Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Na Mimi mkuu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]hii timu acha kabisaa wana roho saba
 
Kwenye mpira hukosi cha kujifunza kwa mpinzani kama anafanya vizuri.

Mara nyingi hizi timu kitu cha kwanza ni kupata kocha sahihi, mwenye falsafa inayoendana na timu husika.

Atleast kwa sasa Liverpool kuna kocha ambaye anafanya kitu unayaona malengo yake, na hata kama hatujachukua kombe lakini unaona tofauti ya msimu na msimu.

Shida kubwa kwa sasa ni uvumilivu, ninyi Man Utd hili limekuwa tatizo kubwa kwenu. Liverpool amepita sana huko lakini angalau tulikuwa tunawapa muda mrefu makocha tofauti na nyie.

Kwa hiyo hata muda wa kocha kutengeneza kikosi anakuwa hana, mlivyomwondoa Van Gaal mkamchukua Mourinho ndiyo siku nilipojua sasa mnapokea kijiti chetu.

Hata huu mkataba wa OGS mimi siukubali kiviile, maana kocha mwenyewe anaonekana anasafiria nyota ya Fergie na ule ulegendary, yalitukuta tulipompa timu King Kenny, na najua muda si muda huyo mtamwondoa pia.
 
Nani anapenda kutembea uchi kariakoo?[emoji23][emoji23]
Liverpool ipo juu mawinguni.

Yani wewe katika Wachawi ni Namba moja! Yani kwenye Prematch Liverpool ipo chini, Lakini kwenye Post match Liverpool ipo juu. 😀😀

Lakini nitakusubiri tu pale Kariako kikubwa nikulia Timing tu nijue kama utapita Sokoni au Mtaa wa Nyamwezi.
 
Mkuu kwema lakini? Mmejiandaaje na game ya leo kwa huyu Professor 👇😀

View attachment 1090529

Mkuu vipi naona Huyu Professor wako kaamua kujiunga na Kundi la Kina Professor Lipumba?

Jana kaamua kudhihirisha kuwa yeye ni Jogoo la Shamba linawika Nuo Camp tu, Nje ya Hapo anakuwa Mtetea.
 
Maana halisi ya mtaka yote kwa pupa hukosa yote ni kwa kuku wa kishingo mwaka huu..Liverpool 0-4 Barca...

Next match Briton anamwagiwa magoli kama njugu...kilichobakia kwenu ni KULIIBA TU hakuna namna mkuu...

Tulichokifanya ni kuokoa Aibu ya Kufunga Mwaka!
Hivi Barcelona kwenda kulichukua Kombe Ndani ya Barnabeu unadhani ingelikuwa ni jeuri gani hii mtakayowafanyia Real?
 
Arsenal pigeni Valencia, tupunguze mdomo wa La Liga vs EPL kwa muda.

Maana jamaa wanatunyanyasa sana washabiki wa EPL.

Ila naona kabisa upepo unaanza kubadilika taratibu.

Ni Ronaldo na Messi ndiyo Walioinyanyua La Liga, Lakini Kabla ya Hawa Wataalamu Wawili La Liga ilikuwa Shit League with nothing special.

Sasa Ronaldo is gone, Messi anaelekea 32years! Nadhani karibuni watarudi walikotoka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…