Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

IMG-20250703-WA0096.jpg
 
JOTA ANATUPA FUNZO JINGINE LA UPENDO VIJANA WA LEO.

Diogo Jota na Rute Cardoso Walifahamiana na kuwa marafiki 2009 wakiwa na umri wa mika 13 Shuleni,
Wote wamezaliwa 1996 Porto nchini Ureno.
2013 wakiwa Secondari walianza uhusiano,
Wamepata watoto watatu.
22 Juni 2025 wakafunga ndoa, Ni wiki mbili tu zilizopita.
Hii Leo Diogo Jota Amefariki akiwa na Kaka yake ndani ya Gari.😢
IMG-20250703-WA0125.jpg
 
🚨 TAARIFA RASMI KUTOKA LIVERPOOL!

Klabu ya Liverpool imethibitisha rasmi kuwa jezi namba 20 itaenziwa milele kwa heshima ya mchezaji wetu kipenzi Diogo Jota! 💔🇵🇹🕊️

Hii ni ishara kubwa ya kutambua mchango mkubwa wa Jota kwa klabu na jinsi alivyogusa mioyo ya mashabiki wetu. Ingawa hatujui sababu kamili ya "kustaafisha" jezi yake (kwa kawaida hii hufanyika kwa wachezaji waliostaafu au waliofariki wakiwa bado wanacheza na kuwa na mchango mkubwa sana), uamuzi huu unaonyesha jinsi anavyothaminiwa sana na klabu.

Maana yake nini kwa mashabiki?

* Kuanzia sasa, hakuna mchezaji mwingine atakayevaa jezi namba 20 ya Liverpool. Jezi hii itabaki kuwa kumbukumbu ya urithi wa Diogo Jota.

* Hii inatupa fursa ya kumkumbuka na kumuenzi Jota kwa mchango wake, mabao yake muhimu, na roho yake ya kupambana kila alipokuwa uwanjani.

Tutaendelea kumkumbuka Diogo Jota kama sehemu muhimu ya historia yetu. 🙏
 
▫️Diogo Jota alianza kucheza soka la ushindani Oktoba 2014 akiwa na umri wa miaka 17, kwa wakati huo Jota alikuwa mchezaji wa Paços de Ferreira na mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Atlético Reguengos na alifunga bao lake la kwanza siku hiyo

▫️Diogo pia Alifunga katika mechi zake mbili za kwanza za akiwa kama mchezaji wa kulipwa ( Yaani mechi mbili mfululizo )

◽ 2021/22 unabaki kuwa Msimu bora ambapo alifunga mabao 21 na assist 6 akiwa na Liverpool.

◽ Jota alicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya wakubwa ya Ureno Novemba 2019 dhidi ya Lithuania.

◽ Mechi ya mwisho kwa Ureno ni juzi dhidi ya Hispania katika fainali ya EURO.

📊 Mechi ________447
⚽ Magoli_______ 150
🅰️ Assist________78
🏆 Makombe______ 7
Hat-trick _______4
 
Mimi huwa nasema ni bora mtu augue ndiyo afe... kifo cha ajali ni kama mtu kadhulumiwa nafsi yake.

Kifo cha Diogo na Andre ni mojawapo ya vifo vya maelfu Duniani kote vinavyotokea kila siku, ila kifo cha Diogo kinaumiza sana aisee: miaka 28, familia yenye furaha, kimsingi 'amejipata' anaamua kumuoa rafiki yake wa miaka mingi na kutimiza ahadi yake, ghafla tu hayupo tena Duniani.

Kifo...!!! 💔🕊
 
Mimi huwa nasema ni bora mtu augue ndiyo afe... kifo cha ajali ni kama mtu kadhulumiwa nafsi yake.

Kifo cha Diogo na Andre ni mojawapo ya vifo vya maelfu Duniani kote vinavyotokea kila siku, ila kifo cha Diogo kinaumiza sana aisee: miaka 28, familia yenye furaha, kimsingi 'amejipata' anaamua kumuoa rafiki yake wa miaka mingi na kutimiza ahadi yake, ghafla tu hayupo tena Duniani.

Kifo...!!! 💔🕊
Inauma sanaaa, sometime huwa nahisi maisha hayana maana yoyote na kifo kinatuonea yaani kwa nini tunakufa dah
 
Poleni sana wana Liverpool, wapenzi wa mpira. Fly high 🕊 Diogo Jota and Andre Silva. You'll Never Walk Alone.View attachment 3393183
Diogo Jota and his brother André are the only children of their parents, Joaquim Silva and Isabel Silva. There is no other sibling. And yes, both parents are still alive and vibrant. Just not in the public eye; very humble people who prefer to cheer and support their footballer sons from the shadows. They are natives of Gondomar, a small city on the outskirts of Porto.

Today, Joaquim and Isabel face a pain that has no comfort. They have lost both their sons in a single night. Two brothers who lived together, grew up playing football together, and left together.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom