Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

My only concern kwa Leo Ni Huyu VVD Kuwa hatocheza!!
Kwani Anatusaidia Sana Kucheza Set-Pieces .....
Akiwa hajacheza basi Ni rahisi sana Kwetu Kufungwa Kwa Set-piece.
 
Umechambua vzr sn lkn kuna kitu kimoja ambacho Pellegrin alikifanya dhidi Ya Chelsea ambacho wewe haujakigusia kabisa.

Ktk game Ya Chelsea na wagonga nyundo, kile kitu walichofanya Hammers ni kuhakikisha mipira haifiki Kwa Giroud. Walikata passes zote na kuhakikisha Giroud hachezi mipira ambayo Kwa mfumo wa Sarri Giroud ndio huwatengenezea kina Hazard Move pamoja na Willian na kiungo mshambuliaji wa kati. Giroud mpk anapumzishwa aligusa mpira mara 24 na mara zote ilikua mgagade mgagade kitu ambacho alishindwa kuwachezesha wenzake.


Ikabidi Morata aingie. Km Unakumbuka Hazard na Willian wakatanua wakawa wanatumia Cross, nayo hiyo mipira ikawa mizuri na kuleta matumaini ya kupata goli lkn muda ulikua umekwisha. Ata hivyo pamoja na hiyo mipira ya Korosi na kutumia wingers bado hammers walikua wabishi kutoka ndani ya Box lao na walikua wanakata mipira yote iliyokua inaingia humo ndani Ya box.


Sasa mkitaka kufanikiwa kuwapoteza Chelsea ktk hili, labda mcheze deep Ndani ya boxi yenu kitu ambacho ni kz sn kucheza Kwa dk90.

Jana Klopp amelia na mfumo au mpira wanaocheza siku hizi Chelsea, mpira wa ku dominate. Na alisema mara zote walipojaribu kukaa na mpira haikua rahisi. Waliupoteza na Chelsea kuwaletea matatizo.

Mtazamo wangu, Liverpool inapaswa jumamosi ili kukabiliana na Chelsea vzr. Swala si kumuangalia Hazard. Inatakiwa Team work ya nguvu na high pressing. Muanze kuikaba Chelsea juu kabisa ktk eneo lao na kuhakikisha mnatibua mipango yote ya Chelsea. Na wakati huo huo viuongo wenu na mabeki wenu wawe makini sn na counter attacks maana mkionekana mko juu sn basi Kante na Hazard na Willian hawa watakua na kz moja tu ya kuwashambulia Kwa kasi sn Kwa usaidizi WA ustadi wa mpiga pass mzuri Jorghinho.

Liverpool ingelikua na Oxlander mzima na Wijnaldum hapo kati ningesema hawa watu watawaokoa.

Lkn ni bora kumchezesha Wijnaldum hapo kati na Miller wanaweza kuwasaidia sn kuliko kamanda Henderson.


Ukitaka kuidhibiti Chelsea, ikabie juu kabisa na uhakikishe Kante na Jorghino hawapati utulivu kabisa.
Hahaha mkuu naona unawapa mbinu.

Lakini wanasema mbinu za kupewa hazina nguvu kama zile unazotengeneza munyewe.
 
Halafu Mimi Sipendi Mtu aniQuote Kwa Mawazo Ya Wengine. Mimi post zangu Nazihakikishia Kuziandika Kwa Mawazo Yangu Mwenyewe Bila Ya Kufuata Mawazo Ya Mtu mwengine na Ndiyomana Hunikuti Kunadia Mechi Kuwa Lazima Tutashinda, Wala Hunikuti Kutangaza Kubeba Kombe lolote Kwani siamini Ramli Katika Mpira Bali Naamini Ushindi Baada Ya Dakika 90 na Kombe Mwisho as Ligi.

Kwahiyo UnapoQuote Watu Wanaojisifia Ni Bora Usinishirikishe.
Hao wenzako wamehakikisha leo wanashinda. Sasa labda na wao watakuwa uwanjani ..em ngoja tuone..
 
Jumamosi itakuwa Ni Siku Ngumu Kwa Upande Wa Mashabiki Wa Upande Mmoja ambao Mimi binafsi Sijaujua Ni Upi.

Kwani Hii Mechi Kwa Matokeo Yoyote Yale Haitamwacha Mtu Salama.

√ Timu itakayofungwa itakosa amani na Washabiki wake.

√ Mechi ikiishia Sare Timu ya Nyumbani itakosa amani na Washabiki Wake Kwa Disadvantage ya Kukosa Points 3 uwanja Wa Nyumbani.

Ni Kizaazaa tu Siku hiyo.
Kama wewe ulivyokosa raha baada ya kukosa zile point tatu ulivyokuwa nyumbani.

Hata mimi bado sijajua ni upande upi mpaka sasa. Mimi na wewe hatujui..!
 
Hahaha mkuu naona unawapa mbinu.

Lakini wanasema mbinu za kupewa hazina nguvu kama zile unazotengeneza munyewe.
Ha ha ha na leo nawaaongeza kitu kingine. Kuna uwezekano mkubwa sn pale kati Klopp akawaanzisha Henderson, Milner na Wijnaldum ili kuweza kuwin battle la viungo amabalo yeye anawaita viungo wa Chelsea kua wanakimbia km gari za Formula One.


Yani liver watahahakisha hakuna kabisa utulivu hapo kati.
 
Huu "Uingereza" tabu kweli kweli! Hendo wamemuanzisha huko kama kawaida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom