Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Na. M. M. Mwanakijiji
Habari ambazo zimekuwa zikitiririka kwa muda wa masaa kadhaa yaliyopita zinatuthibitishia kuwa waoga wanaongoza CCM sasa hivi. Habari za kuwa Spika wa Bunge la Muungano alipewa kibano katika mojawapo ya vikao vya juu vya CCM ni habari za kuudhi, kukera, na kuchekesha; yote kwa kwa wakati mmoja. Vile vile tukio la kujadili mambo ya Bungeni na taratibu za Bungeni kuonesha kutoridhishwa kwa mwenendo wa Bunge kwenye vikao vya chama ni tukio la kulaaniwa na kukataliwa na kila mpenda demokrasia.
Kwa vile CCM wamelewa ugimbi wa madaraka inaonekana hawajui kuwa Bunge siyo tawi la CCM wala Jumuiya ya chama. Spika wa Jamhuri ya Muungano siyo Spika wa Bunge la CCM. Bunge la namna hiyo halipo.
Bunge linaendeshwa kwa taratibu zake na wakati wowote mbunge yoyote hafurahishwi au kuridhishwa na mwenendo wa Bunge taratibu zipo za kutoa malalamiko yake na kama ni kundi kubwa la wabunge basi wana nafasi ya kujadili na hata kumuondoa Spika kwa taratibu za Kibunge (Impeachment).
Lakini CCM imejinyanyua juu na kujiweka kwenye kiti cha enzi ambapo kitu kinachoitwa Katiba hakiangaliwi tena isipokuwa kadi na sheria zilizotungwa na Bunge lenyewe haziangaliwi tena bali taratibu za chama. Imefika mahali watu wanapewa uchaguzi wa "Chama" au "Taifa".
Mjadala wa viongozi hao wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao na "vigogo" wengine wa chama hao kuhusu mwenendo wa Bunge au maamuzi ya "Spika" ni mjadala potofu, usio na msingi na kwa hakika ni wa kiwoga!
Kama kuna kundi la wabunge wa CCM ambao wanaamini kuwa Spika hawatendei haki na wao ndio wako wengi Bungeni kwanini wasilete malalamishi yao ndani ya Bunge na badala yake kutumia mbinu za kiviziaji nje ya Bunge? Kama kuna watu ambao wanaona Spika anawapendelea watu wengine kwanini watu hao wasifuate taratibu za Bunge kutoa malalamiko yao?
Hawawezi. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa kuwa Bunge ni mhimili mwingine wa dola na Spika ni Mkuu wa Mhimili huo. Hawawezi kwa sababu wanajua kabisa hawaungwi mkono ndani ya Bunge; Hawawezi kwa sababu wanajua wakizungumza Bungeni Taifa zima litajua nani kazungumza nini na ana hoja gani! Wanaogopa; wanawaogopa Watanzania! Wanaogopa kujulikana!
Ni waoga.
Alichofanya Spika Sitta ni kile vitani kinaitwa "strategic retreat" yaani kurudi nyuma kimkakati ili kujipanga upya. Kama nilivyoandika wiki iliyopita hii ni vita na siyo mapambano. Unaweza ukapoteza pambano moja au mawili lakini mwisho wa siku utashinda vita.
Wao wametumia vikao vya chama, Sitta anawasubiri tena Bungeni. Bunge haliongozwi na Katiba ya CCM au maoni ya wana CCM peke yake. Hivyo, badala ya kuwapa njia rahisi ya kutokea (kumvua uanachama - kitu ambacho nina uhakika hawawezi pamoja na mikwara yao yote!) Sitta ameamua kuwapa ushindi wa pambano moja.
Ndugu zangu mafisadi wanaweza kushinda kwa sababu nyingi lakini kubwa ni kwa sababu Watanzania tumewaachia hivyo. Kuna watu ambao wanatumia hoja ya kuwa "Sitta naye si safi" hoja hii haina msingi! Uchafu wa mtu haumfanyi ashindwe kuona usafi au kuutetea usafi! Mtu mchafu ambaye hataki kusafishika au kufuata usafi wala kuupigia usafi debe ni mchafu per exellence!
Tanzania haiitaji watu wakamilifu (kwani hawapo duniani); Tanzania haiitaji watu watakatifu (wako mbinguni); Tanzania haiitaji watu wasiokosea (hawapatikani); Tanzania inahitaji watu ambao wanajua mapungufu yao, wamesahihisha makosa yao na wanakubali kusahihishwa. Watu ambao wanatukuza uadilifu na wanautafuta sana. Tanzania inahitaji viongozi ambao wanatambua wito wao kuwa ni mkubwa zaidi kuliko makosa au udhaifu wao, watu ambao wako tayari kusahihissha walikokaribu siyo wanaoendelea kunyosha vidole kuwa "fulani naye si safi"!
Ninaamini kwa moyo wangu wote, hakuna kiongozi wa Tanzania sasa hivi ambaye amesimamia wito huu wakuliinua taifa zaidi kama Spika Sitta. Leo hii anasimama kama ngao peke kati ya mafisadi kuliteka Bunge letu na wananchi kulimiliki. Spika Sitta aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya amelipa Bunge letu kile ambacho kwa miaka mingi tumekuwa tukikilalamikia; meno.
Kuna viongozi watatu wa dola yetu; Rais (Utendaji), Jaji Mkuu (mahakama) na Spika (Utungaji wa Sheria na Usimamizi wa serikali). Mhimili hii mitatu katika nchi ya demokrasia haiwezi kuwa pamoja wakati wote. Urais, Mahakama, na Bunge vikikubaliana kwa kila kitu na wakati wote basi tujue kuwa tunaishi kwenye nchi ya Udikteta! Havipaswi kukubaliana kila kitu na wakati wote; ni lazima vigongane.
Hivyo sasa tunashuhudia kugongana kati ya Urais na Bunge na huko tunakokwenda tutashuhudia kugongana kati ya Urais na Mahakama au Mahakama na Bunge. Hii ni sehemu ya demokrasia.
Ni kwa sababu hiyo tunapoona kikundi cha wahuni wachache (namaanisha neno "wahuni" katika kila maana yake mbaya) kujaribu kuliteka Bunge letu na kulijadili pembeni na kutaka lifanye mambo kwa manufaa ya kikundi cha watu hao wachache kwa jina la "chama" ni lazima tuwapinge.
Tunawapinga kwa sababu siyo kazi yao (ni wabunge Bungeni); tunawapinga kwa sababu Bunge si la kwao (ni Bunge la Watanzania); tunawapinga kwa sababu wamefanya kwa woga (wangetaka kuwa majasiri wangesimama Bungeni mbele ya huyo Spika).
Nawataadharisha CCM, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vyao; Msiliteke Bunge wala kusababisha Bunge lisimame peke yake au Spika afanye mambo yamewahi kutokea sehemu nyingine ambako kumekuwepo na mvutano kati ya Bunge na Urais. Ninawahakikishia kuwa mkiendelea kulishambulia Bunge letu namna hii (kama walivyofanya wengine mwaka jana) tutawapinga kwa nguvu zaidi kwani sasa hivi ni Bunge tu linasimama kati yetu na mafisadi waliiokubuhu wanaoshirikiana na mafisadi wa kizungu (wanaitwa wawekezaji) kutugeuza vijakazi wa milele.
Kama mnafikiri mambo hayaendi vizuri, na mnafikiri mna hoja, Bunge lina watu wenu wengi, na Rais anatoka chama chenu; vunjeni Bunge mrudi kwa wananchi sasa! Kama Bunge halichezi ngoma mnayoipiga au kuitikia mlio wa sauti zetu, rudini kwa wananchi mtafute madaraka upya.
CCM mmeruhusu utajiri wetu utweke nyara na mafisadi na sasa mnataka kuteka na Bunge letu? Nyinyi mmechagua CCM ishikeni na ikumbatieni; nyinyi mmechagua kadi za chama chenu zibebeni na mlale nazo; tuachieni Taifa letu; iacheni Katiba yetu!
Mshindwe!
niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Makala hii inaweza kutumika na gazeti lolote lile bila ya kubadilisha mtunzi.

Last edited: