Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,532
- 81,261
R.I.P Diogo Jota the slotter.
Siku ya leo imevurugika kabisa kutokana na hii habari! Mara zote washambuliaji wetu walipokuwa wakikosa magoli nilikuwa nikitamani Jota aingie. Anyway-Thank you, Diogo. #YNWADiogo Jota, mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Julai 3, 2025, huko Zamora, Hispania. Katika ajali hiyo, ndugu yake André Jota pia alipoteza maisha. Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya A-52 karibu na mji wa Palacios de Sanabria, ambapo gari walilokuwa wakisafiria lilitoka barabarani na kuwaka moto. Tukio hili limetokea siku chache tu baada ya Jota kufunga ndoa na mchumba wake Rute Cardoso [1] [2] .
Jota alikuwa na umri wa miaka 28 na alijulikana kwa mchango wake mkubwa katika klabu ya Liverpool tangu alipojiunga mwaka 2020 kutoka Wolverhampton Wanderers. Alikuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Liverpool na pia alikuwa sehemu ya timu ya taifa ya Ureno, akishiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa [3] .
Kifo chake kimesababisha mshtuko mkubwa katika ulimwengu wa soka, na mashabiki pamoja na wachezaji wenzake wameonyesha huzuni na kutoa rambirambi zao kwa familia yake
Pole sana dada liverpool taarifa za vifo vya dizain hii huwa zinashtusha sana na maumivu yake ni makali mno.Mungu wangu
Hii taarifa ndio naiona baada ya wewe kunitag
Yesu wangu,😭😭😭
Uwii
Jota jamani
Uwii siamini mimi 😭😭😭😭
Shukran mkuupoleni wana eFOOTBALL ni mchezaji wenu pia
Pole sana Rafiki, nina mwezi mmoja rafiki yangu, jirani yangu na shabiki mkubwa wa Man Utd aliondoka maumivu yake usipime, Kuondoka kwa Jota kumenitonesha kidonda tena dahHii taarifa imenitonesha jeraha ambalo bado bichi, kwani hata mimi ni miezi miwili tu iliyopita niliondokewa na mama yangu mzazi.
Inauma sana kwakweli
Uwiii😭😭😭😭💔Diogo Jota and his brother André are the only children of their parents, Joaquim Silva and Isabel Silva. There is no other sibling. And yes, both parents are still alive and vibrant. Just not in the public eye; very humble people who prefer to cheer and support their footballer sons from the shadows. They are natives of Gondomar, a small city on the outskirts of Porto.
Today, Joaquim and Isabel face a pain that has no comfort. They have lost both their sons in a single night. Two brothers who lived together, grew up playing football together, and left together.
Bora angepanda tu ndege jota wetu jamank. What a loss 🙌🏿💔💔Jota alikuwa njiani kurudi Liverpool akitokea Ureno (Porto). Safari hii hujumuisha kusafiri kwa barabara kutoka Ureno kisha kuvuka mpaka kuingia Spain mpaka katika mji wa Santander ulioko pwani ya Kaskazini ya Spain.
Hapo ndio huchukua Ferry kutoka Santander (Spain) mpaka Plymouth au Portsmouth (UK) safari ya takribani masaa 28 mpaka 32. Baada ya kufika Plymouth au Portsmouth ndipo angemalizia tena safari kwa kuendesha mpaka Liverpool.
Kutokana na upasuaji mdogo aliokuwa amefanyiwa siku za karibuni madaktari wakamshauri asipande ndege, hata safari yake ya kutoka Liverpool kwenda Porto kwenye harusi alitumia route hiyo ya gari na ferry.
View attachment 3392869
Hiyo ndio route aliyokuwa anasafiri Jota na mdogo wake kutoka Porto kwenda Santender. Eneo penye dot nyekundu ndipo ulipo mji wa Zamora baada tu ya kuvuka mpaka kutoka Ureno kuingia Spai na eneo hili ndio ajali ilipotokea.
View attachment 3392882
Na hii ndio route ya ferry kutoka Santender mpaka UK.
Jota alikuwa akirudi kujiunga na wenzake kwaajili ya ratiba ya pre season ambayo inatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo.
R.I.P Jota the slotter.
Chalii.