Nilichogundua ni kwamba wapenzi wengi wa traditional top six za epl ukiacha City wanapenda timu zao zisajili average players ili wachezaji wao vipenzi waendelee kupata uhakika wa namba. Hapo hapo utakuta wanataka kushindana na City ambao hata team B inaweza kushindania ubingwa na ikatwaa.
Visingizio kikubwa ni kwamba eti top players hawawezi kukubali kuja kusugua benchi na kwamba eti hawawezi kubali kulipwa mishahara midogo! Maajabu haya!
Ukiangalia namna mastaa wa City wanavyosugulishwaga benchi na namna wanavyolipwa mishahara midogo kuliko hata amateurs wanaosugua benchi kwenye big teams zingine unabaki kushangaa.
Nadhani pia wamiliki wa hizi timu wanajua fika mitazamo hii ya mashabiki wao hivyo huchukulia hiyo kama fursa ya kusajili wachezaji wa viwango vya kawaida. Acha City waendelee kutawala ligi.
Hii huwa ni Mitazamo ya Top Members wa hizi timu kutaka Wazalendo/Wazawa wapate nafasi za uhakika kwenye Timu hivyo wana wabrainwash washabiki waliopo Nje ya Majiji yao kuamini ujinga wanaosema wao.
Mfano:-
Man Chester United:
Lukaku hakuwahi kupewa heshima Ndani ya United mpaka akaondoshwa na kutoa Nafasi kwa Rashford mpendwa wao, Sasa mtazame Rashford anapewa sifa na usishangae akawa knighted na kuitwa
Sir Marcus Rashford.
Liverpool:-
Hapa kuna washàbiki walikuwa blindly fooled kwa kuaminishwa eti Hakuna Mchezaji Mkubwa yoyote atakarkubali kusajiliwa Liverpool mpaka Wastaafu hawa waliopo! Ujinga huu uliaminiwa na Wengi.
Pia wakazusha Propaganda nyengine kuwa Don't disturb front 3 ndiyo waliotupa makombe, Don't disturb our Midfielders ndiyo waliotupa makombe.
Hatimae tukaanza kuletewa kina Adrian, Ki-Jana, Tsimikas, Minamino , Dvies na takataka nyingi tu! Wako wapi leo? Wametusaidia nini?
City anaumia KDB na Laporte lakini moto wanaouwasha utadhani hakuna kilichotokea! Unadhani kwanini? Hawakuamini kama ukimleta Mahrez, Rodri, Diaz utadisturb kina Sterling, Bernardo na Stones.
Sisi kwetu daima tununue Beki mwenye kiwango Kidogo kuliko Gomez kama vile Kabak na Devies ili Gomez akipona asiwe disturbed, tungemnunua Upamecao angedisturd nafasi ya Gomez.
Kwa kweli Watu wana Mindsets za ajabu sana.