Captain Marvelous
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 15,313
- 32,605
Been tight fellow Kopite..Nasubiri mkuu
Hold on Queen Reds.
YNWA
Been tight fellow Kopite..Nasubiri mkuu
Bwana wee Kipara kwa kweli hapa washindwe wao tu ratiba kwao imewapedelea sanaaa.Katika hii Fixtures ni Man City pekee ndiyo mwenye Kitonga cha mteremko.

Nimecheka sana daaaahChelsea fans :
We are Winning the League
We are winning the Leag
we are winning the Le
We are Winning the
We are winning
We are w
We are
We
We are
We are Play…
We are Playing
We are Playing for
We are Playing for top
We are playing for top 4![]()
Nafikiri walitaniana kitu, walicheka wote (niliipenda ile moment i wish ningesikia walichongea).. Hasa kwa aliyofanya Mane na kukosa lile goli (alifanya job well done moja) la kukosa kwake kukamnufaish ma Salah.. Kama Salah angekosa lingewekwa tu.
Chelsea fans :
We are Winning the League
We are winning the Leag
we are winning the Le
We are Winning the
We are winning
We are w
We are
We
We are
We are Play…
We are Playing
We are Playing for
We are Playing for top
We are playing for top 4![]()

,Leo tupo na Captain Fantastic aka Mr Liverpool the dude himself MBE Steven Gerrard.Nasubiri mkuu
Huyu kaka nilimpenda na ninampenda mno.Leo tupo na Captain Fantastic aka Mr Liverpool the dude himself MBE Steven Gerrard.
Alizaliwa 30/5/1980, Whiston Knowsley England. Wazazi wake ni Baba Paul Gerrard na Mama ni Julie Ann Gerrard.
Alizaliwa na tatizo club foots. Wazazi wake walipambana mpaka akapona ili aweze kutimiza ndoto yake ya kucheza mpira.
Miguu yake ilikua hivi
View attachment 2047398
Alisoma shule ya Msingi ya St Micheal.
Nyumbani kwa wazazi wake ilikua jirani zaidi na Uwanja wa Everton hivyo Gerrard akiwa mdogo alikua anatembelea makumbusho ya Everton huku akipiga picha na vikombe na kuvaa jezi ya watoto ya Everton. Aliwapenda sana Everton kwani ndio mahala aliweza kufika na kuona mafanikio ya mpira.
View attachment 2047603
Safari yake ya mpira ilianza kujaribu timu ya kitaa ya Tolgate lakini walimkataa wakisema ana mwili mdogo sana. Wiki hii ilikua mbaya kwake kwani wakati wanacheza mpira kitaa alijikata na kopo la Coca Cola.
Gerrard kutokana na matatizo ya kiafya mwili wake ulidumaa kukua kwa kasi akawa anakua kwa kasi ndogo sana tofauti na watoto wengine. Lakini hili halikumzuia kujaribu na kufanikiwa.
Pia akiwa mdogo wakati anacheza mpira na watoto wenzie aliwai kujikata kidole na sululu wakati wakacheza mpira kitaa kwenye majani, dogo alikua anapiga mpira kumbe pale kwenye palikua na sululu badala apige mpira akakosea na kupiga sululu na kuchana vidole vyake vibaya sana. Hili jeraha lilikua mbaya sana kwake kwani Dokta wa kwanza aliemhudumia alisema wakate kidole kile lakini wazazi wake kwa kutambua kidole kikikatwa asingeweza tena kucheza mpira waligoma ushauri na kumpleka hospitali nyingine na hatimae akapona.
Alijaribu kujiunga na timu kadhaa za vijana wakiwemo Manchester United nk lakini hakubahatika.
Hakufanikiwa kwenda Lilleshall, Centre ya kitaifa ya mpira kwa kukosa urefu uliohitajika.
Alijiunga na klabu ya kitaa ya Whiston Juniors mpaka akiwa na miaka 8. Ma scout wa Liverpool walimuona wakati anacheza pale na akiwa na miaka 9 akajiunga Liverpool.
Akiwa na miaka 14 alijaribu kuodoka Liverpool lakini hakufanikiwa. Kingine pia kilichochangia mara nyingi akwame maedeleo yake ni kutokana na majeraha ya mara kwa mara aliyokua anapata. Akiwa na miaka 14 mpaka 16 alikua anasubuliwa sana mgongo. Hili ilimpelekea kucheza gemu 20 tu kwa miaka miwili.
Alidumu timu ya vijana Liverpool mpaka akiwa na miaka 17 ndio akapata mkataba wake wa kwanza. Mkataba huu alisaini 5/11/1997.
Mwaka 1998 Jamie Redknapp aliumia hivyo Steven Gerrard akapata nafasi ya kucheza gemu yake kwanza Liverpool. Ilikua gemu dhidi ya Blackburn Rovers. Liverpool walishinda 2 bila.
Meneja mpya wa Liverpool Gerard Paul Francis Houllier ndio alimpa Steven Gerrard mechi yake ya kwanza Liverpool.
Alicheza gemu 13 msimu huo lakini tatizo la mgongo likawa linamsubua sana.
Key Points Steven.
*Alikua kiongozi tangu akiwa na umri mdogo. Alikua complete Midfielder akiwa na uwezo wa kufunga, kuzuia, kutoa pasi, kuhamasisha nk
* Alifunga goli lake kwanza dakika ya 69 akipewa assist na Rigobert Song tarehe 5/12/99 mechi dhidi ya Sheffield Wednesday.
* Alicheza mechi yake ya kwanza kimataifa 31/10/2000.
* Mwezi Oktoba 2003 akawa rasmi Captain wa Liverpool. Na pia mwaka huo akaongeza mkataba wake Liverpool.
* Mwaka 2004 Mourinho alijaribu kumshawishi ajiunge na Chelsea na japo Gerrard anadai aliwa consider uhamisho lakini mwishowe alibakie Liverpool. Pia mwaka 2012 Bayern nao walimshawishi kujiunga nao lakini hukuodoka Liverpool. Na Mourinho tena akiwa Real Madrid alijaribu kumsajili ikashidikana tena Steve kuodoka Liverpool kutokana na mapenzi yake kwa hii timu.
* Akiwa Liverpool alishinda makombe yafuatao.
.....*FA Cup 2000
.....*League Cup 2000
.....*League Cup 2002
.....*FA Charity Shield Cup 2001
....*Uefa Cup 2000
.....*Uefa Super Cup 2001
.....*FA Cup 2005.
.....*Uefa Champions League 2005
.....*Community Shield Cup 2006
..... *League Cup 2012.
* mwaka 2007alipata MBE (Member Of The Order Of The British Empire) kutoka kwa Malkia Elizabeth.
* Mwaka 2007 alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Alex Curran. Wana watoto wanne wa kike Lilly Ella 2003,Lexie 2006, Lourdes 2011 na wa kiume Lio.
*Alifunga ndoa siku moja na Michel Carrick na Gary Neville.
* Mwaka 2008 alipata digrii ya heshima kutoka Chuo cha Liverpool John Moore University.
View attachment 2047622
* Ndio mchezaji pekee aliefunga goli katika fainali za FA Cup, League Cup, Uefa Cup na Uefa Champions League na hivyo mashabiki kumpa jina Captain Fantastic.
* Wachezaji hawa alisema ndio bora kabisa kuwai cheza nao timu moja Xavi Alonso, Fernando Torres, Luiz Surez na Wayne Rooney.
* Ni mchezaji wa tatu mpaka anastaafu kucheza zaidi mechi 500 akiwa na timu. Akitanguliwa na Jimmy Carragher mechi 508 akiwa na Liverpool na Giggs mechi 625 akiwa Manchester United.
* Msimu wa 2005 2006 ulikua msimu bora kwake akifunga zaidi ya goli 20.
* Ndie mchezaji wa Liverpool aliedumu muda mrefu akiwa Captain wa klabu. Alidumu miaka 12.
* Alichezea Liverpool kwa miaka 17.
* Amecheza mechi 710 Liverpool. Akifunga magoli 186 na kutoa assist 145.
*EPL alicheza mechi 504 akifunga magoli 120 na kutoa assist 92
* Alifunga goli lake la mwisho kwa Liverpool ugenini mechi dhidi ya Stoke City tarehe 24/5/15 akapwe assist na Rickie Lambert.
* Gerrard alisema endapo angepewa mkataba mapema na wenye masharti rafiki alikua tayari kuedelea kuitumikia Liverpool lakini sio Rodgers wala FSG walionyesha nia ya kuongeza mkataba. Pia kitendo cha kuwekwa benchi ile mechi ya Real Madrid bila maelezo yoyote kutoka kwa Kocha kilichangia kuona ni muda sahihi yeye kutafuta timu nyingine. Kutokana na kuipenda sana Liverpool alikwenda America kumalizia masiha yake ya kucheza kwa vile alisema asingependa aje cheza mechi dhidi ya Liverpool akiwa timu pinzani.
* Mkataba wake ulivyoisha aliodoka Liverpool na kuijunga na LA Galaxy kwa mkataba wa miezi 18.
* Tarehe 24/11/2016 Gerrard akatangaza rasmi kustaafu kucheza mpira.
* Aliingia rasmi kwenye English Football Hall of Fame mwaka 2017
* January 2017 alipata kazi Liverpool kama kocha ya timu ya vijana na akaanza kazi February 2017. Alikutana na Klopp na Alex Ingelthorpe na walivutiwa sana kwa namna alivyoongea nao kuhusu mpira kwa kukuza vipaji pale Liverpool na April 2017 Gerrard akawa mwalimu wa vijana chini ya miaka 18.
September 2017 akapadishwa kua kocha wa Vijana Chini ya miaka 19 walioshiriki Uefa kwa vijana.
* Alicheza Movie inaitwa Will akiwa na Jimmy Carragher, Kenny Dalglish nk
* mwaka 2018 aliodoka Liverpool baada ya kupata baraka za Klopp na akasaini mkataba wa miaka minne kuinoa Glasgow Rangers ya Scotland.
* Msimu wake wa tatu pale Scotland ambao ni 2020 2021 ulikua bora kwake kwani walichukua ubingwa wa Ligi Scotland bila kupoteza mechi.
* Aliodoka Rangers na kuajiriwa pale Midlands Mashariki timu ya Aston Villa November 2021.
* Mwaka 2021 aliingia rasmi Premier League Hall of Fame.
Huyu ndie meneja mtarajiwa wa Liverpool historia yake kwa kifupi sana.
YNWA










Na hii Ollachuga Oc ataikataa.
Ndio wanamaanisha nini hapa?