Lowassa anusurika kifo Morogoro

Lowassa anusurika kifo Morogoro

Nimeaibishwa sana, Nimedhalirika sana na Nimekerwa sana katika hili! Mh.Spika tatizo hapa ni Uwaziri Mkuu Mtu anatumia dakika 90 za mbwembwe kulidanganya bunge na umma wa watanzania? Mheshimiwa Spika nimeshauriana na familia yangu pamoja na marafiki zangu nimemwandikia barua Mh.Rais ya Kujiuzuru.

Alishasema hapo juu kwamba kuna watu waliona yeye kuwa Waziri Mkuu anafaidi kumbe yeye ana michongo mingine.Sijui ndio tembo wetu hao? RIP Magamba.+ Waziri Mkuu Mwizi.
 
Wewe ushajivua u "Father of All".

Ushamtosa mwanako Lowassa.

Lugha hii haina sio tu rehema za ubaba, bali hata ubinadamu ulio duni kabisa ambao unatakiwa kuthamini maisha ya kila mja, hata Osama Bin Laden.

Ni mjinga wa tafakuri na taamuli aso majazi tu anayeweza kukufuru kwa upotovu ulioghilibika kifedhuli kwa hamaniko hivi.

Maneno haya yanatoka kwa mtu asiye na rekodi ya kumpenda Lowassa, lakini mwenye kupenda jaha za ubinadamu zaidi.

Mkuu Kiranga , mimi nimependa namna Lugha ya kiswahili ilivyowasilishwa hapo juu ...

Yaani kuweka pamoja katika sentinsi moja maneno kama tafakuri, taamuli, aso majazi, kukufuru, upotovu, ulioghilibika, kifedhuli, hamaniko bila ya kupoteza maana.
 
Alijiuzulu na sote tunajua na ni mashahidi wa jambo hilo. Anayesema mstaafu atakuwa mwendawazimu mwenzake anayeshabikia jizi kuwa Rais, Sh88nzi type
 
Hivi marafiki zake walioko nyuma yake kuchangia makanisa mbona hawatajwi majina yao?
Well said mkuu, hii inanikumbusha mfanya biashara mmoja ambaye akitoa msaada kidogo anataka DUNIA nzima ijuwe - hii ndio hulka ya binadamu wenye political ambition za chini chini - wanatumia umasikini wa walala hoi na makanisa kujijenga kisiasa.
 
Haya mabasi yanavoendeshwa kama yanataka kupaa, hayana bumps wala nini
 
kale ka-sticker ka "Let Love Lead--TB Joshua",,,,katakuwa kamefanya mambo...nilikaona kwenye VX yake kwa nyuma
 
Waziri mkuu aliye jiuzulu Lowasa amenusurika kifo mkoani Morogoro eneo la bwawani baada ya gari lake kukoswa koswa na basi na kukwaruzwa ubavuni upande wa kulia,hakuna yeyote aliyeumia.

Lowassa alikuwa akielekea Morogoro kuchangia harambee ya ujenzi wa kanisa ambapo yeye na rafiki zake wamechangia shilingi milioni 18.

dah: inabidi na mimi nianze ujenzi wa kanisa nadhani nitapata fugu hapo,

ITV HABARI.
Usianze kwa kuiga, bali mchango wako utoke moyoni
 
Nilimsikia Mtabili Maalim kupitia kipindi cha Friday night show kipindi cha mwisho 2012 kuwa mwaka huu 2013 kuna fisadi atakufa. naona amekata rufaa lakini mwaka haujaisha tusubiri.
 
Kwa mujibu wa picha ya hilo garilake, Hajanusurika kifo kanusurika kuumia. Usitishe watu tafadhali
 
Huyu atakuwa muhimu kwako. I wish angepata mstuko wa uti wa mgongo, ili alale kitandani akiona 2015 mchakato utakavyopita bila ufisadi wake.

nakwambia ni muhimu tena hasa kwako mwenye shida ka mie tunaolialia unayelialia jifunze pia kufikiria beyond an issue.
 
tunapo fika kwenye suala zima la utu na ubinadamu sidhani kama kuna mantiki ya kumuombea mtu babaya ndiyo maana kwenye mazishi aliye mwizi na asiye mwizi,jambazi na asiye jambazi wote huwa tuna waonbea walalea mahara pema peponi
 
Mkuu naungana na Lole Gwakisa katika hili.
Hilo basi lingeingia kwa ndani kwa futi moja tu,hapo ungepata bonge la kishindo!
RIP Lowassa zingekuwa nyingi humu.

Hii "ISHU" ni publicity zaidi kuliko reality. Mbona karibu 95% ya DALADALA za Dar zina MIKWARUZO kama hiyo na mingine mpaka gari linatoboka. Nazo tuziite ni KUNUSURIKA VIFO? Kama ndo hivo nani ataishi Dar?
 
Back
Top Bottom