Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Shots 23 afu unasema tulikua tunalinda
Hizo shots mmezipata baada ya red card kuwa mkweli red imewabeba bila hiyo red leo mngepigwa kabla ya red card mchezaji wenu mmoja tu ambaye ni Mane ndio aliweza kuingia ndani ya box.Plan ya Tuchel ilikufa baada ya red ndio maana akafanya sub ya kulazimishwa kwakumtoa Kai havert ( kiungo mshambuliaji) akaingiza beki ili kulinda draw
 
Yani kama siyo red card tungewanywa hapo kwenu hii game huyu refaree aliyoichezesha ni mamluki huwa ayipendi Chelsea muna bahati sana kuku nyie
Nani aliwazuia kumleta refa wenu?!
Mnalalamikia red card! Hebu weka hapa takwimu za 1half tuone....mnachojua ni kupaki vichwa vya train tu!
 
@Captain Marvelous anaweza sifia, the guy huwa ni kops na smtime huwa anaweka ushabiki pemben na kuongea mpira,

Post zake nyingi humu huwa anaweka ushabiki pembeni, na kuongea kuhus mpira
Chelsea outsmarted us

Klopp alidhani Chelsea ni small team kama zaman

Chelsea ni kubwa sana aisee kwa sasa huwezi tegemea Elliot ndo ai unlock chelsea dakika 90 klopp katukosea sana leo aombe msamaha
 
Klopp kazinguwa sana leo
Chelsea outsmarted us

Klopp alidhani Chelsea ni small team kama zaman

Chelsea ni kubwa sana aisee kwa sasa huwezi tegemea Elliot ndo ai unlock chelsea dakika 90 klopp katukosea sana leo aombe msamaha
 
Chelsea watabaki isingekua ile red card, red ni part of the game penalty too. Ila ikiwa upande wako ni maumivu na ikiwa kwa mpinzani wako ni kicheko

Chelsea yeyote hawezi kuja kusemaile sio kona iliyowapa goli zaidi watakomaa na red card halafu mtu anataka tuwasifie.

Naamini ukizungumza kiupenzi wa mpira na sio ushabiki majibu yatakuja vivyo hivyo na kinyume chake ni sawa pia.

Lakini haya yooooote ndio utamu wa mpira ulipo kikubwa kutovunjiana heshima.

31/8 still we have room to do something otherwise struggling kwa upande wetu kuhusu UNLOCKING DEEP DEFENDING TEAMS tutateseka nazo.

Credit kwa Tuchel Credit kwa mendy the guy did it what a goalie suppose to do...

Credit kwa Matip one on one man soldier kamfanya lukaku aonekane wa 2015, kuna tik tak alii block otherwise tungezungumza mengine...

Race itakua nzuri season hii kuanzia champion to europe league qualifiers...

Tusubiri international break maana hizi timu za taifa huletaga maafa kwa wachezaji.


YNWA...
 
Klopp kwa maoni yangu jana kafanya makosa maeneo mawili. Kwanza ni kumwanzisha Bobby badala ya Jota. Na Robbo badala ya Smikas .Robbo hajarudi kwenye kiwango chake cha miaka miwili iliyopita. Zile ranning alizokuwa anaanzishia mashamnulizi jana hazikuwepo. Hii ilipelekea Mane kuonekana kaflop.
Bobby Muda wke umeisha pale Anfild. Kwanza yupo slow, anapokuwa na mpira. Amepoteza umakini kwa kiwango cha juu. Hata kujiamia hakupo tena.
 
Mimi niliangalia mpira na wala sijaenda kucomfirm matokeo niliyobeba Mfukoni that's why nasema tumecheza Vizuri.

Ila tumeshindwa kuibuka na ushindi kwa sababu ndogondogo tu za kiufundi.

- Kwanza: Kuna wachezaji ambao tayari zile skills zao za kimpira zimeshapotea ambao ni Mane na Firmino.
Firmino: Hakupaswa kuanza kwenye game ya jana na ukweli usiofichika tokea last season hakupaswa kuwa Mchezaji wa kikosi cha kwanza kwani hana tena kabisa uwezo, hivyo yeye akiwa kama Striker anakuwa sio tishio tena kwa maadui.
Mane: Pia amepoteza skills za kudribble na kufanya maamuzi, he can't shot, can't score, can't dribble and can't pass. Anaburuta mipira mingi na kuishia kuiwacha miguuni mwa adui, hivyo hakuwa threat kwenye Defence line ya Chelsea.

Pia kuna wachezaji waliocheza chini ya kiwango:

1) Robertson
2) Henderson
Hawa ni wachezaji ambao kwa jana walikuwa hawajui wanafanya nini uwanjani, kwa sasa Tsimikas yupo bora kuliko Robertson na anaweza kuchukua namba ya Robbo.
Henderson hapaswi kuwa Mchezaji wa kikosi cha kwanza kwani ameshapoteza uwezo.
 
Pengo la Coutinho halijawai zibwa ukitathmini haya maelezo
Kabisa ndugu we lack that kind of dude klabuni na waliopo wana offer something different.

Klopp sijui hua anaogopa kitu gani. With Chelsea 1 man down ilitakiwa aingie Keita na Chamberlain at least hawa niball carriers at some degree.

Nwa that is past. Tujipange kwa yajayo.

Tupo na Leeds aafu UCL tupo na Milan.

Hopefully wanaokwenda mechi Kimataifa watarejea wakiwa wazima.

YNWA
 
Amezngua mnooo
That Klopp at his best. On his day he is the best of the best. Well he do have those days kama jana.

He will learn from jana na be better au asajili kabisa tuodokane na haya maneno.

Mara pap akatua namba 8 Bissouma haha..

Klopp come on request the cheque from the Yankees itue Seagulls.

YNWA
 
Tukiondoa ile penalty na Reece James kupewa Red ina maana Liverpool wangefungwa goli sio chini ya 3 kwenu na mbele ya mashabiki wenu

Hapa unachoongea ni ushabiki tu lakini sio facts za kimpira.

Labda nikuulize kabla ya ile Red kuna threat yoyote ambayo muliifanya tunayoweza kusema ingeliweza kuzalisha goli?
OK mulikuwa munaongoza lakini, hata hilo goli lenu ni la kawaida la Free head sio kwamba kulikuwa na movement yoyote ya kupika goli.
Na hata possession kabla ya Red Liver ilikuwa juu ingawa munadanganyana Liver kabla ya Red ilikuwa haifiki kwenye FainL third yenu wakati hiyo red ilitokea katika last line yenu na sio Final third. Na asingeushika mpira ulikuwa ni goli tu hata hiyo penalty isingelipigwa.

Huo uwezo munaojisifia hamukuwa nao kwani nilishindwa hata kumiliki mpira.

Na kwaida ya mpira baada ya Red ndiyo mulicheza kwa umakini zaidi wa kujilinda, hivyo pengine musingepata Red ndiyo mungefungwa kutokana na uroho wa kutaka kufunga huku mungekosa umakini wa kujilinda. Yote hayo ni Probability.

Hivyo zungumzeni mambo kimpira na badilikeni sasa achaneni na baadhi ya Washabiki wenu wasioeleweka kufanya akili zao ndiyo munabeba nyinyi munaoeleweka.

Nadhani ungetulia kuiangalia mechi ya Jana licha ya Red Cards basi ungegundua kuwa Team yenu bado ina weakness kubwa sana lakini unabeba akili za kina Ollachuga na Cash money kuanza kutanga Munabeba CL, EPL na makombe yote, nadhani muda ni mwalimu sahihi tupo hapa.
 
Wewe mngecheza pungufu mngepakibaiskeli kabisa, hujui mpira nyamaza kabisa wakongwe wa footbal wanapojadili mpira
Ivi huyo jamaa Alitaka Chelsea ifunguke baada ya Red card ili wafunge magoli mengi ndiyo ionekane kama Chelsea inajua mpira ama???

Mwambie ivi ukishakuwa pungufu lazima utumie Akili kwenye kudifence athawais utaogea magoli kama Arsenal. Pia mwambie Chelsea ni Bingwa wa ulaya anacheza kibingwa bingwa
 
Wachezaji waliocheza vizuri jana ni VVD
MATIP
FABINHO
ELLIOT
SALAH

Waliocheza kawaida
TAA

Walioboronga
Firmino
Mane
Robertson
Henderson

Alison Becker ni N/A kwasababu hakupata changamoto ya mashambulizi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom