Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Sina la kuongeza zaidi ya kuona sisi M wanakufa na kuibuka na chama kipya chenye matumaini mema kwa watanzania bila kujali ni chama gani.
Sijali huu usanii wa vikao viiiingi vya kujifungia maana hii ni jadi yao na hapo ndipo walipotuletea msanii JK tokana na vikao sampuli hii hii.
 
the vicious circle, the NEC results are out!!!!!!!

Sidhani kama kuna mtu ana shida ya hizo results, watu wanataka kujua kilichojadiliwa huko ndani ili waweze kuona kuna mwelekeo wowote huko mbele ya safari.

Wakikubali kuwatosa mafisadi basi tunaweza kusema labda watajisafisha na hivyo watakuwa wamefungua mlango mpya wa kashfa kubwa kubwa ambazo labda hatujawahi kuzisikia.

Lakini wakisema wabebane msobe msobe hivyo hivyo kama walivyombeba Makamba basi tujue tumeisha maana kitakachotokea mbele ya safari ni mafisadi kukusanya nguvu ili kuwaengua wale wote wanaopiga kelele za kupinga ufisadi.

Kimsingi CCM kama chama kujisafisha mbele ya wananchi ni kazi ngumu sana kwa kuwa na chenyewe kimeshiriki kwenye ufisadi na mafisadi wana data zote, kwa hiyo wenye tuhuma za ufisadi kama akina EL na RA wakitupwa nje, utashangaa tunaanza kupewa ufisadi wa CCM kuanzia ndani mpaka nje na hakuna atakayebaki salama. Ni wachache sana, kama wapo, ambao ni CLEAN kiasi kwamba wanaweza kusema wao as individuals wako safi. Ila kama walikuwa kwenye NEC na CC, ilikuwaje wakaruhusu CCM ihusike kwenye ufisadi?

Yetu macho na masikio kutoka Dodoma.
 
Sitta chupuchupu CCM
• Yaaminika ushauri wa Kikwete umemuokoa

na Mwandishi Wetu, Dodoma (Tanzania Daima)

