Katika mazingira ya polisi kuvunja nyumba wakati mwenye nyumba hayupo hata kama kulikuwa na mjumbe bado ni tatizo. Je,vitu walivyochukua viliorodheshwa,je kulikuwa na uharaka gani wa kupelekea kuvunja mlango pasina kumsubiri mke wa mhusika arudi walau hata kumpigia simu aje,je vitu hivyo vilipelekwa wapi na kwa sababu zipi? Hapo hatuna polisi tuna mazombi.
 
Bado

Bado kuna maelezo kina nani walikuja na wakaacha namba zao. Walipofuatwa walikiri kufika sehemu husika si kulinda nyumba bali ....
mahakama ndio itakua na majibu juu ya swali lako na ndio maana kila maelezo jaji anaandika
 
mahakama ndio itakua na majibu juu ya swali lako na ndio maana kila maelezo jaji anaandika

Binafsi sijatoa hukumu wala sijauliza swali. Bali nilikuwa nimeeleza kuwa, katika kujenga hoja husika bado kuna mazingira mengine kama jirani kuhusishwa/kuwa na taarifa za aina ya watu waliofika pale, wahusika kuacha ujumbe wa namba za simu, wahusika kukili walipofuatwa na mke wa mshitakiwa, mjumbe kuhusishwa/kuwa na taarifa etc.

Haya yote yatahusika katika kujiridhisha ni nani hasa alitenda kinachoongelewa.

Hivyo, mama mwenye nyumba yake hawezi kusema ni nani alibomoa, ila mazingira yatamfanya jaji kung'amua nini kilitokea au hakikutokea na nani alihusika
 
Correction fluid zipatiwe ulinz tafadhal😅

Hata kama ni vipofu, majina yote ya wahusika, sehemu zote/vituo yaingie kwa correction fluid kupita kwanza na section karibu zote za register.

Hiyo ni kesi nyingine watapewa waitetee na si kwa wanasheria hawa wa utetezi.
 
mimi nimemueka sawa jokakuu kwamba hakuna kwenye sentensi ya shahidi palipo andikwa polisi walivunja mlango bali kumeandikwa yeye alikuta kitasa kimevunjwa

Kwani kuvunja mlango ni mpaka uvunje mbao/chuma au bati lililotengeneza mlango husika au ni pale unapoleta kasoro kwenye mlango husika ili usitimize kazi yake ya msingi/kufungwa?
 
Anaendelea na maisha yake akiwa wapi?

Wacha uongo wewe utalaanika

Kutajwa kwake kunaweza kuhitaji pia yeye kufika mahakamani iwe ni upande wowote mshitaki au mshitakiwa kama kiungo cha ushahidi muhimu. Kumbuka bado kesi kuu.
 
Unajaribu kumlaumu nani? Raisi samia eti?

Kwa taarifa yako hawa watu walifanyiwa huu unyama wakati wa mwendazake. Na ujue,serikalini watu wa mwendazake wamejaa,hususani kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Na hii kesi ni initiative yao,siyo ya raisi samia.
Umeongea vizuri sana na hapo tuko pamoja. Je kwa sasa ni nani mwenye Mamlaka ya kiutendaji kwenye nchi yetu?? Je ni hawa masaila wa mwendazake? Je ni Mama mwenyewe?? Au ni kundi la Unknowns??
 
Binafsi sijatoa hukumu wala sijauliza swali. Bali nilikuwa nimeeleza kuwa, katika kujenga hoja husika bado kuna mazingira mengine kama jirani kuhusishwa/kuwa na taarifa za aina ya watu waliofika pale, wahusika kuacha ujumbe wa namba za simu, wahusika kukili walipofuatwa na mke wa mshitakiwa, mjumbe kuhusishwa/kuwa na taarifa etc.

Haya yote yatahusika katika kujiridhisha ni nani hasa alitenda kinachoongelewa.

Hivyo, mama mwenye nyumba yake hawezi kusema ni nani alibomoa, ila mazingira yatamfanya jaji kung'amua nini kilitokea au hakikutokea na nani alihusika
yeah!na hivyo ndivyo ilivyo
 
Wanasheria watuambie kama kesi hii itakuwa upande wa utetezi wakashinda - what is impact kwa kesi ya msingi?
 
Siku za hivi karibuni kikosi hiki kimetajwa sana na kusikika sana ndani ya nchi, nimejiuliza maswali mengi, huko Jeshini kuna tatizo gani? na kwenye hiki kikosi cha 92 KJ kuna nini haswa? maana tunaambiwa wanajeshi kutoka kikosi hiki baadhi wanatuhumiwa kwa ugaidi, wengine wapo mahakamani, wengine kwa mujibu wa maelezo wapo vituo vya Mbweni au Tazara na kwa mujibu wa maelezo wanateswa, na wengine kwa mujibu wa maelezo washauawa.

Sasa nabaki najiuliza, huko kikosini kuna tatizo gani haswa lilitaka kutokea au hawa vijana wa kikosi hiki walifanya jambo gani hadi wakafanyiwa haya yote? na je hii ndo ilionekana adhabu murua kwao? hakukua na adhabu nyingine ya kuwapa?

Naamini mkuu wa majeshi anajua hili swala vzr na majenerali wenzake, ingekuwa vyema akatoka hadharani akaeleza umma ni nini kinatokea katika kikosi hiki au pengine na vikosi vingine au labda vijana wake ni watukutu au walipanga njama iliyotibuliwa aseme.

Siyo dhambi na hatakuwa amevunja kanuni za kijeshi kwa kuliongelea hili swala, kuliko kutesa binadamu mwenzio kiasi kile ni bora akaeleza umma ni nini kilijili na wanafanyaje kutatua tatizo hili.
 
Siku za hivi karibuni kikosi hiki kimetajwa sana na kusikika sana ndani ya nchi, nimejiuliza maswali mengi, huko Jeshini kuna tatizo gani? na kwenye hiki kikosi cha 92 KJ kuna nini haswa?...
Nahisi huenda kuna kikundi wametumwa na nchi jirani wachafue kikosi chetu Cha makomandoo, hii haijakaa sawa,JWTZ ni jeshi lenye sifa nzuri kimataifa
 
Back
Top Bottom