Kuna kitu hutakiwi kusahau! Project ya Arteta inaweza ikakwamishwa na Vitu vilivyo nje ya uwezo wake na ikapelekea isilete mafanikio. You know why? Nakumbuka Misimu miwili ya mwanzo ya Klopp project yake ilifeli vibaya sana licha ya kuintroduce gengenpressing kwenye EPL lakini kulingana na qualities ya Wachezaji alifeli kwasababu ya kuwa na very limited Budget ya kusajili wachezaji aina ya Origi.
Mafanikio aliyapata baada ya kununua wachezaji aina ya VVD, Fabinho, Alisson, Salah, Mane na Keita ambao kiuhalisia ni Very expensive.
Hivyo mbinu pekee haziwezi kuleta mafanikio isipokuwa Budget ya uhakika ya kuweza kusajili wachezaji wenye Vipaji nayo ni moja ya Factors za kuleta mafanikio.
Na sasa baada ya Umri wa kina Salah na Firmino kusogea tayari Jota na Diaz wamesajiliwa.
Hivyo Talented Players + Arteta = Trophy.
Sasa je Wamiliki wenu watamsapoti Arteta kwenye Market ili anunie the likes ya VVD, Fabinho, Diaz, Alisson, Mane?
Na kama Wamiliki watashindwa maanayake yatawafika kama yaliyotufika sisi kukimbiwa na kina Sterling, Torres, Mascherano, Alonso, Suarez kwa ajili ya kwenda kutafuta Makombe.
Hivyo Superpowers watahijack Vijana wenu kina Saka na Martinel na kuwarudisha nyuma katika project yenu.