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, jana jioni alilazimika kuwaomba radhi wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kunusurika na hatari ya wazi ya kupoteza uanachama iliyoanza kujionyesha tangu juzi jioni.
Hatua hiyo ya Sitta kuomba radhi ilikuja baada ya wajumbe takriban wote wa vikao viwili vya juu vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) vya chama hicho kujenga hoja za kumshambulia wakipinga namna anavyoliendesha Bunge katika mwelekeo wa kukidhalilisha chama hicho na serikali yake.
Habari za uhakika kutoka ndani ya vikao hivyo vilivyokuwa vikifanyika katika Ukumbi wa Mlimani mjini hapa tangu juzi, zinaeleza kwamba, takriban wajumbe wote waliokuwa wakisimama kuzungumza katika vikao hivyo walikuwa wakitaka kuona Sitta akipokonywa uanachama wa chama hicho, ili liwe fundisho kwake binafsi na wana CCM wengine.
Taarifa kwamba Sitta angeomba radhi zilianza kusikika tangu jana asubuhi baada ya wajumbe kadhaa wa vikao hivyo kuieleza Tanzania Daima kwamba spika huyo alifanya kikao na Rais Kikwete kabla ya NEC kuanza.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha siri kati ya rais na Sitta zinaeleza kwamba, mwenyekiti huyo wa CCM alimtaka kiongozi huyo kutafakari kwa makini tuhuma zote zilizokuwa zikielekezwa kwake na kutoa utetezi ambao utamuepusha katika hatari ya kupokonywa kadi ya uanachama na hatimaye uspika wake.
"Kuna taarifa kwamba Rais Kikwete alipokutana na Sitta leo asubuhi (Jumatatu), alimuomba kiongozi huyo atumie busara kulimaliza suala hilo ambalo hatima yake ingeweza kuwa mbaya," alisema mjumbe mmoja.
Tukio hilo baya kabisa kuwahi kumfika Sitta ambaye amekuwa akijinadi kuwa ni spika wa kasi na viwango, lilihitimishwa na uamuzi wa NEC kuunda kamati maalumu kuchunguza kiini cha kufikia hapo.
Habari kutoka ndani ya vikao hivyo vya CCM, zinaeleza kuwa, kamati hiyo maalumu itaongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wake wengine watakuwa ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa habari hizo, mwelekeo wa wana CCM hao kutaka kumwadhibu Sitta ambaye katika siku za hivi karibuni amejizolea umaarufu wa kisiasa ndani na nje ya Bunge, hata kuwa na uwezo wa kumnyoshea kidole mtu au taasisi yoyote, ulianza kujitokeza tangu katika Kamati Kuu juzi.
Hali hiyo ya mambo, ilimlazimu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwaomba wajumbe wa CC, wamruhusu kuipeleka ajenda hiyo ya Sitta katika kikao cha NEC kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa uamuzi.
Mjadala huo ulipoanza ndani ya NEC, wajumbe takriban wote waliokuwa wakizungumza walionekana kumshutumu Sitta wakihoji namna anavyoliendesha Bunge katika misingi isiyozingatia taratibu na kanuni za mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.
"Jana na leo ni siku mbaya na ngumu kwa Sitta, kwani kati ya wajumbe zaidi ya 40 waliozungumza, ametetewa na wajumbe watatu tu, ambao wote waliposimama kuzungumza walikuwa wakizomewa hata kusababisha mwenyekiti kuingilia kati na kutaka hali ya utulivu," alisema mmoja wa wajumbe ambaye alionekana dhahiri akiwa upande uliokuwa ukimshambulia spika huyo.
Habari zaidi zinasema, mjumbe mmoja alisimama na kumshutumu Sitta kuwa ndiye chimbuko la kuongezeka kwa ufa wa makundi ndani ya chama hicho, kutokana na tabia yake ya kuliendesha Bunge akiwa ameambatana na kundi moja la wabunge wanaomuunga mkono.
Mjumbe huyo (jina tunalo), alifikia hatua ya kusema Sitta ameanzisha kikosi cha wabunge wake (aliowaita first 11) ambao siku zote amekuwa akiwapanga kuzungumza wakiwalenga watu fulani na wakati mwingine kuirarua serikali bungeni kwa sababu tu ya kutimiza malengo yao binafsi.
Mbali ya huyo, mjumbe mwingine kati ya wajumbe zaidi ya 50 waliozungumza tangu juzi, alifikia hatua ya kufananisha mashambulizi hayo na kitendo cha wawindaji kumjeruhi nyati na kumwacha pasipo kumuua kabisa, akisema ni cha hatari kwa maisha ya wawindaji.
Wajumbe wa NEC waliozungumza na Tanzania Daima wanasema, mjumbe huyo alifikia kutoa matamshi hayo, lengo likiwa ni kukitaka kikao hicho cha NEC kuhitimisha mjadala mzima wa juzi na jana kwa kumpokonya kadi ya uanachama kiongozi huyo.
Habari zaidi zinaeleza kuwa, mjumbe mwingine aliyekuwa akiunga mkono hoja hiyo alifikia hatua ya kusema, CCM haiwezi kutikisika iwapo Sitta atapokonywa uanachama, akisema katika wakati tofauti chama hicho kimepata kupoteza makada maarufu katika siku zilizopita.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, makada wengine wa chama hicho aliokuwa akiwazungumzia walikuwa ni aliyekuwa Makamu wa Rais, Aboud Jumbe, ambaye mwaka 1984 alivuliwa wadhifa wake na NEC, baada ya kuvuja kwa taarifa zilizokuwa zikimhusisha na mipango ya kuudhofisha muungano.
Mwingine aliyetajwa katika kundi hilo ni Maalim Seif Sharif Hamad na wana CCM wengine 16 wa Zanzibar ambao walivuliwa uanachama mwaka 1988, wakituhumiwa kukihujumu chama hicho na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kada wa tatu wa chama hicho aliyelazimika kukihama chama hicho akiwa na umaarufu aliyetajwa na mjumbe huyo kuwa mfano wa watu walioondoka CCM na kukiacha kikiendelea kuwa imara, ni Augustine Mrema, ambaye aliondoka mwaka 1995 kutokana na kuhitilafiana na serikali na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Cleopa Msuya, akamshauri rais amfukuze kazi.
Wakati mjumbe huyo akitoa matamshi hayo, mjumbe mwingine aliitaka NEC kutohofia uamuzi wa kumvua Sitta uanachama, akitaka wajumbe wajifunze kutoka nchini Afrika Kusini ambako chama tawala kilifikia hatua ya kumvua madaraka rais wa nchi (Thabo Mbeki) na bado kikajihakikishia ushindi uchaguzi mkuu ulipoitishwa tena.
Mjumbe mwingine wa CC na NEC aliyezungumza na Tanzania Daima jana alisema, mwelekeo wa vikao hivyo, zilikuwa ni salamu tosha kwa Sitta na makamanda wenzake wa ufisadi wakati huu chama hicho kinavyojiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani.
"Huyu jamaa (Sitta) na wapambe wake wamekuwa wakikivuruga chama na serikali ndani na nje ya Bunge kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kwa kisingizio cha ufisadi. Leo hii wamejionea wenyewe namna damu ya watu waliowaonea kama Edward Lowassa na wenzake inavyowalilia," alisema mjumbe huyo aliye karibu kimtazamo na waziri mkuu huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana baada ya jina lake kuhusishwa katika sakata la Richmond.
Wakati mjumbe huyo akitoa maoni hayo, mwingine aliyezungumza na gazeti hili alisema, mtiririko mzima wa hoja ndani ya vikao hivyo, unaonyesha namna kundi moja la watu wenye fedha lilivyojipanga kuhakikisha linammaliza Sitta kwa kutumia kila mbinu.
Hata hivyo, habari zaidi kutoka ndani ya vikao hivyo zinaeleza kwamba, kikubwa kilichoonekana kumfikisha Sitta hapo alipo ni namna ambavyo amekuwa akilishughulikia sakata la Richmond na mengine yanayohusu ufisadi ndani na nje ya Bunge.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza na Tanzania Daima ambao walieleza kutoridhishwa na namna suala la Sitta lilivyoshughulikiwa, walisema kwa jinsi mjadala ulivyokuwa ukienda, wachangiaji wote ni kama vile walipangwa kummaliza Sitta, kwa madai kuwa amekuwa akiruhusu mijadala inayokimaliza chama kwa hoja ya kupambana na ufisadi.
Wajumbe hao walielezea wasiwasi wao kuwa endapo Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Kikwete angekubaliana na matakwa ya wajumbe wengi ya kutaka Sitta apokwe uanachama, hali hiyo inaweza kuibua tatizo kubwa, si nchini tu, bali pia kimataifa.
Nje ya Ukumbi wa White House ambako mkutano huo ulikuwa ukiendelea, vikundi vya baadhi ya wajumbe walionekana kutofautiana kuhusu suala hilo, kwa madai kuwa limeibuliwa kwa makusudi na watu wachache wenye ushawishi kifedha ili kupunguza makali ya Sitta.
Katika hali iliyoonyesha kuwa mjadala wa NEC ni mgumu, wajumbe wa kikao hicho jana walilazimika kuendelea na kikao chao usiku kwa siku ya pili mfululizo.
Wakati huo huo, baadhi ya wajumbe na wagombea wao walikuwa wakiendelea na kampeni za lala salama katika uchaguzi wa kuziba nafasi ya ujumbe wa NEC, iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, marehemu Richard Nyaulawa, aliyefariki dunia mwaka jana. Tayari CC imeteua majina matatu kati ya 19 ya waliokuwa wameomba nafasi ya kuziba pengo la Nyaulawa. Walioteuliwa ni pamoja na Sifa Amani Swai, Jasson Rweikaza na Ramadhan Maneno, ambao walitarajiwa kupigiwa kura na wajumbe wa NEC jana.

blank.gif
 
Halafu bado watu wanasema CCM ni safi? Usafi wa CCM uko wapi? Ina maana mtu kupinga ufisadi ni kosa? Hata pale ambapo makosa yako wazi? Kweli ninawashangaa wale ambao wanakwenda kugombea kupitia CCM wakidai kwamba wataleta mabadiliko from within.

Tatizo ni chama chote kimeoza, kama kansa (saratani) inavyosambaa mwilini kiasi kwamba unashindwwa uanzie wapi kutibu, kwa hiyo na anayekwenda kugombea kupitia CCM awe tayari kuambukizwa saratani na kesho na keshokutwa akija hapa tutamuuliza amesimamia wapi? Yuko na mafisadi ama yuko na wananchi. Kweli kama kuna watu wako serious na wanataka kuwatumikia wananchi na kuwakomboa walalahoi, sidhani kama kugombea kwa kupitia CCM ni njia sahihi, hapo ni kwamba wanaenda kutafuta ulaji na baada ya hapo watafungwa midomo. Hao walioitwa First 11 wakae mkao wa kuondoka ifikapo 2010, na si ajabu watatolewa kwenye kura za maoni.

Nasubiri kikao cha Novemba, najua Zuma anataka kurudi ulingoni kwa kishindo, sabuni foma iliyotakiwa kumuosha mwezi uliopita haikuwa inatosha sasa nadhani ameenda kununua Foma Gold ili ang'ae kabisa na aweze kurudi kundini kirahisi bila maswali.

Kwa mwendo huu Tanzania tumwisha!
 
Last edited:
CCM haiokoleki, haiponyeki, na haibebeki! Ni ukosefu wa maono kufikiria kuwa matatizo ya CCM ni Spika Sitta!

Hata hivyo, wafanye hima kutimiza unabii; imesemwa na itatimia.

MMM;

Baada ya yote yaliyojiri wiki chache zilizopita na hasa ripoti ya Meremeta ambayo naona wanaCCM wamekaa kimya naomba kutoa dukuduku kidogo;

Je unadhani maamuzi haya ya CCM yana tofauti na yale ya serikali ya Putin au medvedev; au ya Chaves na venezuela?

Wazo langu ni kwamba for anyone outside CCM needs to learn from similar cases outside Africa and Tanzania and see how best we can move forward

Otherwise CCM will still lead and do the needful to the party first and then Tanzanians second

Let me declare that i am not against CCM but i am concerned jinsi approach yetu na sesitive issues inavyokwenda

Nahisi bado tupo zama za kale za mawe na wachache bado wanazungusha chain

Naona jana na leo ni darkes hours za CCM kwa public lakini sioni kama kuna nafuu

THINK OF A WOMAN WITH HIS HUSBAND CHEATING EVERYDAY AND ONCE YOU SEEK FOR WAZEE ADVICE THEN THEY GIVE YOU STERN WARNING

THINK OF A WOMAN WITH HIS HUSBAND CHEATING EVERYDAY AND ONCE YOU SEEK FOR WAZEE ADVICE THEN THEY GIVE YOU STERN WARNING

Nimeipenda hiyo ... unaweza kuta hao wazee wenyewe nao ni ma-cheater wakubwa so kumhukumu mwenzao inakuwa ni case ngumu, watamgeuka vipi?
 
Kumeingia Ufa Mkubwa CCM,na hata Msamaha wa Mh.Sitta aliouomba mbele ya wana-NEC huko Dodoma sio kwamba alipanga kuuomba,bado anajiona ana haki ya kusimamia anachoamini...sasa kazi imebaki kwa Wananchi,Msiirudishe CCM kwenye Utawala,katika Uchaguzi wa 2010.......Ile CCM aliyoiongoza Mwalimu amekwenda nayo Kaburini....CCM ya leo inaongozwa na watu wenye Uwezo wa Pesa,Huyu Kikwete kamshinikiza Mh.Sitta kuomba Msamaha leo,akumbuke kuwa Kesho itakuwa zamu yake,Hao Mafisadi wanajipanga kuwashawishi wanaCCM wenzao kumuondoa Kikwete kwa kutokuwa na Uwezo wa kushinda tena...Kikwete kazungukwa na watu wenye Uwezo na akili Kumshinda yeye....Na kwa akili yake anashindwa kuligundua hilo!.....Malecela amelijua hilo,Yeye ni supporter wa Sitta kwa kuogopa Mvurugano yupo nje ya Nchi........Mzee Mwinyi ,Mzee Msekwa wote wanajua fika kuwa Sitta ni Mkweli...Sipendi kabisa Mazingaombwe haya...Kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu.

Hapa ndipo ninapomkumbuka mwanachama wa JF anayejiita Mwanafalsafa kuna Tundiko moja alisema Nanukuu "Tanzania tumejaliwa kila kitu,kasoro yetu ni Uongozi".

Bila Uoga nathubutu kusema leo...Bila kuiondoa CCM kwenye Sanduku la kura...kila siku tutapiga mark time...maendeleo ya kweli yanazuiwa na Uongozi mbovu wa CCM....Ni karibu nusu karne sasa toka tupate Uhuru..lakini bado tumekuwa nyuma kwa huduma nyingi Muhimu kwa maisha ya kila siku.

Mwalimu aliwahi kusema kuwa...Upinzani Imara utatokea ndani ya CCM, Ewe Sitta,warudishie hao CCM hiyo kadi yao...Kwani CCM ni Mama yako?
 
Maneno mazito haya mkuu Mwawado lakini CCM bado wana mambo 2 ikikia kwenye kura .

1.Tumeya Uchaguzi ni yao watatangaza wakitaka
2.CCM ikishindwa jeshi litakuchukua Nchi .

Unasemaje juu ya haya ? Ndiyo maana Sitta hawezi kuthubutu kuacha kadi yao .Wacha tuobe Bunge lijalo itakuwaje .Lowasa and Rostam at work JK anaongozo kundi la mafisadi mbele ya macho ya watanzania masikini wa mwisho Duniani .
 
- Okay the dataz ni kwamba kwanza kikao kimekwisha, ni kweli kulikuwa na njama kubwa sana ambayo imekua ikisukwa na Lowassa, ya kumn'goa Spika.

- The dataz ni kwamba jumla ya shillingi millioni 50 zilitumika hasa kuwanunua wajumbe wa visiwani, ambao wote kwa pamoja walililia kichwa cha Spika lakini hela zilizotumika hazikuwa nyingi sana, meaning kwamba hata mafisadi wameanza kupungukiwa na pesa, kundi la upande wa pili liliweza kuwazima kwa hoja nzito sana kwamba tatizo la Spika ni la CCM kwa ujumla, na kwamba chanzo ni tatizo la Taasisis za CCM na Serikali na hasa kamati ya wabunge wa CCM.

- The compromise baada ya jaribio la kumnyanga'nya Spika kadi yake ya CCM, kushindwa ikaamuliwa kamati maalum itakayochunguza na kutoa maelekezo kwa taasisi za CCM na serikali kufanya kazi kuzuia matatizo madogo madogo ambayo siku zote huishia kuwa makubwa, na kamati itaongozwa na Rais Miwnyi.

- Katika siku zote hizi mbili, hoja ya makundi ndani ya CCM ndiyo iliyotawala vikao vyote, infact the dataz ni kwamba hoja zingine combined zilichukua only less than one hour kujadiliwa, lakini hoja moja ya Spika, ndiyo iliyoshika moto ndani ya hoja ya makundi na reconciliation. Kama ninavyosema siku zote huko Tanzania Daima, kuna mkono wa Lowassa maana mengi waliyosema sio ya kweli, hakuna wakati wowote wa kikao hicho Spika aliomba radhi on anything.

- The dataz pia ni kwamba Muungwana, was caught in the middle lakini the message was very clear na maneno maneno yake ndani ya kikao kwamba Spika anahitaji ku-watch his back na Muungwana, kwa sababu kwa mara ya kwanza hakuwa na maneno mazuri sana kuhusu Spika.

Dataz nyingine ni too hot kuzitoa kwa sasa, naomba time kidogo tuone upepo kwanza! Maana nyingi ya dataz ni za kukatisha tamaa sana kwa the so called mashujaaa!

Respect.

FMEs!
 
Dataz nyingine ni too hot kuzitoa kwa sasa, naomba time kidogo tuone upepo kwanza! Maana nyingi ya dataz ni za kukatisha tamaa sana kwa the so called mashujaaa!

Respect.

FMEs!

Naona kamanda na wewe unaelekea kubwaga manyanga. Kama unasema data zinakatisha tamaa wapiganaji, hiyo ni signal kwamba mafisadi wameshinda na kilichobaki waachieni chama ili hao wanaojiita wapiganaji wapigane kutoka nje. Maana kupigana kutoka ndani inaonekana ni ngumu sana, kila kona mafisadi wamewekana ili kulindiana maslahi yao.
 
Mh. Six ni sawa na mtu aliye ndani ya jumba la vioo (TZ) halafu anawatukana wapita njia waliokamata mawe (mafisadi), sasa wanamrushia mawe na vioo vinapata nyufa na vingine vinavunjika.
 
- Okay the dataz ni kwamba kwanza kikao kimekwisha, ni kweli kulikuwa na njama kubwa sana ambayo imekua ikisukwa na Lowassa, ya kumn'goa Spika.

- The dataz ni kwamba jumla ya shillingi millioni 50 zilitumika hasa kuwanunua wajumbe wa visiwani, ambao wote kwa pamoja walililia kichwa cha Spika lakini hela zilizotumika hazikuwa nyingi sana, meaning kwamba hata mafisadi wameanza kupungukiwa na pesa, kundi la upande wa pili liliweza kuwazima kwa hoja nzito sana kwamba tatizo la Spika ni la CCM kwa ujumla, na kwamba chanzo ni tatizo la Taasisis za CCM na Serikali na hasa kamati ya wabunge wa CCM.

- The compromise baada ya jaribio la kumnyanga'nya Spika kadi yake ya CCM, kushindwa ikaamuliwa kamati maalum itakayochunguza na kutoa maelekezo kwa taasisi za CCM na serikali kufanya kazi kuzuia matatizo madogo madogo ambayo siku zote huishia kuwa makubwa, na kamati itaongozwa na Rais Miwnyi.

- Katika siku zote hizi mbili, hoja ya makundi ndani ya CCM ndiyo iliyotawala vikao vyote, infact the dataz ni kwamba hoja zingine combined zilichukua only less than one hour kujadiliwa, lakini hoja moja ya Spika, ndiyo iliyoshika moto ndani ya hoja ya makundi na reconciliation. Kama ninavyosema siku zote huko Tanzania Daima, kuna mkono wa Lowassa maana mengi waliyosema sio ya kweli, hakuna wakati wowote wa kikao hicho Spika aliomba radhi on anything.

- The dataz pia ni kwamba Muungwana, was caught in the middle lakini the message was very clear na maneno maneno yake ndani ya kikao kwamba Spika anahitaji ku-watch his back na Muungwana, kwa sababu kwa mara ya kwanza hakuwa na maneno mazuri sana kuhusu Spika.

Dataz nyingine ni too hot kuzitoa kwa sasa, naomba time kidogo tuone upepo kwanza! Maana nyingi ya dataz ni za kukatisha tamaa sana kwa the so called mashujaaa!

Respect.

FMEs!
heshima baba!upo juu zaidi
 
Naona kamanda na wewe unaelekea kubwaga manyanga. Kama unasema data zinakatisha tamaa wapiganaji, hiyo ni signal kwamba mafisadi wameshinda na kilichobaki waachieni chama ili hao wanaojiita wapiganaji wapigane kutoka nje. Maana kupigana kutoka ndani inaonekana ni ngumu sana, kila kona mafisadi wamewekana ili kulindiana maslahi yao.

- Hapana mkuu wangu, tatizo ni Muungwana haeleweki na unajua kwua rais wetu kisheria ana power ya ajabu sana, so far anakuwa tatizo kubwa sana na everything!

Respect.

FMEs!
 
- Okay the dataz ni kwamba kwanza kikao kimekwisha, ni kweli kulikuwa na njama kubwa sana ambayo imekua ikisukwa na Lowassa, ya kumn'goa Spika.

- The dataz ni kwamba jumla ya shillingi millioni 50 zilitumika hasa kuwanunua wajumbe wa visiwani, ambao wote kwa pamoja walililia kichwa cha Spika lakini hela zilizotumika hazikuwa nyingi sana, meaning kwamba hata mafisadi wameanza kupungukiwa na pesa, kundi la upande wa pili liliweza kuwazima kwa hoja nzito sana kwamba tatizo la Spika ni la CCM kwa ujumla, na kwamba chanzo ni tatizo la Taasisis za CCM na Serikali na hasa kamati ya wabunge wa CCM.

- The compromise baada ya jaribio la kumnyanga'nya Spika kadi yake ya CCM, kushindwa ikaamuliwa kamati maalum itakayochunguza na kutoa maelekezo kwa taasisi za CCM na serikali kufanya kazi kuzuia matatizo madogo madogo ambayo siku zote huishia kuwa makubwa, na kamati itaongozwa na Rais Miwnyi.

- Katika siku zote hizi mbili, hoja ya makundi ndani ya CCM ndiyo iliyotawala vikao vyote, infact the dataz ni kwamba hoja zingine combined zilichukua only less than one hour kujadiliwa, lakini hoja moja ya Spika, ndiyo iliyoshika moto ndani ya hoja ya makundi na reconciliation. Kama ninavyosema siku zote huko Tanzania Daima, kuna mkono wa Lowassa maana mengi waliyosema sio ya kweli, hakuna wakati wowote wa kikao hicho Spika aliomba radhi on anything.

- The dataz pia ni kwamba Muungwana, was caught in the middle lakini the message was very clear na maneno maneno yake ndani ya kikao kwamba Spika anahitaji ku-watch his back na Muungwana, kwa sababu kwa mara ya kwanza hakuwa na maneno mazuri sana kuhusu Spika.

Dataz nyingine ni too hot kuzitoa kwa sasa, naomba time kidogo tuone upepo kwanza! Maana nyingi ya dataz ni za kukatisha tamaa sana kwa the so called mashujaaa!

Respect.

FMEs!

Mkubwa heshima mbele sana na kweli napenda kuthibitisha kwamba dataz ulizoleta ni bayana kabisa na zimefika kama kikao kilivyokwenda ila umefanya la maana sana ku-skip nyingine maaana watanzania huwa wanapenda kulipuka baada ya kupata taarifa fulani.

Cha msingi angalia alama za nyakati Mkuu na upepo kwa ujumla wake.
 
Back
Top Bottom