Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA

[emoji599]Orodha fupi ya washambuliaji wanaohitajika na Klabu ya Arsenal msimu huu wa joto.

Lautaro Martinez -- Inter Milan
Gabriel Jesus __ Manchester city
Dominic Calvert-Lewin-- Everton

[emoji117]Arsenal wanatarajiwa kuwasaini washambuliaji wawili

[emoji117]Inter Milan wao wanataka kitita kati ya euro million €70 na €80 kwa Lautaro Martinez.

Chanzo: Times)

[emoji599]Everton itakuwa tayari kukubali dau la pound million £50 kwa timu inayotaka saini ya mshambuliaji wake Richarlison raia wa Brazil.

Kwa mjibu wa Football Insider)

[emoji599]Kiungo wa kati wa Ureno Ruben Nerves anatarajiwa kuondoka Wolves msimu huu wa joto, kipaumbele Cha kiungo huyo ni kujiunga na Klabu ya Barcelona.
Arsenal na Manchester United pia wanahutaji Saini yake.
Chanzo: Sport)

[emoji599]Tottenham Hotspur wameonyesha Nia ya kutaka kumsajili beki wa Klabu ya RB Leipzig Josko Gvardiol na beki wa kati wa Klabu ya Inter Milan Alessandro Bastoni.

Kwa mjibu wa Athletic)

[emoji599]Kiungo wa klabu ya RB Leipzig Konrad Laimer yupo kwenye rada za Bayern Munich, Liverpool, na Tottenham Hotspur.

Kwa mjibu wa Kicker)

[emoji599]Klabu ya Norwich City inatarajia beki wake wa kulia Max Aarons ataondoka klabuni hapo msimu huu wa joto mara baada ya klabu hiyo kushuka daraja.

Chanzo: Telegraph)

[emoji599]Cesar Azpilicueta na Marcos Alonso wote wanataka kujiunga na Klabu ya Barcelona msimu huu wa joto.

Chanzo: Mundo Deportivo)

[emoji599]Klabu ya Napoli imewaambia Arsenal kuwa itawagharimu taklibani pound million £100 Ili kupata Saini ya mshambuliaji Victor Osimhen msimu wa joto.

Chanzo: Sun Sport)

[emoji599]Ludovic Giuly anaongoza katika mbio za kuwa kocha wa klabu ya Barcelona B dhidi ya Javier Mascherano na Antonio Hidalgo.

Chanzo: Sport)

[emoji599]Manchester United imempa ofa Ousmane Dembele ya mshahara kati ya euro million €10 na 15 Ili kujiunga nao kwa uhamisho huru msimu huu wa joto.

PSG wao wamempa ofa ya mshahara wa euro million €17 kwa mwaka.

Chanzo: Dario Montero G)

[emoji599]Mkataba mpya wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp hautajumuisha ongezeko la mshahara lakini alihakikisha wasaidizi wake wanaongezwa.

Chanzo: David Oenstein)

[emoji599]Klabu ya Bayern Munich haitamuuza mshambuliaji wa Robert Lewandowski msimu huu wa joto na tayari wamemwambia mchezaji na wakala wake kuhusu uamuzi wao.

Chanzo: DiMarzio)

[emoji599]Romelu Lukaku anatarajiwa kukataa nafasi yeyote kutoka AC Milan msimu huu wa joto kutokana na uhusiano wake na Inter Milan

Chanzo: Evening Standard)
 
Sijapinga maelezo yako ni huyo kocha alicheza Anfield na anamjuwa klopp vizuri lakini tuliona jinsi Villa alivyocheza vibaya Anfield. Namuongea Keita kipindi cha kwanza kama yeye hata kama hukucheza vizuri lakini alifanya makosa mengi sana kuna kipindi akataka hata kuwapa penalty wale jamaa na pass ya nyuma bila kuangalia. Baya zaidi Arnold na Robertson walicheza hovyo sana kipindi cha kwanza sio kushambulia hata defence. Sote tunajuwa Liver ni bora kuliko walivyocheza kipindi cha kwanza sasa ukisema Unai anamjuwa sana Klopp kwani alivyoenda Anfield alikuwa hamjui? second half almsahau Klop? Liver kwa team ni bora kuliko Villa kwa mbali zinatokea siku huchezi vizuri team au mchezaji. Hakuna hata mchambuzi mmoja aliona kuwa atatolewa Jota na kuingia Diaz kipindi cha pili kwa baade tulijuwa Diaz ataingia kila mtu alikuwa anaona shida ni Keita na Thiago lakini hakuwatoa. Liver waliingia na kucheza kama Liver na Mane miaka yote na mafanikio yetu alikuwa anatoka huko kushoto tusiseme leo Mane sio mzuri kushoto hiyo ndio nafasi yake. Jamaa walichoka tu mziki ulivyoanza.
Mkuu inaonekana wewe ni mbishi sana
 
Mkuu inaonekana wewe ni mbishi sana
Hapana mimi sio mbishi ila napenda majadiliano na napenda kumsikiliza mtu mawazo yake lakini sio lazima nikubaliane na kila mtu au watu wakubaliane na mimi, unajuwa mpira tunatizama mmoja lakini ukiisha tunakuwa na maono tofauti hata huko majuu studio wanakuwa na maoni tofauti ila haimfanyi mmoja kuwa sawa na mwingine sio sawa ni maoni tofauti tu kwa kitu kimoja.
 
Adjustments.jpg
 
Hapana mimi sio mbishi ila napenda majadiliano na napenda kumsikiliza mtu mawazo yake lakini sio lazima nikubaliane na kila mtu au watu wakubaliane na mimi, unajuwa mpira tunatizama mmoja lakini ukiisha tunakuwa na maono tofauti hata huko majuu studio wanakuwa na maoni tofauti ila haimfanyi mmoja kuwa sawa na mwingine sio sawa ni maoni tofauti tu kwa kitu kimoja.
Tatizo unajenga hoja kwa uelewa wako, wakati huko juu umeshajibiwa kiprofessional jinsi Game plan zilivyokuwa uwanjani mpaka tukapata ushindi.

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom