani mpaka ukumbini, halafu hela zote hizo haingii akilini.
 
Moderators tafadhali chukueni hatua, mwingereza and his group has made us fools including you mods, please close this topic and ban mwingereza for good.
 
Unajua unachoonge inabaki ni maneno tu na unaendelea kudhalaulika tu. Ni kweli kuna funds zilimwagwa na si kitu cha ajabu kwani nakumbuka niliudhulia dicota ilipofunguliwa houston na ni kweli hawa dicota huwa wanapewa funds na serikali thats a fact.

Hii ya DC inayoendelea si kitu cha kushangaza na kuna jamaa wengi ninawafahamu personally nimezungumza nao walisema campaign ya kupeleka watu DC ilianza kama miezi miwili na wao walipewa maagizo na ubalozi kupiga debe sehemu zenye watanzania (states mbalimbali) kuwaahidi mpaka tickets ili waweze kufika. Kuna baadhi ya watanzania wasio na mwelekeo na ni rahisi sana kuwashawishi kupanda ndege na kuwaweka hotelini kwa kula bure na kukaa bure na kunywa pombe za bure ... this's not a shock ni tabia ya wale wasiojali kuwa hata kama hizo funds mnapewa i.e. tickets, food, alcohol huwezi kufikiria zingetumiaka kuwahudumia watanzania wenzako katika hii hali ya sasa? Anyway it's typical na wakimaliza kunywa watatuma pesa nyumbani kuwasadia wazazi wao....

The embarrassment ya hii dicota na hii mikutano yao ni kwamba wapo tayari kuchukua funds za wananchi kukaa na kusikiliza serikali ya ccm ikitoa ahadi na speeches za udanganyifu kila mwaka at the same time wakijua hakuna chochote kinafanyika au matokeo ni yaleyale ya uongo mtupu. Hiki sio kitu cha mzaha cha kucheza na maisha ya watanzania, nilipohudhuria hii dicota Houston waliokodi hotel kama hiyo hiyo Marriott na hakuna information yeyote ile ya jinsi gani wanapata funds ku-run hii mikutano na zaidi cost wanalipaje ... maybe they (dicota) si wange-confirm tunapewa na ofisi ya ubalozi DC. Shame kubwa ni kwamba wapo watanzania wanadanganyika there's something important they are gaining for attending these social events in expense of maisha ya wananchi.

This is third meeting and we will see hizo speeches na failed policies zitasaidia vipi wananchi Tanzania. Wanaoishi Marekani wataendelea kulalamika na kuumia kwa kutoa misaada ya fedha kila mwezi kwa ndugu zao mpaka wajue na kupata majibu nani anasababisha au ni policies gani zinawaumiza ndugu zao na kupata huduma mbaya .... shame nobody in the room don't think of their families.... We will not surrender to fight for our rights!

Wakati kikwete, membe na balozi wao DC wanaona this is success story kuweza kupata venue ya kuongea na kuacha wajinga watafakari ....
 
Hii thread ilitakiwa iwe imeshapotea toka Jamaa aliposema wanataka kuongwa dola 3m ili kuuwa maandamano.UWT na Kikwete wanajua tabia za Watanzania,watoe dola 3m kwa kipi haswa?
 
Mimi naona walio andaa ile FACEBOOK AGAINST VODACOM wameonyesha wako effective kuliko hawa wanaompinga JK

Kwanza hawaeleweki

Pili haiulikani wanataka nini

Tatu inaonekana ni wazugaji tuu

Nnne hawana tofauti na Invisible kutulea story za alinacha eti Shimbo kakutwa na Trilioni 3 bila kuleta ushahidi

Lakini pamoja na hayo thread ibaki tuu hapa hakuna kunyamazisha watu kwa sababu hamkubaliani nao. Watu wajadili mpaka mwisho tukijua ukweli kisha tutamove on kwenye mengine
 
Swala Muhimu ni Promises za Kikwete, Membe na dicota yenyewe

Tusisahau kuna report za mafanikio makubwa ya mikutano ya dicota inakuja. Subirini viongozi wa dicota wanatarajia kutoa report ya jinsi gani na mafanikio gani yatawasaidia watanzania walio nje ya nchi ili maisha yao yatakuwa nafuu na zaidi hawatahitaji kutuma fedha tena au hakuna tabu tena ya kupanda hati za viwanja na kufungua biashara Tanzania , zaidi kuna investments zinakuja toka US kutokana na kazi ya dicota... I love these ccm meetings!

Let's stop focusing on who's was protesting or who's failed to show up, the main issue remained is relation between kikwete gov and dicota. Who's dicota and what's its purposes in US?


 
Sasa hii inahusina na nini kuhusu hii thread? Kweli nchi yetu inavichwa maji kweli kweli ... zaidi huu utumbo wako nyote mnaonekana ni mashetani matupu, unajua shetani akikuingia huwezi kujua yupo mwilini mwako?

 
Last edited by a moderator:
kikwete,tambua kuwa watu wanapinga na wamechoshwa na ufisadi uliopo ndani ya CCM, hivyo wana-CCM mkiendelea na upuuzi huu na ufisadi wenu huu mtaishia pabaya, wana-CCM tambueni kuwa ^MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI- tutaonana 2015.
 
MODS ifungeni hii thread inashusha JAMVI hii ni SCAM

MODS, hii thread ibaki hapa hapa kwa kumbukumbu na rejea. inatupa picha nzuri ya harakati za malimbukeni na ni aibu kwa CDM. Jamvi halihusiki na aibu hii. Thread iachwe ili watafiti waone kudanganyana na mwelekeo wa vyama uchwara, nadhani itawasaidia kufanikisha utafiti wao.
 
UPDATE:
Wana Jamii Forums. Kwanza tunanaombeni radhi kwa kuwaangusheni. Mpango mzima ulisukwa Tanzania. Wafadhili wetu wapo Tanzania na wachache nchini marekani. Hatuhusiani na CHADEMA kama wengine wanavyofikiria. Sisi ni Wana CCM waliochishwa na ufisadi wa Kikwete. Sisi ni Wana UVCCM ila waandamanaji ni watanzania ambao hawakuonysha itikadi zao za kisiasa. Ukweli ni kwamba, tumekuwa tukifuatiliwa kwa muda na watu wasiofahamika. Tulikuwa na makundi matatu, sasa jana baada ya Kufika Washington DC kutoka majimbo tofauti tofauti, tulikaa hoteli tatu tofauti. Punde wakatokea watu waliojifanya ni wenzetu wakisema kwamba, wamepata taarifa kwamba Mh. Rais angekuja siku ya Jumamosi.

Cha ajabu ni kwamba, viongozi wote wa msafara walipewa hela nyingi sana ambazo chanzo chake hazieleweki. Kati ya watu 106 waliofika na mabasi, kila mmoja alipokea siyo chini ya $25,000. Viongozi inasemekana walipewa hela nyingi sana. Haikuchukua muda mrefu tukawa tunaambiwa na viongozi wenzetu kwamba tutapelekwa sehemu tofauti tofauti kula chakula cha jioni. Kumbe muda huo ndio JK alikuwa anafika ukumbuni. Nilipopigiwa simu kutoka ukumbuni kwamba JK kafika, kuwakusanya kila mshiriki ikawa ni shida. Usiku tulipokutana ndo ukweli unafahamika. Kila mshiriki akaanza kushangaa ni kwa nini waligawiwa hela? Hakuna aliyetambua kwamba hawa walikuwa ni watu wa kikwete

Waliogawa hela muda huo walishatokomea. Hawa ni Watanzania wenzetu. Wadada wawili na Wanaume watatu ambao walijitambulisha kwamba wamepewa hela na mfadhili na mmoja wa wafadhili wetu ili kujikimu tukiwa Washington DC. Kwa hiyo hivi ndo mambo yalivyokuwa Jana. Wala msihofu, mapambano bado yanaendelea. Vita vinarudi Tanzania. Kikwete awaelezee watanzania kwamba hizo dola millioni tatu walizowanga wenzetu kiujanja zimetoka wapi?


FACEBOOK PROTEST AGAINST KIKWETE
TUNAOMBA MJIUNGE NA TUSAMBAZE HABARI KWA TANZANIA WOTE
**************************************************************************************


Tunapanga maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubasli kushiriki.Hii kumshinikiza kushugulikia swala la ufisadi na matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. Maandamano yetu yataishia STATE DEPARTMENT. Naye apate Aibu, kwa kucheza na maisha ya watu, na kuiaca familia yake ikoroge nchi yetu. Ridhiwani anamilika robo ya uchumi wa Tanzania? Kwani Tanzania ni Tunisia....Ukitaka kushiriki tuma barua pepe kwenda eliakimmallya@yahoo.com

Tayari watu 974 wamesha confirm kujumuika katika maandamano haya ya amani....Jamani tuendeleeni, kushirikiana tumuaibishe huyu msanii , mtalii Vasco Dagama a.k.a Dr. Livingstone hadi atoke madarakani. Kadhalika tumeni barua pepe pamoja na malalamiko kwa wingi kwenda wiegertjr@state.gov ili kupinga Vasco Dagama kupewa VISA na wapambe wake. Ifahamike kwamba mimi siyo mwana CHADEMA wengine wanavyodai. Mimi ni mwana UVCCM tena ngazi ya Juu, lakini Kikwete hakufaa kuwa Rais, ndo maana Watanzania wanaumia. Mapinduzi yanakuja. Wasio na makaratasi, tunachoomba ni sala zenu tu. Watu wanaongezeka sana. Tayari tumefikisha watu 512 ambao wapo marekani ki halali na wako tayari kujiunga nasi kwa ajili ya haya mapinduzi

SERIKALI YA TANZANIA KUPITIA WATU WASIOFAHAMIKA, WAMEANZA KUTUTOLEA VITISHO PAMOJA KUJARIBU KUTUHONGA WAANDAAJI $3MILLION KUZIMA ZOEZI ZIMA LA MAANDAMANO. JIBU LETU NI KWAMBA, HATUWEZI KUUZA HUTU WETU NA UBINADAMU WETU. HIZO HELA WAPELEKE KWENYE MAHOSPITALI SIYO KUTUHONGA SISI. WAKAWAONGE WATANZANIA MILLIONI 40 WANAOKUFA NA NJAA SIYO SISI. MAANDAMANO LAZIMA, NA RAIS KIKWETE AJITAYARISHE. TUNAKUTANA NAYE MARRIOT WASHINGTON DULLES AIPORT NA HOTELINI KWAKE. TUMESHAJITAYARISHA

View attachment 37743


Ungepewa $25,000 ungeleta hoja hiii ? i think umeleta hii hoja ya maandamano kwa sababu ulikosa fupa,kwani haya yalianza leo,mbona hatukusikia yaliojiri hapo nyuma ? Naomba jibu mkuu samahani.
 
Sasa hii inahusina na nini kuhusu hii thread? Kweli nchi yetu inavichwa maji kweli kweli ... zaidi huu utumbo wako nyote mnaonekana ni mashetani matupu, unajua shetani akikuingia huwezi kujua yupo mwilini mwako?


mie naona tunayeyushana tuu sasa kama mnatuyeyusha na sisi pia tunawayeyusha

Thread inayojadili hili suala ipo lakini maswahiba zenu wanapitisha tuu hizi threads zenu zinazolingana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom