Duu
mimi binafsi nawashangaa watanzania wezangu ktk uangaliaji wa mambo na ufuatiziaji wa nyenendo,labda mimi ndiye naangalia ktk kingo za box.
Hawa mananyang'au wanao pukuchuwa nchi yetu wamekaa ktk makundi mawili ama ktk majeshi mawili ,moja la angani na lingeni la ardhini.
Lilo angani kazi yake ni kushambulia ,ni kundi ambalo liko upande wapukutuaji nchi kwa uwazi,na kundi la pili ni lile la ardhini ambalo linajinadi linapinga mafisadi ,ni kundi lilo hatari maana limejiunga na wananchi wapigania haki wa kweli ,tatizo linaanza kwamba wenye miono miepesi watapotezwa nalo,lakini hata hivyo haliitaji ugumu kulitambuwa kwani matendo yao ni tosha.
Huwezi sema una uchungu na nchi yako na unapigania ubadhirifu unaofanyika nchini kwako wakati huo huo wewe ukaishi kwenye nyumba ya mabilion ya fedha wakati ukitoka nje kilometa 1 ndani ya hekalu lako unakutana na masikini wa kutupwa ,eti tu kwa vile Bunge/ama sheria imefuata.
Hii ni sawa kabisa japo ni ngumu kuielewa yani ya kwamba je ni sahihi? kwa mjibu wa sheria/Bunge ikipitisha sheria kwamba Sitta yani spika kila siku asubuhi awe anakamata watanzania 100 na kuwalamba viboko vya nguvu itakuwa sahihi kwa vile sheria imefuatwa.?
Wapigania haki ktk nchi yao hawako tu kuangalia nini bunge/sheria inasema bali ni watu wenye kuvuta hisia za kizalendo na haki (right) ya natural ,mazingira na pia kuwa na huruma kwa ndugu zao.
Hawa akina Sitta,Mwakyembe,Kilango ,RA,Lowasa nk wote kwangu wapo ktk chungu kimoja ,tusdanganyike!! hata majambazi wanapoenda kuvamia basi na ktk mgawo ,mmoja wao akawa mjanja hugeukana na hata kupelekea kufyatuliana risasi ,anayemfyatulia jambazi mwenzie risasi si kwamba ni mwema ,ama jambazi mwingine anaenda kumchomea mwenzio polisi na huyu jambazi aliyechoma si mjambazi mwema eti kwa vile kaenda kutoa siri za jambazi mwenzie.
Mimi nafikiri tuwe huru (labda mie ndiye siye) ktk kutafari mambo tuiipe akili homework na tuichoshe zaidi ,pia tujaribu kuangalia na kuoanisha historia ya mhusika huko nyuma na anachokihubiri ktk mda muafaka.