MAAJABU: Bei ya mafuta yapanda tena hadi 3247 Dar, wakati soko la dunia ikishuka mara dufu

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,835
#BIASHARA Bei ya rejareja ya mafuta ya petroli katika mwezi Desemba 2022 kwa mkoa wa Dar es Salaam, imepungua kwa shilingi 59 kwa lita ambapo petroli itauzwa shilingi 2,827 kwa lita, na bei ya dizeli pia imepungua na itauzwa kwa shilingi 3,247 kwa lita.

Bei hizi zitaanza kutumika kesho Desemba 07, 2022.

Wakati huo huo bei za mafuta zimezidi kushuka zaidi kwenye soko la dunia ambapo sasa ni dola 79 kwa pipa moja
Bei hii ni sawa na bei iliyokuwepo kabla ya vita ya Urusi na Ukraine iliyoanza mwezi wa 2 mwaka huu, ambapo kipindi hicho hapa nchini yalikuwa yakiuzwa kati ya shilingi 2400 na 2500

Angalia graph hii hapa chini kuhusu bei za mafuta duniani
1670424661165.png


1670424935707.png

1670425017532.png
 
Kuanzia jana bei ya mafuta kwenye soko la dunia imepanda tena kwa asilimia 3.
 
Bei soko la Dunia imeshuka tatizo thamani yetu ya shilling against usd na kodi ya ndani, mwanga hauko mbali tuendelee kuvumilia, ni kagiza kabla ya kupambazuka...!!!
Kuanzia jana yamepanda tena kwenye soko la dunia baada ya nchi za magharibi kuweka ukomo wa bei kwa mafuta ya Urusi.
 
Labda Ndo siku za mwisho hizi Yesu anarudi. Kila sehemu duniani hali ngumu ispokuwa GCC countries Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, UAE, Kuwait na kimtindo Oman. Yani hadi taifa takatifu teule wanalalamika hali ngumu.
 
Hii Mada ni very complicated.

Kuna uzembe pia kuna Geopolitics, especially baada ya EU kuweka ukomo wa dola 60 kwenye mafuta ya Russia, na OPEC+ wakiwa njia panda.

Duniani makampuni makubwa yanayosafirisha Mafuta kwa njia ya bahari yanategemea mikopo na bima zinatoka Ulaya, hivyo wataweza kupata hizo huduma kama watakuwa tayari kuuza kwa dola 60 au chini, hii inamuumiza Russia kwa sababu itambidi apunguze kwa zaidi ya 50% ya uzalishaji wake, na kupunguza uzalishaji ghafla in long term utapelekea vifaa na mitambo ya kuzalishia mafuta kuharibika.
 
Kuanzia jana yamepanda tena kwenye soko la dunia baada ya nchi za magharibi kuweka ukomo wa bei kwa mafuta ya Urusi.
Acha uzuzu mkuu, effect hii tutakutana nayo January!,November crude oil imeshuka kutoka 95usd per barrel hadi 85usd per barrel, ilitakiwa mwezi huu bei ishuke,definitely mwezi ujao mafuta yatapanda, majirani zetu wote bei mwezi huu mafuta yatashuka
 
Acha uzuzu mkuu, effect hii tutakutana nayo January!,November crude oil imeshuka kutoka 95usd per barrel hadi 85usd per barrel, ilitakiwa mwezi huu bei ishuke,definitely mwezi ujao mafuta yatapanda, majirani zetu wote bei mwezi huu mafuta yatashuka
Bei ya mafuta haya inatumika ya miez miwili nyuma (Muda walioagiza)
Nadhani sasa tutaanza kuagiza mafuta urusi mana inaruhusiwa hivyo nategemea price nzuri zaidi

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom