View attachment 2048058
Salah jana hakufurahia kutolewa kama ambavyo siku zote hua hafurahii kutolewa.
Upande fulani unamwelewa kwa vile dogo ni mpambanaji mpaka kipenga cha mwisho akitaka goli ama atoe assist.
Upande mwingine sasa nae ni binadamu anahitaji mwili uwe na utulivu kujiweka sawa akusanye nguvu upya kwani mechi kuanzia hii ya jana mpaka tarehe 2 kuna mechi 6 kali tunacheza EPL mpaka tarehe 2/1/22.
Upande mwingine pia sasa afahamu hata wanaosubiri kwenye benchi nao wanahitaji dakika kadhaa uwajani kupambana kwa ajili ya timu.
Najiuliza hivi akina Gomez, Origi, Tsimikas, Ox, Keita, Taikumi ambao muda mwingi hua hawapati namba kikosi cha kwanza hua wanajisikia aje kila siku ya mechi wakianzia benchi bila kua na uhakika wa kupata kucheza mpaka pale aidha itokee majeruhi ama sub kama jana vile.
Naona hii ni unspormanship way kwa kuzingatia tunakoelekea mpaka January 2 na mechi zilivyobanana na zikiwa zinatisha. Fair play muhimu kwa kujenga umoja wa kikosi na pale mwalimu anatoa ishara ya sub basi mchezaji yeyote awe tayari kutoka bila kuonyesha kama kukereka fulani. Wote kazi ni moja tu kuiletea klabu hii mafanikio na hii ni kazi ya wakiwa kama kundi sio mchezaji mmoja mmoja.
Klopp aa usual hanaga mambo ya kung'ang'ania jambo jana ile ile kaipotezea chap na kuanza mipango mechi ijayo dhidi ya Tottenham Jumapili.
YNWA