Namuheshimu Sana Klopp.Infact Kwangu ndiye kocha ambae ameleta mafanikio makubwa zaidi Liverpool katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.Ndiye kocha ambae amerudisha ukubwa wa Liverpool,heshima ya Liverpool na ametuletea mvuto ambao unawafanya wachezaji nyota kabisa kutaka kucheza Liverpool.Makampuni makubwa kama Nike sasa yanafanya kazi na Liverpool..Hauwezi kutenganisha hivi vitu na Klopp...
Lakini Klopp huyu nae kuna muda anazingua Sana.Kitu kimoja cha uhakika ambacho Klopp anazingua ni kuendelea kutumia 4 3 3 wakati anazo sababu za msingi za kubadili mfumo.Injuries za mabeki, kushuka viwango kwa full backs na hata front three na kuwa na wachezaji ambao ni wazuri kwenye mifumo mingine kuliko 4 3 3.Hizi zilitakiwa kuwa sababu za kufanya mabadiliko ya shape ya timu kulingana na opponent.Takumi,Thiago,Keita,Gini,Origi etc ni wachezaji ambao wanaweza kuonekana flops kwenye mfumo wa 4 3 3 lakini wakawa wazuri zaidi kwenye 4 2 3 1 au hata 4 4 2.Sasa kwa nini usitumie huo mfumo ambao utakufanya upate asilimia zaidi ya 80 za ubora wa mchezaji na badala yake unaamua kukomaa na mfumo ambao unaupata ubora wa mchezaji yule yule kwa asilimia 20?Unafanya makusudi Ili aonekane ni flop?
Hata hao akina Mane ,Salah sometimes tunawaonea tu kuwakosoa.Wamecheza Sana mfululizo bila break na kocha hataki kutumia wachezaji wengine kwenye mifumo inayowasuit zaidi.Rotation ilitakiwa kuhusika Sana baada ya majeruhi huku mfumo ukiwa unabadilika mara kwa mara Tusingekuwa ambapo tupo sasa hivi..
Bado Hizi lawama zangu kwake haziondoi heshima kwake kama nilivyoeleza para ya kwanza...