Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Sio upangaji tu mkuu hata uwekezaji ni muhimu liverpool walikuwa bora sana baada ya kuwekeza klopp akasinzia alisahau kama aliwekeza kufikia mafanikio aliyopata msimu uliopita kule kwa pep tumemsahau kabisa laporte wachezaj wake wa gharama na quality.
Tatizo Klopp aliwaaminisha wenye timu yeye ni miracle worker na kikosi anachopewa yupo tayari kukomaa nacho mpaka mwisho matokeo yake hana like for like sub kwneye maeneo muhimu kipindi kama hiki tuna majeruhi...

Unajua wakati mwingine usisubiri yakukute ndio ujipange.. Tazama kilichomkuta Manchester City na kukosa ubingwa wa 2019-2020 ilikua hivi kumuachilia Kompany bila kusajili mbadala wake matokeo yake akaja umia Laporte na Pep akajaribu kukomaa na Fernandiho kutoka DM na kumrudisha CB ambapo alichemka vimbaya mno na mwishowe tukachukua ubingwa.. Hili ilitakiwa iwe somo kwa Klopp wakati wanamwachia Lovren endapo wangesajili upya CBL immediately.. Sasa tunakuja kupata majeruhi Matip, Gomez na VVD imagine wewe ndio kocha huna plan B ya hap wachezaji zaidi ya kuchukua mchezaji wako bora pale Kati Fabinho kumrudisha CB sasa pengo la Fabinho nani wa kulizimba hayupo ndani ya Anfield..

Tukafika January 2021 badala wenye timu yao waingie sokoni chap na kumsapoti kocha walisubiri mpaka Klopp awatupie dongo ndio waka react na huku wameleta ma amateur playere sio proven na mpaka mida hii Klopp hajashawishika nao kuanza hata gemu moja..

Ki ukweli Klopp alivyowachana hawa wamiliki nilimwelewa yaani unaweza kuta pale chaguo lake ni Allison na VVD mbali wengine ni chaguo la wenye klabu yaaani kuna vimaneno fulani alisema nikabakie kutoa macho..

Kwa hio hayo ya kumsaidia kujenga kikosi sijui yataanza lini kwa hawa FSG kwani jamaa wanategemea maajabu ya Edwards na Klopp kuwavusha salama..

Everything has a beginning and an end and many of this current players have reached thier end we need new hungry blood...

YNWA
 
Mkuu kwa mimi nilichokiona leo ni kwamba hatuwezi kufunga mipira ya kona ,mipira yote ameruka stone,hapo angekuwa vvd yangekuwa magoli hayo.

Hakuna mruka vichwa kama ndio hivyo unakuwa unategemea magoli ya aina moja tu,ambayo sio magoli ya kona .
Last season we had a league high ya magoli kutokana na kona na mipira ya adhabu na hii ilichangiwa na VVD kwani his aerial presence is scary kwa wapinzani...

Msimu huu tumepiga kona 150 EPL tupo nyuma ya Manchester City lakini sasa magoli hatufungi yaani hata Chelsea wenye kona 145 wana magoli kuliko sisi ina maana pengo la VVD na Matip kwneye mipira ya kichwa linaonekana wazi wazi...

Tumepiga shot on target 127 huku tukiwa na magoli 44 ambayo ni EPL namba 2 lakini tazama magoli hayaji ina maana hatupo clinical golini wala kwenye kona ama mipira ya adhabu...


Klopp ana kibarua kweli kweli..

YNWA
 
Mwanzoni msimu ukikaribia kuanza klopp alisema WE ARE GOING TO ATTACK THE TITLE,sasa ndio nimemuelewa
 
1. We are unbeaten at anfield since 2017- kilichofuata naona hata aibu kusimulia
2. Pep has never won a game against klopp- kila kitu kina mwanzo na mwisho maana kumbukeni hata pep hajawahi kumfunga lwandamina

Kama kuna rekodi yoyote ambayo bado mnadhani inasimama tuwekeni wazi tuifanyie kazi tafadhali.
 
Kusema ukweli siamini kama Alson alikuwa golini leo!
Kawapa bao zote 4 Man City,bao zote nne.
Bao la kwanza ndiyo limeniuma zaidi,mpira ule ulikuwa hauna hata nguvu,alikuwa analala anainuka nao!
Hata ukiona reply TAA na Robbo waliisha fungua na Fabihno aka relax maana walikua kipa anauokota tu

Bao la 2 na 3 ni aibu sana aisee
La 4 kakwepa mpira

Lkn tumefungwa WOTE,tunajipanga
Wewe leo kumlaumu Allison ni sawa sio? Ila wenzako wakishusha tuhuma kwa Hendo unaanza kuwaita wao sio halisi? Leo na wewe umetuhama wanamshikamano? Maana sisi hatuwanangi wachezaji.
 
  • Bro Henderson is a leader.
  • Bro Henderson ndiyo chachu ya ushindi wetu.
  • Bro Henderson ndiyo anayetupa Makombe.
  • Bro Mechi zote tunazofungwa huwa Henderson hajacheza.
  • Bro blah blah blah blah!

UHALISIA:
  • Kipindi tuna kikosi cha ushindi Henderson kila akimulikwa na Camera alikuwa anafoka ili awaaminishe Watu Kuwa yeye ni kiongozi muongeaji. Sasa Timu ipo kwenye wakati mgumu, Haki ya nani unaweza kuuliza 'ivi uwanjani hamuna Captain leo'? Ile Leadership yake katika kipindi hichi kigumu imeenda wapi? Si atuvuushe basi angalau andelee kuwapokeae Wachezaji waache ujinga.
  • Ile kauli ya Chachu ya ushindi si ndiyo tuione sasa! Alikuwa atuthibitishie kuwa VVD si lolote kuhusu ushindi bali yeye ndiye anayetupa matokeo.
  • Kama HENDO ndiye anayetupa Makombe nadhani msimu huu wa EPL umeshatoa majibu.
  • Tulikuwa kila siku tunawekewa virekodi uchwara eti akicheza HENDO hatufungwi! Dadeki ndiyo tunafumuliwa ndani ya Anfield kama Wendawazimu vile.

=> Timu ikishinda sifa zinakwenda kwake, ikiboronga ziende kwa nani??? Ili kulificha hili walijaribu kumtoa kafara Salah kumtupia lawama zote za timu kufanya vibaya.
 
Mkuu kwanza leo my best Liverpool player kwenye hiki kikosi Allison kafanya blunder za ajabu yaaani haikumbaliki kipa wa level hizi kweli afanye vile lakini sasa Soka ni mchezo wa makosa na ukayafanya dhidi ya Pep bila shaka utaumia...

Technically Allison kauza hii gemu..

Unavyokua vile unaifanya timu nzima icheze kwa wasiwasi mno..

YNWA
I dont blame Allison , in my side i think no sabotage for our Club is what he did but sabotaging Red devils is what he did which in the end is an act which i commend

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Nimeangalia ratings za Liverpool Echo wamemrate Jones 8/10 na kuandika comment hii 👇

Curtis Jones 8

Brilliant tracking back denied Foden first half and always looked to get Liverpool moving forward. Very harsh to be subbed

👉 Wamemalizia na neno 'Very Harsh To Be Subbed'.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom