
Mkuu kweli nimeamini kuna watu mnajua kuchambua mpira,unaweza ukamuona mchezaji kwenye mechi fulani hayupo fit kumbe kuna hesabu tu unakuta hakufanyika vizuri na kocha.Mbona haya maelezo yako yapo Kimtazamo zaidi kuliko kimpira?
Kuna maelezo niliyaandika huko juu kufanya ufafanuzi mdogo wa kilichokuwa kinaendelea jana unaweza kuyapitia.
Kwa kuongezea tu:
Jana hatukuwa na Tatizo la Mchezaji yoyote uwanjani bali kwenye First Half Unai alimu-outclass Clopp, kama utafuatilia Fainali ya Europa dhidi ya Sevilla basi utajua Unai ni Kocha wa aina gani.
Kabla ya Mechi unai alisema Amegundua udhaifu wa Liverpool/Klopp ambao hakuna Kocha yoyote aliyewahi kuugundua. Wengi tumemchukulia poa lakini kumbe alimaanisha alichokisema.
Hivyo Keita na Thiago hawakupotea uwanjani accidentally bali ni Unai plan kuwapoteza kwa kuhakikisha hawapokei mpira wala hawatoi mpira kwa mshambuliaji yoyote.
Unai alijua kuwa zuia Keita na Thiago tayari umeizuia Liverpool kwa upande wa Washambuliaji.
Mwiba wa kuvuruga game plan ya Unai ni Diaz: Unajua kwanini?
Defensive Line ya Villarreal kwenye First Half iliziba space zote na Kufanya RB kuziba nafasi baina yake na RCB, hivyo mane hakuwa na space ya kupita.
LB aliziba nafasi baina yake na LCB na kumfanya Salah akose Space ya kupita.
Hivyo ikapelekea kusiwe na space yoyote between LCB na RCB na ikapelekea Jota akawa kama mdoli tu pale mbele.
Nini Klopp alichokishtukia na nini alichokifanya Diaz kuvunja mipango ya Unai?
Alimtoa Jota na kumuingiza Diaz ili kutengeneza Space baina ya Walinzi. Kivipi?
Baada ya kuingia Diaz kama ulikuwa makini alikuwa akichezea pembeni kabisa kwenye Chaki na sio kucheza inside left? Kwanini Diaz alikuwa akitembea na Chaki? Huu ni mpango maalum iliyomfanya RB wa Villarreal kukiacha RCB na kukimbilia mbali kwenye Chaki kwenda kumkaba Diaz.
Kudadeki! Hapo RCB akaachwa pekeyake kwenye mataa na kutengeneza bonge la Pace baina yake na RB, hapo ikambidi nayeye atanue kidogo kupunguza ukubwa wa sapce baina yake na RB, hii ikapelekea sapace baina yake na LCB kuongezeka.
Na upande mwingine Salah naye akasogea pembeni zaidi kumvuta LB ili amfuate kwenye Chaki aache nafasi katikati, hapo RCB na LCB wakawa exposed 😂😂
Ndiyo DM na namba 8 wao wakashuka chini kuja kusaidia kuziba space zilizoachwa wazi! Ndiyo hapo Thiago, Keita na Fabinho wakawa released na huru kucheza wanavyotaka na ikapelekea Maangamizi kwa Unai 😂😂
Ndugu tukiambiwa mpira ni Sayansi sio Lawama tukubali tu.
Kama Tatizo lilikuwa Keita Klopp asingemuingiza Hendo dakika za mwisho tukiwa tumeshajihakikishia ushindi.





Mtakuja kupigika mara mbili ,Sitaki kusema direct kwamba nawaogopa city ila ningependa kukutana na madrid![]()



mnaleta visasi kwenye football 
Mi nawataka nyie shity najua Pep ataovathink tena
Hakika...ataingia fainali ya tano ndani ya muda mfupi ujao.View attachment 2211457
Klopp made for Liverpool and Liverpool made for Klopp haha perfect match.
Hii rekodi mpaka 2026 haitosoma hivi
YNWA
Mkuu wacha na Sisi tufurahi, tumepitia magumu mno, tulisemwa sana. Mara Liverpool ina miaka 30 bila ubingwa wa epl, mara hakuna kombe la maana kwa karibuni tofauti na UEFA ya 2005.Imagine Being Us
Na akibeba UCL, linafuataMkuu wacha na Sisi tufurahi, tumepitia magumu mno, tulisemwa sana. Mara Liverpool ina miaka 30 bila ubingwa wa epl, mara hakuna kombe la maana kwa karibuni tofauti na UEFA ya 2005.
Ile 2008 kuna wanoko walichukua makombe yote waliyoshiriki wakawa na midomo kama tarumbeta, mbaya zaidi ile 2009 Madrid (tunawadai pakubwa sana) wakatupokonya Alonso, timu ikawa kama imekatika. Literally first eleven ilikuwa ni Reina, Gerald, na Torres. Kuna kipindi hadi UEFA tunaiangalia kwenye TV tu, siye zetu ilikuwa Alihamisi tukabondwe na kina Atiletico, Sevila, Valencia na Vila real(hawa ndio walikuwa wamiliki wa europa cup).
Sasa hivi tunachukulia for granted kuangalia Liverpool akicheza fainali tatu kubwa Ulaya ndani ya msimu mmoja zingatia nafasi aliyonayo ya kuchukua EPL, lakini tusisahau miaka kumi nyuma ndoto zetu kwenye msimu ilikuwa kumaliza top four EPL(It was not easy being us). Maswala ya ubingwa wa FA, EPL, UEFA, yalikuwa ya kina Man UTD, Chelsea, Real Madrid, Baryurn, Barcelona n.k ambao kwa sasa wana wish wakutane na Shetani kuliko Liverpool. Wakikutana na Shetani watafanya maombi na Dua kumkabili lakini hakuna mbinu au silaha itokayo Peponi ama Jehanamu inayoweza kuikabili Liver.
Jurgen Klopp anastahili credit kwenye hii revolution iliyotokea ndani ya Liverpool. Mambo aliyofanikisha ndani ya miaka 7 inawafanya watu wamuone kama vile ana miaka 3 tu, yaani bado tunamuona ni mpya.
Iwapo Liver atafanikiwa kuchukua quadruple itakuwa ni mapinduzi mengine ndani ya LFC. Itaifanya Liver iwe the brightest football brand in Europe. Makampuni makubwa, mashabiki wapya, wachezaji mastaa wakubwa watataka kujihusisha na Liverpool, then automatically LFC itajiseti kwenye momentum ya kutawala soka la Ulaya kwa miaka kadhaa ijayo.
The future is bright, YNWA.
@Pain killer njoo ukatike huku, uje ukiwa umelowesha hiyo kanga na majiMtakuja kupigika mara mbili ,mnaleta visasi kwenye football
![]()