Sasa Mkuu wangu kama Rais ambaye ndio Mwenyekiti wa CCM haeleweki, na inaonyesha mafisadi wamemshika pabaya ama wamezidi nguvu, hivi kweli hapo kuna matarajio kwamba hiyo vita mtashinda from within?
Mzee Malecela hakuwepo kwenye kikao, na sijui kama Mama Kilango alikuwepo. Sasa kama hao ambao wanaongoza vita vya ufisadi wanashindwa kuhudhuria vikao kama hivyo ambavyo ni muhimu sana katika mapambano, huoni kwamba na wao wanaonekana kama wamekata tamaa? Walitakiwa wahudhurie hicho kikao ili wapambane na mafisadi kwa hoja na kuwaambia usoni kwamba fulani ni fisadi alifanya hiki na kile na kwamba kwa chama kuendelea kuwakumbatia wanakichafua chama na kukiweka kwenye hali ngumu kwenye uchaguzi ujao.
Mzee Malecela aliposema uchaguzi wa 2010 utakuwa mgumu alikuwa anatumia hali halisi aliyopambana nayo Busanda wakati wa Uchaguzi mdogo, kila kona mnazowema mafisadi. Bila kuiba kura 2010 hakitakuja kueleweka.
Mafisadi wote walikuwa Dodoma na walishapangana kuanzia kamati ya Maadili, CC mpaka kwenye NEC.
Kamanda FMES tuseme ukweli, hivi kweli hoja ya ufisadi ikiletwa kwenye kikao cha kamati ya maadili, Chenge atachangia kitu? Hao wengine nao usafi wako una mashaka. Ukienda kwenye CC same story, wajumbe wengi wa CC wana tuhuma za ufisadi, sasa ikiletwa hoja ya ufisadi unategemea wataipigia debe kwamba chama kisafishwe wakati wanajua wazi kwamba usafi ukianza na wao wenyewe watatakiwa kuondolewa. Kwa hiyo kupendekeza kwamba watu wenye tuhuma waondoke CCM ni sawa na kusema vunja secretariat yote ya CCM, Vunja kamati ya Maadili, vunja CC na vunja NEC, yaani watu waanze moja.
Ndiyo maana ninasema kwamba CCM kama chama kimechafuka, unaweza ku-single out very few members kwamba ni wasafi lakini majority ni wachafu na hao wachafu ndo wameshikilia nafasi muhimu kwenye secretariat ya chama, kamati ya maadili, CC na NEC.
Kwa mwendo huu hatuwezi kufika na CCM kuwa safi ni ndoto ya mchana. Dawa pekee ni kama Mwawado alivyosema ni kuwaondoa kwa kutumia sanduku la kura, japo ni ngumu sana kwa kuwa Tume ya Uchaguzi ni ya kwao, Jeshi la Polisi ni la kwao, TAKUKURU ni ya kwao na Usalama wa Taifa unalinda maslahi ya mafisadi. Bado tuna safari ndefu kufikia uhuru kamili na Zuma ninamuona anakuja kwa kasi kubwa sana.