Msela Wa Kitaa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2021
- 2,217
- 4,272
Bradley
Inauma sanaaa kifo kisikie kwa mwingine ila ikifika kwa umpendae maumivu yake ni makali mnoooAisee pole nyingi zikufikie wewe na wafiwa, kwa kumpoteza rafiki yako kipenzi.
Kifo ni cha kuskia tu kwa watu, ila yakikikuta hasa kwa mtu wako wa karibu unaweza kutamani ufe na wewe umfuate aliko, unahisi kama vile maisha hayana maana tena sababu ya maumivu makali sana.
Pole sana MkuuAsante sana rafiki kipenzi, ndio hivyo bado niko naugulia maumivu na hali ya kutokuamini.
Mkuu hata sijaenda kokote kule, nimetulia zangu tu wapenda vya bure ndio wanaenda kuchukua.Dah
Mwamba ushahamia kwenyr mali😂😂😂😂😂
Hatq mazishi Bado?? 😆😆😆
NakuzinguaMkuu hata sijaenda kokote kule, nimetulia zangu tu wapenda vya bure ndio wanaenda kuchukua.
Tunaomboleza Mkuu kwenye huu uziNakuzingua
Na alijiunga na liva 2020Mwamba anashinda Taji la 20 akiwa na jezi namba 20 na uhai wake unafikia tamati.
RIP DJ20
View attachment 3393496
..Master aliyemleta Melwood Klopp
View attachment 3393005
Kaka usikufuru kuna ajali hapa hapa bongo tu zimeondoa familia nzima yenye baba mama na watoto zaidi ya hao wawili. Kikubwa ni kumuomba Mungu atujalie mwisho mwema.Utakuta waswahili nao wanaiga kma wazungu kuzaa watoto wawili huku akijitapa mimi watoto wengi wa nini
Ndo inakuja kutokea kma hivi mtu huna ata wa kukupeleka hospital
aaView attachment 3392925
R.I.P kutoka kwa Baba yake na Luiz Diaz
Kaka usikufuru kuna ajali hapa hapa bongo tu zimeondoa familia nzima yenye baba mama na watoto zaidi ya hao wawili. Kikubwa ni kumuomba Mungu atujalie mwisho mwema.
Hakuna aijuae kesho yak
Jamaa ameumiza watu ....Huwezi amini jana nilikuwa na night shift, nimetoka night na natakiwa nirudi night. Nilipotoka nikalala nimeamka saa saba naingia X nakuta hii kitu nikawa na scroll machozi yananitoka tu nikajiona kabisa sitaweza kwenda night ya pili nikatamani niende bar kunywa nikaona naweza kuharibu kazi.
Kuna jamaa hapa maskani nilimwambia aje alime majani yaliyozunguka nyumba hakuwa amekuja ilibidi nizime simu nikachukua jembe nikaanza kulima majani kuzunguka nyumba kuanzia saa 8 mpaka saa 12 ili tu nisipoteze focus. (Sijawahi fanya hii kazi huwa nalipa mtu afanye).
Sehemu ni kubwa nikajikuta saa 12 kasoro bado nalima tu ndio nikajiandaa kwenda job.
Hawa wachezaji mtu anaweza kuuliza kwanini huwa hupost hata status ila huyu unampost ila hajui tu connection ambayo huwa ipo kati ya sisi mashabiki na wachezaji wetu.
It's so immense kiasi kwamba hata anapohamia tu team nyingine huwa tunaumia sana achilia mbali kufa.
Jota ameniuma mazee hata night ya jana niliomba tu nipumzike nisifanye kazi.💔😭
Ukiongeza na fact kuwa ana watoto watatu wadogo wote wamezaliwa Liverpool, ametoka pia kufunga ndia juzi tu na pia amefariki na kaka yake pamoja ambao ndio watoto wa pekee wa familia yao inaumiza zaidi aseeJamaa ameumiza watu ....
Yaani Kuna groups flani za Wana Liverpool ..watu wanalia kama vile ni ndugu yao....
Jota alikuwa mpole sana, Hana makuu...natural finisher wa hali ya juu...
Ameiacha familia yake katika hali ya kustaajabu...hapa Duniani tuishi kwa unyenyekevu tuu
Rest in peace JotaJota alikuwa njiani kurudi Liverpool akitokea Ureno (Porto). Safari hii hujumuisha kusafiri kwa barabara kutoka Ureno kisha kuvuka mpaka kuingia Spain mpaka katika mji wa Santander ulioko pwani ya Kaskazini ya Spain.
Hapo ndio huchukua Ferry kutoka Santander (Spain) mpaka Plymouth au Portsmouth (UK) safari ya takribani masaa 28 mpaka 32. Baada ya kufika Plymouth au Portsmouth ndipo angemalizia tena safari kwa kuendesha mpaka Liverpool.
Kutokana na upasuaji mdogo aliokuwa amefanyiwa siku za karibuni madaktari wakamshauri asipande ndege, hata safari yake ya kutoka Liverpool kwenda Porto kwenye harusi alitumia route hiyo ya gari na ferry.
View attachment 3392869
Hiyo ndio route aliyokuwa anasafiri Jota na mdogo wake kutoka Porto kwenda Santender. Eneo penye dot nyekundu ndipo ulipo mji wa Zamora baada tu ya kuvuka mpaka kutoka Ureno kuingia Spai na eneo hili ndio ajali ilipotokea.
View attachment 3392882
Na hii ndio route ya ferry kutoka Santender mpaka UK.
Jota alikuwa akirudi kujiunga na wenzake kwaajili ya ratiba ya pre season ambayo inatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo.
R.I.P Jota the slotter.
Chalii.
Dah! Hiki kitu cha kuwa alikuwa ni mpole ndio kilicho niumiza mimi na kila ukiingia FB au social media unakuta post za kumuhusu yeye yaan mpaka sasa mwili unaishiwa nguvu 😭😭.Jamaa ameumiza watu ....
Yaani Kuna groups flani za Wana Liverpool ..watu wanalia kama vile ni ndugu yao....
Jota alikuwa mpole sana, Hana makuu...natural finisher wa hali ya juu...
Ameiacha familia yake katika hali ya kustaajabu...hapa Duniani tuishi kwa unyenyekevu tuu