Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

The time ambayo City alikuja Anfield alikuwa na target ya droo, sisi ndo tulihitaji ushindi zaidi ingawa matokeo ya droo hayakuwa mabaya.

This time City desperately needs to win, while a droo to us is very favorable.

Kwa hiyo Klopp ataweka kikosi ambacho in every means ni kuhakikisha hatufungwi, hatahangaika kutafuta ushindi, ila ukija itakuwa shangwe.
matokeo ambayo Alhamisi tunayahitaji ni mawili tu adiha ushindi or droo.....

Pep will demand th mother of all cheering from his fans ila sasa hua wanachoka haraka kupiga kelele after 20 minutes kama goli hamna hawatasikika...

kiukweki Anfield we are lucky maana mashabiki hua na timu full kushangalia kuanzia mwanzo hadi mwisho wa gemu...hii inatia morale kwa wachezaji sana tu...
 
DullyJr , Ollachuga Oc na Mwenyeji wenu ambaye ni Mshabiki wa Liverpool ipogolo

Mtaongea Mengi Mwaka Huu!

Sasa Mumeacha Kuzungumzia Mpira Munafanya Mashambulizi kwa Washabiki Wa Liverpool.

Mimi Na Wataka Makombe Wenzangu Hatujutii tuliyoyafanya tokea Msimu Wa Mwanzo Wa Klopp! Mambo tuliyoyafanya ni:

1) Tulimkataa BENTEKE tukashambuliwa na kuitwa Wasiliti, lakini hatimae Klopp kamuondoshwa.. Kwahiyo Klopp kaungana na sisi kwenye usaliti Wa Timu.

2) Tuliwakataa Sakho, Moreno, Klavan na Lovren kuwa si Mabeki ni Wabovu wanatufungisha! Tukaitwa wasaliti! Hatimae Klopp Kawaondosha Sakho na Klavan, Na Moreno na Lovren kawaeka pembeni! Lovren sasahivi anacheza kwasababu wenyewe GOMEN na MATIP ni injury.
Kwahiyo hapa pia Klopp Kaungana na sisi katika usaliti.

3) Tuliwakataa Mignolet na Karius na tukasema ni Wabovu wanatufungisha! Tukaitwa wasaliti! Kwahiyo Klopp kaungana na sisi katika Usaliti kwa Kumleta ALISSON.

4) Tulilia sana kuwa Kiungo Mkabaji halisi ni FABINHO na si HENDERSON! Tukaitwa Wasaliti! Sasa Klopp ameshirikiana na sisi kwenye Usaliti kwani Anamchezesha FABINHO tuliyempigia kelele.

Hao wote tuliowalilia hapo juu tuliambiwa Kuwa sisi Hatujui Soccer Management.

Kwahiyo Kitendo cha Klopp Kutompanga Mignolet golini, Na Kutomchezesha Moreno beki 3, na Kuwaondosha Klavan na Lovren kwenye Beki 4 na 5, na kumchezesha FABINHO namba 6! Ni kwamba na Klopp pia Hajui tens Soccer Management!.

Hivi mpaka leo Kikosi Hichi kingelikuwa

FIRMINO - BENTEKE - MANE

LALLANA - HENDO - GINI

MORENO - KLAVAN - LOVREN - CLYNE

MIGNOLET
Hao waliokuwa Wakituita Sisi kuwa NI WASALITI na HATUJUI KITU leo hii wangeliyaona haya?

Au hawajui kuwa PRESSURE kutoka Dunia Nzima za WASHABIKI KAMA SISI LIVERPUDLIANS DIE HARD FANS ndiyo kilichomfanya Klopp akawanunua kina ALISSON, VVD, ROBERTSON, SALAH, XHAQIRI, FABINHO na KEITA ?

Kwa Usaliti huu Wa Kutaka Mafanikio basi bora Niwe Msaliti Siku Zote.

Na Kwa Upenzi Wa Kukubali Vipigo Kama Misimu Miwili na Nusu ya Klopp iliyopita kisa tu eti Niwakubali Wachezaji Hata Kama Wabovu! Basi Sitokuwa na Upenzi huo.

Sina cha kuongeza hapo chief...
 
Ni kweli mumejenga timu na matunda yanaonekana. Apo Klopp anahitaji pongezi za kutosha

Kwanini mliwanunua wachezaji ambao hamkuwa na future nao? Moreno mpka analalamika ubaguzi wa klopp unazani hilo liko sawa??

Sent using Jamii Forums mobile app

Klopp siyo mbaguzi kwa Moreno, bali uwezo wa Moreno ni mdogo when compared to Robertson, na kwa kipindi tulichopo no room for errors.

After all Klopp alimbeba sana Moreno.
 
Mbona huzungumzii kina FABREGAS kupigwa benchi so FABREGAS alinunuliwa wa nini??

Kila kitu kina mahala pake sahihi katika muda sahihi

Yaan kwa akili yako Moreno acheze Robertson apigwe bench ww utakua punguani kias gani???

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao sakina Fab & its company wana gemu zao za katikati ya wiki.

Sasa Klopp kawabagua kabisa akina Sturrigde, Moreno ...hakuna gem hata moja wanapangwa.

Watapataje uzoefu kama mambo ndo hayo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alim'beba vipi mkuu.? Kusingekuwa na malalamiko kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo Moreno bado yupo kwenye denial kuwa hazidiwi na Robertson, ndiyo maana unaona analalamika but ukweli ni kuwa AR26 is way better than Moreno by a MILE!

Ninaposema alimbeba sana nilimaanisha Klopp was supposed to buy a left zamani but almvumilia Moreno hata baada ya kuwa keshamnunua AR26.
 
Hao sakina Fab & its company wana gemu zao za katikati ya wiki.

Sasa Klopp kawabagua kabisa akina Sturrigde, Moreno ...hakuna gem hata moja wanapangwa.

Watapataje uzoefu kama mambo ndo hayo??

Sent using Jamii Forums mobile app
kina moreno,sturridge na mignolet mbona walipangwa kwenye carabao dhidi ya chelshit na badala ya kupambana ili kumconvice coach wakaboronga tukatolewa sasa kama walipewa nafasi ya kuonesha kuwa wanauwezo wa kuichallenge first 11 ya klopp wakashindwa wewe ulitaka wapangwe kwenye epl na uefa ili tuwe tayari tumeshatolewa uefa na huku epl tuwe tunastruggle kufight nafasi ya 6?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Club zao zinaongoza ligi na wananafasi ya kutwaaa makombe kila mwaka point yako ni ipi mkuu?
Point yangu huko wamekua sehem ya mafanikio wakati Liver walikua ndo mafanikio yenyewe.

Labda unambie wanapata heshima kama waliokua wanaipata Liverpool.

cc radika
 
Mbona huzungumzii kina FABREGAS kupigwa benchi so FABREGAS alinunuliwa wa nini??

Kila kitu kina mahala pake sahihi katika muda sahihi

Yaan kwa akili yako Moreno acheze Robertson apigwe bench ww utakua punguani kias gani???

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu wewe hujamwelewa huyu jamaa wa chelshit yeye alitaka hao kina moreno wacheze ili uefa tayari tuwe out na epl tuwe nyuma yao kama vile walivyotutoa carabao sababu ya haohao kina moreno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point yangu huko wamekua sehem ya mafanikio wakati Liver walikua ndo mafanikio yenyewe.

Labda unambie wanapata heshima kama waliokua wanaipata Liverpool.

cc radika
Hawawez kupata heshima kama walivyokuwa wakipata liverpool sababu hizo timu zimewakuza kisoka kule wamefata mafanikio na pesa kama ronaldo tu na manchester united madrid hakupata heshima kama tuliyompa
 
kina moreno,sturridge na mignolet mbona walipangwa kwenye carabao dhidi ya chelshit na badala ya kupambana ili kumconvice coach wakaboronga tukatolewa sasa kama walipewa nafasi ya kuonesha kuwa wanauwezo wa kuichallenge first 11 ya klopp wakashindwa wewe ulitaka wapangwe kwenye epl na uefa ili tuwe tayari tumeshatolewa uefa na huku epl tuwe tunastruggle kufight nafasi ya 6?

Sent using Jamii Forums mobile app

Umemjibu Vyema!

Anajifanya Kuwa kasahau Kuwa Hao anaowatetea ndiyo waliowapa wao Mdomo kwa Kututolesha Kwenye Carabao.

Now wanawapigia debe tuwachezeshe kwenye EPL ili tuje tupogwe Mkono na Man City.

Bora Hata waondoke lakini hatuwezi kuwapanga tena wakatuulisha kama walivyofanya kwenye Carabao.
 
Hao hawajui maana ya ushabiki, wanataka mchezaji abaki tu timu moja na akiondoka wanamchukia mazima na kufikia hatua ya kumuombea mabaya.

Kama kupata majeruhi, aanguke afe....

Sent using Jamii Forums mobile app
nafikiri hatupo serious hadi tuwaombee majanga ya kuwa majeruhi bin-adam wenzetu sema tu tunaongea kiushabiki tunaelewa pia kuwa kuna factor nyingi zinazofanya mchezaji kuhama timu na mojawapo ni maslahi mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom