Kama ambavyo Sancho hakua na value ya £70m na ndio hivyo hivyo huyu Jude hana mpira wa kununuliwa kwa £130m lakini kwa vile ni wajukuu wa Malkia bei inakua predetermined affair kwa magazeti ya ubea wa michezo na mawakala wao kutengeza habari za kutakiwa na Real Madrid nk ili BvB wakomae na bei yao ili dogo apigwe mnada kwa highest bidder.
Kama ni kweli lazima amunum Muingereza pale Liverpool basi aje Declan Rise ambae ni ana afadhali kwa kua ana experience ya kucheza Premier League kwa muda mrefu.. Napata wasiwasi huyu Jude ni Sancho aliechangamka, imagine dogo Sancho pale Manjesta anakula £300k+ kwa wiki aafu ndio anacheza vile yaaani sijui ni kupagawa na ela ama Ligi ngumu hata haeleweki japo ETG amejaribu sana kumrudisha Sancho yule wa BVB lakini bado bado sasa miss Liverpool chukulia atue Jude aje aanze kusinzia huku macho yote yakiwa kwake tuone combination ya Jude, Nunes na Joao
Palhinha... Klopp kama kweli ana nia ya kusahau haya maumivu wala asihangaike sana kusaka wachezaji nje ya Uingereza kwa sababu pale pale wapo wachezaji wazuri wenye uzoefu safi wa Ligi design kama Gini, Mane, Robbo, VVD, Ox hawa walikuja na kukiwasha safi kwa kua walikua na uzoefu wa kutosha wa EPL...
Kazi ipo.
YNWA