For my very personal views, wachezaji baadhi walikua wauzwe kabisa ama waachwe tulete watu wa kazi ili kutoa gundu la miaka 30.
Divock Origi, toa magoli yake ya nusu fainali na baadhi ya ndondokela za hapa na pale, nadhani wengi wanamwona kama mr lucky-man hivyo wamemwongezea kandarasi ndefu. Japokuwa bahati ipo ila haipo kila siku for a player who cant even break into man u first eleven( aiming at top 4 spots) kwanini abaki kwetu tulio na harakati za kutoa gundu la miaka 30?
2. Gini wiljinaldum, mmatumbi mwingine wakufyekelewa mbali alikua huyu, playing either 10/8 bado hana madhara kabisa katika final third ya adui(assist/goals) unamwacha fekir aende betis kwa 30m£ unambakiza huyu mr slow guy halafu unakuja kutudanganya epl tutaipata tu. Madhara yake tunayapata kwenye mechi wanazorundikwa hawa wamatumbi pale kati gini/henderson ama gini/milner ama henderson/milner mfano mechi ya jana tunakosa kabisa creativity from the centre hivyo kuigawa timu vipande viwili bila kiunganshi kati.
3. Henderson, nitalia na aliyempa kitambaa cha unahodha, jamaa ukitoa kitambaa cha unahodha tu, pale liver sidhani kama atavuka dirisha hata moja hajasukumizwa nje. Huyu inatakiwa awe anambebea viatu tanguy ndombele pale tott.
4. Milner, hata milner??? Ndiyo, uwepo wake umefanya tusiongeze mashine moja kijana kijana hapo kati. Our versatile player, yes our versatile player 33yrs old. Umri umekwenda kasi akiwa kaishiwa plus pumzi cha kushangaza itafika january ndio atakua tegemeo letu either rb or lb. Mpaka hapo city wanaanza kushona suti za ubingwa hata kuwe na gap la point 12.
NB kwanini hatujanunua central striker wa hata goli kumi tu za msimu atuongezee kwa kina mane na salah? Je tumekubali origi ndio awe back up ya mane?(refer yday game) tumeshindwa kweli kumpata flexible winger atakaye weza toa kashkash pale mbele kweli???? TUNAUTAKA UBINGWA KWELI?